Waziri wa fedha atumbuliwa

Waziri wa fedha atumbuliwa

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019
SEOUL, KOREA KUSINI
RAIS Moon Jae-in wa Korea Kusini, amemfukuza kazi Waziri wa Fedha, Kim Dong-yeon na msimamizi mkuu wa sera, Jang Ha-sung, wakati ambapo taifa hilo likikabiliana na kasi ndogo ya ukuaji uchumi na ongezeko la ukosefu wa ajira.
Msemaji wa Ikulu ya Korea Kusini, Yoon Young-chan, amesema jana kuwa nafasi hizo tayari zimeshajazwa. Imeelezwa kuwa maofisa hao wamekuwa wakipingana katika kulishughulikia suala la uchumi.
Serikali ya Moon imeongeza kima cha mshahara pamoja na kupunguza muda wa kufanya kazi.
Wakosoaji wanasema hatua hiyo imewaathiri zaidi wanaopata kiwango cha chini cha mshahara na kampuni ndogo zimepunguza wafanyakazi, huku kampuni kubwa zikipunguza kuwekeza kutokana na sheria ngumu za uwezekaji.
Mwezi uliopita Benki Kuu ya Korea Kusini, ilipunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wake kwa mwaka huu hadi asilimia 2.7, ikiwa ni chini ya asilimia 3.1 zilizofikiwa mwaka uliopita.
 
HAHAHHAA ..NDUGU KWANI MAADA HAIJAELEWEKA ..AU ULIKUA UMEPANGA KUSIKIA KITU GANI?
Genye zako mbaya wallah, wenzio tumejua ni huyu wa kwetu, umetutoa mbio kutoka huko kuja kumbe mambo ya korea ha ha ha
 
Genye zako mbaya wallah, wenzio tumejua ni huyu wa kwetu, umetutoa mbio kutoka huko kuja kumbe mambo ya korea ha ha ha
HAYA MAMBO YANAFANYIKA DUNIANI KOTE...LAKINI AKIFANYA MAGUFULI INAONEKANA KAKOSEA NA HAJUI MADARAKA....KUMBE NI MAMBO YA KAWAIDA SANA WATANZANIA TUBADILIKE
 
HAYA MAMBO YANAFANYIKA DUNIANI KOTE...LAKINI AKIFANYA MAGUFULI INAONEKANA KAKOSEA NA HAJUI MADARAKA....KUMBE NI MAMBO YA KAWAIDA SANA WATANZANIA TUBADILIKE
Ni kweli yanafanyika, lakini popote pale kubadilisha mawaziri siyo jambo la kawaida, kote kule huwa wanakuwaga na mijadala mikali, kwahiyo sio dhambi kwa wabongo kuwa na mjadala, kuonekana kukosa au kupatia huwa inatenemeana anatoka nani anaingia nani....pia kumbuka sasa hivi kateuliwa Mwita ambaye miezi minne nyma alikuwa upinzani..kwa vyovyote vile maneno lazima yasikike tu, jamaa ywtu mwaijage naye hakosi kuongelewa...kwahiyo sio dhambi
 
Back
Top Bottom