Waziri wa Fedha Punguza Jazba

Waziri wa Fedha Punguza Jazba

Jana kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku niliona waziri wa fedha alipofanya ziara ya kushutukiza pale bandarini (dhow). Kwa kweli sikupendezwa jinsi waziri alivyokuwa akiwatuhumu watumishi wa TRA pale bandarini kuwa kiini cha kushuka mapato ya ukusanyaji za forodha.
Kwasasa kiuchumi hapa nchini kununua na kuuza bidhaa kumeshuka kwa kiasi kikubwa na hiyo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kushuka kwa kiasi kikubwa, ndugu waziri kwanza ukiwa waziri wa fedha na uchumi lazima ufanye utafiti nini kilichosababisha katika kipindi chako kama waziri iwe hivyo. Wafanyabiashara biashara wengi kwasasa wamekimbilia kupitisha mizigo Zanzibar kwanini? Unapotoa vitisho utawafukuza watumishi waliopo pale bandarini kwasababu ya kutokusanya kodi utafukuza wangapi?
Lazima Mheshimiwa Waziri ukae na wadau ujue tatizo liko wapi, kwasasa circulation ya pesa hapa nchini ipo chini sana na hilo ndio tatizo kubwa.
Leo ukimwondoa mfanyakazi wa TRA mwenye uzoefu na kumleta mfanyakazi mwingine kutoka chuoni asiye na uzoefu usitegemee kama kutakuwa na mafanikio. Kwasasa watumishi wote waliopo kazini wapo makini sana kwa masuala ya rushwa.
Huyo waziri mwenye PhD, naye ni mwanafunzi mbumbumbu kiasi fulani.
Mwanzoni mwa mwaka huu aliulizwa kwa nini biashara Zaidi ya 2000 zimefungwa , jibu lake lilikuwa nayeye hajui!!!
It was remarkable!!
Leo bishara Zaidi ya 8,000 zimefungwa nafikiri bado hajui kwa nini!!!
 
Huo ushauri wape waume zako hapo ufipa .

Waambie wajenge ofisi ya chama
Tatizo Elimu Elimu mtu anapotoa wazo badala ya kujibu hoja ndio matusi tu..
Wewe na familia yako we are sailing in the same boat.
 
Kadri siku zinavyokwenda yanazidi kushuka si wanataka watu waishi kama mashetani. Mashirika yakipunguza wafanyakazi wao wanakenua meno wanafurahia wanajua tunanyooka, makampuni yakifunga kampuni zao na wafanyabiashara wakifunga biashara zao wanafurahia wanajua wanatunyoosha. Wanasahau kua mapato yanapungua maana hata PAYE zinapungua pamoja na kodi mbalimbali
Ni bora wangewezesha kwanza biashara/ajira mpya zinazokidhi matakwa yao ndio waziue hizo za "Wapiga dili"...sijui nani aliwaambia kuwa kwa kuua "Wapiga dili" na waliokuwa wanawategemea wataendelea ku survive.
 
Ukweli mchungu, sio vizuri kila siku kumtembelea mambo yale yale
 
Unatetea kibarua? TRA wale wanao verification wanapenda sana kuonea waleta mizigo. Akili yenu lazima muiweke kwenye Business oriented,Competitive analysis na Customer expectation sio mnakurupuka tuu. HS Code zenyewe zinawapa shida mmekariri mnapelekea Tariff classification kuwa ya kuumiza.
What kind of person mnaotaka kufanya kazi za verification Hakuna mfanyakazi anaweza kufanya kazi kwa kutishwa. Mpe uhuru wa kufanya kazi. Watumishi wa TRA wamekuwa terrorized kwa kutishwa kila siku. Wafanyabiashara pia wanatishwa kila siku. Waziri ana haki ya kuwa na mikutano ya ndani na watumishi wa wizara bila kuwatisha ama kuwafokea. Mheshimiwa Waziri Mipango inabidii awatafute akina Mramba na Mgonja wampe Siri ya mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kipindi chao.
 
Hivi ni urasimu ndo sababu pekee inayo weza kuwakimbiza watumia bandari?
Mimi nimeoana hiyo,wewe ongezea na mengine.
kuna vitu vinahitaji pesa ili vifanyike
lakini uzembe na urasimu unaweza huitaji hela ili kuvikomesha.

