Waziri wa Fedha naomba ufafanuzi utozaji kodi kwenye fungu la kumi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,095
164,436
Katika makanisa yetu ya kiroho tuna utaratibu wa kutoa sadaka iitwayo fungu la kumi. Sadaka hii huenda moja kwa moja kwa mchungaji na haihusiki na gharama za kulihudumia kanisa.

Swali:
Kwa mujibu wa sheria ya kodi pato lolote halali kwa mtu binafsi linapaswa kulipiwa kodi ya mapato, je ni utaratibu gani hutumika kutoza kodi vipato vya wachungaji? Najua wachungaji wa kimisheni kutoka Ulaya hujaza annual return na kulipa kodi zao accordingly but sielewi hawa wa nyumbani utaratibu ukoje?

Pili kwanini usiwepo utaratibu wa kuwithhold, say kabla sijalipa fungu la kumi nawithhold kiasi fulani cha fedha ambacho nitakiwasilisha TRA kama kodi ya mchungaji at the same time na mimi nifikiriwe kwenye deductions zangu maana fungu la kumi kanisani linakuwa calculated kutoka kwenye gross income/salary.

Ahsante nasubiri majibu kwa utii na upole!
 
Mods naomba msiunganishe/msihamishe uzi huu.Katika makanisa yetu ya kiroho tuna utaratibu wa kutoa sadaka iitwayo fungu la kumi.Sadaka hii huenda moja kwa moja kwa mchungaji na haihusiki na gharama za kulihudumia kanisa.Swali:kwa mujibu wa sheria ya kodi pato lolote halali kwa mtu binafsi linapaswa kulipiwa kodi ya mapato, je ni utaratibu gani hutumika kutoza kodi vipato vya wachungaji?Najua wachungaji wa kimisheni kutoka Ulaya hujaza annual return na kulipa kodi zao accordingly but sielewi hawa wa nyumbani utaratibu ukoje?Pili kwanini usiwepo utaratibu wa kuwithhold, say kabla sijalipa fungu la kumi nawithhold kiasi fulani cha fedha ambacho nitakiwasilisha TRA kama kodi ya mchungaji at the same time na mimi nifikiriwe kwenye deductions zangu maana fungu la kumi kanisani linakuwa calculated kutoka kwenye gross income/salary.Ahsante nasubiri majibu kwa utii na upole!
Umeeleza vizuri kuwa kwa mujibu wa taratibu zenu hilo 'fungu la kumi' ni mapato ya mchungaji. Anapaswa alipe kodi sawia. TRA angalieni hiki chanzo, kuna mapato mengi sana hapa yanapotea. Kila mtu alipe kodi.
 
Mshahala nilio toa fungu la kumi unasahau kwamba nisha lipa kodi unataka tena iliko kwenda acheni hizo
Mshahara niliotoa pesa ya kununulia shati nilishalipia kodi, lakini ninaponunua hilo shati muuzaji atalipa kodi kwenye mapato yale. Vivyo hivyo kwa mchungaji wako, anapaswa kulipia kodi mapato hayo.

Pesa ambayo ningesema isamehewe kodi ni ile inayotolewa kama sadaka ya kusaidia wenye shida kama yatima, wagonjwa nk, lakini sadaka hiyo hiyo ikitumika kulipa mshahara aliyepokea mshahara anapaswa kulipa kodi.
 
Dah, yani fungu la 10 anakula lote mchungaji!! Kwetu sisi sadaka ya fungu la 10 huingizwa kwenye pesa za miradi ya maendeleo ya Usharika husika. Hailiwi hata senti kwani anapata mshahara wake na posho zake kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
 
Mtoa mada hajui dimension ya FUNGU LA KUMI,kwanza sheria inasema nini kuhusu mapato ya nyumba za ibada.lakin pia nimuulize siku asipotoa fungu la kumi mchungajia huwa anakuepeleka polisi ? utoaji wa nyumba za ibada ni wa kiimani na sio laazma so sio pato la uhakika alafu sio kweli kwamba makanisa yote fungu la kumi anatumia mchungaji lote.najua kunaunacho tafuta
 
Katika makanisa yetu ya kiroho tuna utaratibu wa kutoa sadaka iitwayo fungu la kumi. Sadaka hii huenda moja kwa moja kwa mchungaji na haihusiki na gharama za kulihudumia kanisa.

Swali:
Kwa mujibu wa sheria ya kodi pato lolote halali kwa mtu binafsi linapaswa kulipiwa kodi ya mapato, je ni utaratibu gani hutumika kutoza kodi vipato vya wachungaji? Najua wachungaji wa kimisheni kutoka Ulaya hujaza annual return na kulipa kodi zao accordingly but sielewi hawa wa nyumbani utaratibu ukoje?

Pili kwanini usiwepo utaratibu wa kuwithhold, say kabla sijalipa fungu la kumi nawithhold kiasi fulani cha fedha ambacho nitakiwasilisha TRA kama kodi ya mchungaji at the same time na mimi nifikiriwe kwenye deductions zangu maana fungu la kumi kanisani linakuwa calculated kutoka kwenye gross income/salary.

Ahsante nasubiri majibu kwa utii na upole!
wewe si muumini wa Kikristo maana sadaka zitolewazo zikiwamo fungu la kumu au zaka si mali ya kiongozi wa kanisa mahali husika bali ni mali ya kanisa.

Makanisa ya Kikristo yana uongozi wa kanisa unajumuisha kiongozi wa kidini na waumini; viongozi hao ndio huandaa bajeti ya kanisa na kuratibu mapato na matumizi ya kanisa. Kanisa ili matumizi kama posho ya kiongozi wa kidini, mishahara kwa waajiriwa wa kanisa, ulinzi, umeme, maji na mengineyo mengi yanayogharamiwa na sada na michango mbalimbali itolewayo na waumini.

Ufafanuzi wangu unahusu makanisa yenye usajli halali hapa nchini na si vibanda vya kuabudiwa vinavyomilikiwa na wahubiri walioanzisha hivyo vibanda vya kuabudiwa na kukusanya sadaka
 
Nahisi sijakuelewa vyema ndugu. FUNGU LA KUMI, kwanza maana yake nini pengine nielewavyo mimi ni tofauti na ulichokikusudia
 
Note: sio sahihi kusema fungu la kumi linaenda moja kwa moja kwa mchungaji na haihusiki ma gharama za kulihudumia kanisa. -
Hii scenario labda ina apply huko kwenye kanisa unalosali wewe.

Huku kwetu Anglican huwa tuna utaratibu wa kutangaziwa mapata yoote na matumiz ya Sadaka zetu, ikiwamo pia mapato ya Fungu la kumi.

Sadaka zote zinazotolewa ikiwa ni sadaka za kawaida, fungu la kumi, sadaka za shukrani na sadaka maalumu ni mali ya Bwana na zitatumika katika shughuli za kanisa na uinjilisti (kwa uelewa wangu)

(Sasa ninyi endeleeni kuliwa na kuwalisha hao mitume na manabii wenu.)

Mimi si mchungaji wala shemasi, - ila nakushauri pitia makabrasha yako uone nini maana halisi ya neno Fungu la Kumi.

Turud kwenye mada.

Je sheria inasema nn kuhusu mapato ya kanisa?
Hilo ni suala la kiimani...

Je ukiwa na utaratibu wa kugawa pesa kwa taasisi za yatima kila mwisho wa mwezi itabid na hizo hela zikatwe kodi?

Nadhan bado watz hatuna tafsir sahihi ya hizi kodi.
 
Fungu la kumi ni la mchungaji kivipi?

Vipi kuhusu umeme, maji, samani, mishahara ya watumishi, akiba etc?
 
Mtoa mada hajui dimension ya FUNGU LA KUMI,kwanza sheria inasema nini kuhusu mapato ya nyumba za ibada.lakin pia nimuulize siku asipotoa fungu la kumi mchungajia huwa anakuepeleka polisi ? utoaji wa nyumba za ibada ni wa kiimani na sio laazma so sio pato la uhakika alafu sio kweli kwamba makanisa yote fungu la kumi anatumia mchungaji lote.najua kunaunacho tafuta
Acha mara moja kuwachimba wapakwa mafuta wa Bwana.Tafuta laana utapata.
 
Hili fungu la kumi ni dhambi kubwa sana inatendeka, ni utapeli wa waziwazi unaofanywa na wachungaji hasa wa haya makanisa makubwa ya kiroho, wanatumia uelewa mbovu wa kiimani kuwatapeli watu pesa zao hasa wajane. Nina ushuhuda mkubwa juu ya hilo. Kuna siku tulikuwa tunanunua kiwanja+nyumba kutoka kwa mjane mmoja anayeabudu katika haya makanisa ya kilokole (Sitamtaja huyo mchungaji) masharti aliyotoa ni haya;
  1. Kabla ya kununua hilo eneo ni lazima wanunuzi pamoja na hati tukaombewe na huyo mchunguji.
  2. Hati itakabidhiwa kwetu na mchungaji baada ya kuiombea.
  3. Pesa tutalipa katika account mbili, moja ya muuzaji na hiyo fungu la kumi tutalipa kwenye account BINAFSI ya mchungaji.
Kilichotokea, tulikubali hayo masharti kwa sababu nia yetu ilikua ni kiwanja, masikini yule mama mjane siku ya maudhiano tulienda nyumbani kwa mchungaji akafanya maombi ya uongo na kweli akiwa na mke wake, tukamlipa milioni 16 kama fungu la kumi, na hayo yote yalifanyika kwa masaa ma 2 tu. Baada ya miaka 3 yule mama ni masikini kutokana na kuendelea kutoa michango mbalimbali kanisani, kutumia muda wake mwingi kanisani, na sina uhakika kama atakua na thamani tena mbele ya yule mchungaji.
 
Nahisi hilo kanisa lako ni la uchochoroni au hujui kabisa maana ya fungu la kumi na maana ya sadaka
 
Tutofautishe mali za binadamu na mali za Mungu.Wakala wa mali na fedha za binadamu ni TRA na serikali.Wakala wa mali za Mungu ni viongozi wa dini wawe wachungaji,mapadri,masheikh,wazee wa makanisa,maketekista nk.

kUZITOZA kodi ni sawa na kumtoza Mungu kodi ambako kwaweza leta laana katika nchi.Si sahihi kutoza kodi hela zozote za kidini zinazotolewa kwenye majumba ya ibada kwa ajili ya maswala yao yahusianayo na ibada za dini
 
Dah, yani fungu la 10 anakula lote mchungaji!! Kwetu sisi sadaka ya fungu la 10 huingizwa kwenye pesa za miradi ya maendeleo ya Usharika husika. Hailiwi hata senti kwani anapata mshahara wake na posho zake kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
kwasababu ana mshahara na posho, lazma hilo fungu lifanye mambo mengine, lakini kwenye makanisa ya kiroho hakuna mishahara ya wachungaji, ndo mana wanaishi kwa kutegemea hilo fungu la kumi
 
Back
Top Bottom