Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Mkurugenzi Mtendaji mbadala wa Benki ya dunia, Kanda ya Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza umasikini.

Katika mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa nguvu zote.

Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la Tanzania.

Pia Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler's Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji.

Kupitia miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt. Mpango alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya Dunia ili uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada inazozionesha hasa katika kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee na juhudi zetu za kuimarisha uchumi wetu hususani katika sekta ya kilimo na pia amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda.


IMG_2027.JPG
IMG_2043.JPG



Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Washington D.C
 
Sasa mnatuchanganya. Mnasema pesa ipo, hapo hapo tena Bank iwasaidie? Tushike lipi tuache lipi?
 
Sielewi, hiyo miradi tunaomba benk ya Dunia itusaidie au hela tunazo?

Maana kila wakati nasikia serikali ikisema hela zipo, sasa benk ya Dunia ya nini?
 
Jana tu Lukuvi amebwabwaja bungeni mpaka mishipa ya shingo ikamtoka eti tunajenga Steigler's Gorge kwa fedha zetu za ndani, leo huyu anaomba msaada world bank kwa ajili ya kufanikisha projects hizo hizo.

Yaani ukijidanganya kuifikiria hii serikali na matendo yake, faster tu utapatwa na stroke yaani ni serikali ya hovyo kwa kiwango cha PhD
 
Sasa mnatuchanganya. Mnasema pesa ipo, hapo hapo tena Bank iwasaidie? Tushike lipi tuache lipi?
Jaribu kuwa mtu basi. Unapokopa kwenye kikoba si kama huna Pesa. Tanzania Pesa ipo ndio maana tunakopesheka.
Leo hii Mengi akienda kukopa CRDB billion 30 akawekeze sehemu atapewa kwasababu anazo Pesa. Mengi atalipa kwa Pesa zake vilevile Tanzania atalipa kwa Pesa zake.
Kwa kuwa wewe sio mtu huwezi kujiuliza mpaka usetiwe.
 
Acheni uongo bwana, kama una pesa hauhitaji kuingia tena gharama kukopa ili uje ulipe kwa riba.

Tunakopa kwa kukosa mitaji na sio vinginevyo. Mbona kuna mataifa mengi tu humu duniani hayakopi na yako vizuri tu. Iran, Kuwait, Saudi Arabia, UAE, Botswana, Mauritius, Taiwan, Brunei, Singapore, Namibia, Equatorial Guinea na zingine nyingi tu.
 
Mi naomba niwaambie kwani wanaposema tunajenga kwa hela zetu wenyewe si wanamaanisha sio za msaada mana hata kama watakopa watazirudisha na hapo tutakuwa tumetumia chetu na sio za wahisani
 
Mi naomba niwaambie kwani wanaposema tunajenga kwa hela zetu wenyewe si wanamaanisha sio za msaada mana hata kama watakopa watazirudisha na hapo tutakuwa tumetumia chetu na sio za wahisani
Ukisema unapesa zako inamaana unaweza kuzitumia utakavyo na ukienda kukopa inamaana utapangiwa masharti kuanzia matumizi na jinsi ya kulipa na fidia zake, kwahiyo hela mkopo sio za kwako kamwe.
 
Ukisema unapesa zako inamaana unaweza kuzitumia utakavyo na ukienda kukopa inamaana utapangiwa masharti kuanzia matumizi na jinsi ya kulipa na fidia zake, kwahiyo hela mkopo sio za kwako kamwe.
Ukikopeshwa zinakuwa zako au sio zako?
 
Deni la dunia ni USD trilioni ngapi vile? Na ayeongoza kudaiwa ni nani?
Tuacheni masihara, uwe unaweza au huwezi kulipa, kuongoza kwa madeni si sawia. Hasa kwa maskini.
 
Sasa mnatuchanganya. Mnasema pesa ipo, hapo hapo tena Bank iwasaidie? Tushike lipi tuache lipi?
Mkuu kwa wale wenye familia wanaweza kunielewa nikiuliza maswali yafuatayo
1 Kuna familia imewahi kujitosheleza kwa kila kitu ?
2- Kuna familia haojaeahi kuomba msaada wa aina ye yote ile ?

Kama hakuna basi,nchi ni kama ilivyo familia haiwezi kujitosheleza kwa kila kitu.
Hakuna nchi imewahikuwa kuwa na uchumi wa kujitosheleza.
Rais Magufuli anaposema tuna pesa hana maana kwamba Tanzania sasa tupo kamili kwa kila jambo.
Mradi wa reli ya kisasa hii inayojengwa itagarimu zaidi ya trilioni 30 mpaka kukamilika.
Makusanyo ya kodi ni trillioni 25 kwa mwaka,hapo unaweza kuona kwamba bila mikopo reli haiwezi kwisha.
Ndio maana taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi na kiulinzi duniani,yaani USA ndilo taifa linaloongoza kuwa na madeni dumiani.
Kwa hiyo mkuu,waziri wetu wa fedha juimba benki ya dunia kusaidia kufadhili baadhi ya miradi ni mswano tu.
 
Ukikopeshwa zinakuwa zako au sio zako?
Utakuwa umekopeshwa na unahitaji kulipa kwa masharti ya mkopo. Zakwako ni zile ulizo fanyia kazi au zilizo toka kwenye rasili mali zako, mfano umeuza Madini yako au umekusanya pesa zako kutoka kwa wadaiwa unao wadai.
 
Mi naomba niwaambie kwani wanaposema tunajenga kwa hela zetu wenyewe si wanamaanisha sio za msaada mana hata kama watakopa watazirudisha na hapo tutakuwa tumetumia chetu na sio za wahisani
Hueleweki umeongea nini, la ajabu kunawatu wake like!!
 
Back
Top Bottom