Uzembe unaweza kusumbua wateja wakakuhama
ukaanza kutafuta mchawi wakati
umejiloga mwenyewe,sasa unapotafuta
dawa unaanza na mambo mepesi,
katika hili,unaanza kushughulikia na wazembe
na wenye urasimu ndo unaendelea na miundombinu
ambayo bila pesa huwezi kuibadilisha.
 
Sio kila kitu kukosoa tu Waziri ni wajibu wake kusimamia shughuli chini ya wizara yake na halafu ukiangalia wizara ya fedha ndio kama moyo wa serikalin.

Pia kumbuka watanzania tumezoea kukumbushwa hata majukumu yetu.

All in all yupo sahihi na ajavunja katiba wala sheria za nchi anatekeleza wajibu wake.
 
~~~>>>>Huyu Waziri hivi ameshamaliza kufunga vutuo vya kuuza mafuta visivyo na mashine za kutolea Risiti???

Hii nchi kila siku viongozi wanaangalia jambo litakalowafanywa watokee kwenye media .....

Babu aliniambia

"Baba ukiwa mkali sana bil sababu za msingi, watoto wakikusikia unakuja hata kama ni Usiku watafungua ng'ombe wajifanye wanaenda kuchunga"

Lengo ni kukudanganya uone kuwa wako bize

Huyu Waziri Mipango kwa kuogopa kutumbuliwa anajifanya anafanya kazi lkn ktk Uhalisia hakuna kitu
 
Haya ni matokeo ya kuhamisha fixed deposit accounts zote na kuzirudisha central bank,hali inayopelekea mabenki kushindwa kukupesha ipasavyo na hatimaye importation ku drop kwani wafanya biashara wengi wanategemea mikopo ili kuipa nguvu mitaji yao.Nchi imefikia stage mtu anapigwa bunduki ili aporwe 2 million lakini waziri wa fedha anajifanya haelewi tatizo nini,ilihali hata ngumbalu asiye na elimu ya uchumi anajua kwamba mduara wa uzungukaji wa pesa umepungua ukubwa(The collapse of maney flow circle). Na haya ndio matatizo ya nchi za Kiafrika watu wanajibu changamoto nzito za kitaifa kwa siasa za mchangani.Waziri tuheshimu wa Tz acha siasa uchwara za kuwaongopea watu kuwa hali ngumu bandarini inatokana na wizi.
 
Mfa maji haishi kutapatapa Mkuu. Kamuachia dhalimu auvuruge uchumi kwa sera zake uchwara kwa mfano kuondoa 1 trilioni shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini. Sasa makusanyo ya kodi yamepungua sana na kibarua chake kiko kwenye hati hati kuota magugu hivyo anatafuta mchawi wa kumnyooshea kidole. Wa kumnyooshea kidole ni huyo aliyemteua kwenye huo wadhifa wake.

Jana kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku niliona waziri wa fedha alipofanya ziara ya kushutukiza pale bandarini (dhow). Kwa kweli sikupendezwa jinsi waziri alivyokuwa akiwatuhumu watumishi wa TRA pale bandarini kuwa kiini cha kushuka mapato ya ukusanyaji za forodha.
Kwasasa kiuchumi hapa nchini kununua na kuuza bidhaa kumeshuka kwa kiasi kikubwa na hiyo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kushuka kwa kiasi kikubwa, ndugu waziri kwanza ukiwa waziri wa fedha na uchumi lazima ufanye utafiti nini kilichosababisha katika kipindi chako kama waziri iwe hivyo. Wafanyabiashara biashara wengi kwasasa wamekimbilia kupitisha mizigo Zanzibar kwanini? Unapotoa vitisho utawafukuza watumishi waliopo pale bandarini kwasababu ya kutokusanya kodi utafukuza wangapi?
Lazima Mheshimiwa Waziri ukae na wadau ujue tatizo liko wapi, kwasasa circulation ya pesa hapa nchini ipo chini sana na hilo ndio tatizo kubwa.
Leo ukimwondoa mfanyakazi wa TRA mwenye uzoefu na kumleta mfanyakazi mwingine kutoka chuoni asiye na uzoefu usitegemee kama kutakuwa na mafanikio. Kwasasa watumishi wote waliopo kazini wapo makini sana kwa masuala ya rushwa.
 
Sio kila kitu kukosoa tu Waziri ni wajibu wake kusimamia shughuli chini ya wizara yake na halafu ukiangalia wizara ya fedha ndio kama moyo wa serikalin.

Pia kumbuka watanzania tumezoea kukumbushwa hata majukumu yetu.

All in all yupo sahihi na ajavunja katiba wala sheria za nchi anatekeleza wajibu wake.
Yupo sahihi mara kutisha wafanyabiashara mara kutisha watumishi wa TRA ? Unafahamu kuwa kwa structure ya kazi Waziri wa Fedha ni mtu mkubwa kwani kuna Kamishina Mkuu wa TRA na Kamishina wa Forodha na hawa wote ndio Waziri wa Fedha anatakiwa ku deal nao. Kisheria waziri kupitia viongozi hapo juu alitakiwa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika kama wamefanya makosa. Uchumi wa nchi haujengwi kwa vitisho ama kufukuza.
 
Nahisi ukuangalia vizuri iyo taarifa ya habari,mimi nimeangalia alikuwa anampa kamishna wa forodha maelekezo na jinsi ufisadi ulivyokisiri pale, sasa wewe ulitaka afanyaje?
 
Haya ni matokeo ya kuhamisha fixed deposit accounts zote na kuzirudisha central bank,hali inayopelekea mabenki kushindwa kukupesha ipasavyo na hatimaye importation ku drop kwani wafanya biashara wengi wanategemea mikopo ili kuipa nguvu mitaji yao.Nchi imefikia stage mtu anapigwa bunduki ili aporwe 2 million lakini waziri wa fedha anajifanya haelewi tatizo nini,ilihali hata ngumbalu asiye na elimu ya uchumi anajua kwamba mduara wa uzungukaji wa pesa umepungua ukubwa(The collapse of maney flow circle). Na haya ndio matatizo ya nchi za Kiafrika watu wanajibu changamoto nzito za kitaifa kwa siasa za mchangani.Waziri tuheshimu wa Tz acha siasa uchwara za kuwaongopea watu kuwa hali ngumu bandarini inatokana na wizi.
Wizi wakuporwa pesa unataka kusema umeanza kipindi cha utawala huu?

Mimi navyoona utawala huu umedhibiti sana uporaji wa pesa kuliko tawala zilizopita,inatakiwa kusema ukweli kwenye ukweli sio kupotosha na unapotosha ili iweje? Na kwanini unamasisha importation badala ya exportation?

Na ukisema sijui pesa zimeamishiwa BANK kuu siwatetei serikali ila waliamisha kwasababu na kuna advantage kubwa kuliko disadvantage.

Na unajua BANK kuu wameshusha viwango cha Riba ivi karibuni? Labda nachotaka kuwa sisitizia BANK kuu wawe wafuatiliaji wa viwango vya riba kwa mabank ya biashara ili ziwafikie wafanyabiashara wadogo.
 
wale jamaa wameendekeza sana urasimu na umangimeza...nilishangaa Masamaki alishindaje kesi.

Waziri Mpango haukuwa serious ktk kukusanya mapato; ulipaswa kuflash wapokea rushwa wote TRA na kuweka vijana wapya mpaka watu wa usalama.

Watu waliokuwa kwenye payroll ya home shopping mpk leo wamejaa ofisi zote za TRA na home shopping anaendelea na kazi zake km kawaida, unategemea mapato kweli? Hapo bado kampuni nyingne zenye kutumia mbinu za home shopping... ulitakiwa ufanye complete overhaul

na njia ni ndogo tuu, anzia na mali wanazomiliki compare na gross salary zao za 1,800,000...angalia biashara zao na source ya mitaji yao!!

Hao TRA Police n.k wameshakula nyama ya mtu hawawezi acha, fukuza wote tuingie nasisi tuitumikie nchi
Mkuu hizo gross za 1,800,000 wanalipwa watu wa customs au?
 
Kwa hali iliyopa na inavyoendelea kwa sasa nchini...

Kupungua kwa mapato ya nje ni jambo siyo lakushangaza...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom