Waziri wa Elimu Prof Ndalichako awasimamisha kazi Mkuu wa chuo, Makamu, Mhasibu na Boharia wa chuo cha ualimu Patandi

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Habari za hivi punde zinadai viongozi tajwa hapo juu wa chuo cha ualimu Patandi cha mkoani Arusha.

Nazidi kufuatilia sababu za kusimamishwa kwao.

Source: Mkufunzi chuoni hapo.

======

Arusha. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi watumishi sita wa Chuo cha Elimu Maalumu Patandi Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kwa makosa mbalimbali yakiwamo uzembe, matumizi mabaya ya fedha za umma na upotevu wa vifaa vya ujenzi wa Sekondari Maalumu Patandi.

Akizungumza na uongozi wa chuo hicho leo Jumapili Februari 3, 2019, Profesa Ndalichako amesema Serikali haiwezi kuwavumilia watumishi wazembe wanaokwamisha miradi ya maendeleo bila sababu za msingi.

Watumishi waliosimamishwa ni mhasibu mkuu, Rose Kijaka; makamu mkuu wa chuo, Isack Myovela; mwenyekiti wa kamati ya mapokezi, Peter Mosha; boharia wa chuo, Charles Njarabi; na Henry Matei aliyehamishiwa Chuo cha Ualimu Monduli ambaye ameagiza arudishwe kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kuhusu mkuu wa chuo hicho, Janes Liana amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, kumuondolea madaraka na kuendelea na utumishi kutokana na maradhi yanayomsumbua kwa muda mrefu.

Pia, amemuagiza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), kumchukulia hatua aliyekuwa msimamizi wa mradi huo, Israel Mayage kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Profesa Ndalichako amechukua uamuzi huo baada ya kubaini ucheleweshaji wa ujenzi wa shule hiyo maalumu ambayo ilianza kujengwa Aprili 2017 hadi sasa haijakamilika, huku ikiwa imepangiwa kupokea wanafunzi 650 wenye ulemavu Februari 7, 2019.

"Haiwezekani shule moja ijengwe kwa karibu miaka miwili wakati fedha zipo na sioni thamani ya fedha kwa kazi iliyofanyika na watumishi wote waliosababisha tukafikia hapa tutawachukulia hatua za kisheria na ikibainika wamechukua fedha za umma mali zao zitataifishwa na mafao ya kustaafu," amesema Ndalichako.

Amesema kulingana na nyaraka zinaonyesha mifuko 8,500 ya Saruji imenunuliwa lakini kamati ya ujenzi inadai ni mifuko 6,500 tu ambayo nayo haiendani na kazi iliyofanyika.

Waziri huyo amesema makosa aliyoyabaini ni kuwapo ununuzi uliofanyika bila risiti hatua ambayo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) aligundua zaidi ya Sh237 milioni kutokuonyesha risiti zake.

Pia, katika ununuzi moja ya risiti inaonyesha Novemba 30, 2017 kiasi cha malori 170 ya mchanga yalinunuliwa wakati wajumbe wa kamati ya ujenzi wakiwa hawana taarifa.

"Sitakubali fedha za umma zipotee sioni thamani ya Sh990 milioni kwenye awamu ya kwanza na tayari tumeshatoa nyingine Sh1 bilioni, lazima tuwe wazalendo kwa ajili ya nchi yetu," amesema Profesa Ndalichako.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema kesho atakuwa na kikao na kamati ya ujenzi kujiridhisha kama wana uwezo wa kusimamia kazi hiyo au awape kazi hiyo kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro.

Amesema atahakikisha kasi ya ukamilishaji wa madarasa, mabweni na bwalo vinakamilika kwa wakati ili kuruhusu wanafunzi kuanza masomo kwa wakati.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk AveMaria Semakafu amesema baada ya kubaini kasi ya ujenzi kutokuwa nzuri alimteua mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuwa mwenyekiti wa ujenzi ili kufanikisha nia ya Serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Sijawahi kumuelewa Huyu mama hata siku moja, Mkwere hakuwa mjinga kumtimua pale Necta, Huyu Ndalichako ni Pandikizi tu mwenye nia ya kutaka kuua Elimu yetu. Sijui inakuwaje mpaka anafika Rank ya juu sana, We should wake up now
Nasikia ni Mtaalam wa Mathematics! Hapo ndipo tatizo linapokuja....

Anao utalaam wake mzuri tu kwenye uongozi.

Halafu pale NECTA hakutolewa bali aliamua kutoka mwenyewe kutokana na sakata la Matokeo ya NECTA kidato cha 4 mwaka 2012.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu I'm telling u, She is not among of us Hio wizara ni sensitive sana.
 
Habari za jioni hii ni kuwa Mheshimiwa Waziri wa Elimu Prof Joice Ndalichako amewasimamisha kazi viongozi hao chuo cha ualimu Patandi cha mkoani Arusha.

Patandi ni chuo cha elimu maalum. Nazidi kufuatilia habari hizi.

Source: Mkufunzi chuoni Patandi.
 
Hivi hao mawaziri huwa wanatumia mamlaka yapi kumfukuza mtumishi kazi????.anayejua naomba anifahamishe
 
Habari za hivi punde zinadai viongozi tajwa hapo juu wa chuo cha ualimu Patandi cha mkoani Arusha.

Nazidi kufuatilia sababu za kusimamishwa kwao.

Source: Mkufunzi chuoni hapo.
Nimeambiwa, Mkuu huyo wa Chuo ni Mchagga.
 
Sijawahi kumuelewa Huyu mama hata siku moja, Mkwere hakuwa mjinga kumtimua pale Necta, Huyu Ndalichako ni Pandikizi tu mwenye nia ya kutaka kuua Elimu yetu. Sijui inakuwaje mpaka anafika Rank ya juu sana, We should wake up now
Aliwahi kunifundisha statistics for education students......kwa kweli huyu mama ni mweupe peee kichwani...msema kweli ni mpenzi cha Mungu....hata JPM anajua hili. Nilikuwa nashangaa huyu mama alipataje masters na PhD? Sasa leo ni waziri wa elimu, unategemea nini?
 
Mkuu I'm telling u, She is not among of us Hio wizara ni sensitive sana.
Wizara ingekuwa sensitive isingezalauliwa Kias hichi! Waziri Hana msaada kwa walimu waliochin yake! Walimu wanamiaka mnne SASA hawapandishwi madaraja,hakuna nyongeza ya mishahara mpaka nashangaaa kwa NN hii idara(walimu)wanafundisha kwa bidii ili Hali maisha Yao kwa kipnd hichi ni mabaya Sana hata haielezeki wkt waliojuuya hii idara wote n walimu ukianza na jiwe mwwnyewe lkn kaamua kuwaonesha kuwa yeye n jiwe
 
Ni vizuri uainishe tatizo lake ni lipi, mfano amezingua katika kipi?

Ni kwa vipi ni pandikizi?

Itatusaidia kumfahamu zaidi mama huyu katika nafasi hiyo nyeti.
Sijawahi kumuelewa Huyu mama hata siku moja, