Waziri Wa Fedha Na Mipango Aridhishwa Na Kasi Ya Ujenzi Wa Ofisi Za Wizara Ya Fedha Na Mipango –ihumwa

kiwenini

Member
Nov 25, 2018
73
125
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Mpango ameyasema hayo jana alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo ambazo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

‘Nafikiri tunaenda vizuri, quality of work inanifurahisha, ikifika tarehe 1 Machi, 2019, nijisikie nipo huru sasa nabadilisha ofisi nipo Ihumwa’ alisema.

Aidha Dkt. Mpango ameuagiza Uongozi wa Wizara kuanza mchakato wa ujenzi wa Jengo kubwa la Ofisi ili kuweza kutosheleza Watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi hizo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi Elisante Ulomi amesema ujenzi wa awamu ya kwanza umejumuisha Ofisi ya Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Wakuu, ukumbi wa mikutano, ofisi za madereva, pamoja na ofisi za Wakurugenzi saba.

Mhandisi Ulomi amesema ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 92, na utakamilika tarehe 28 Februari,2019.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom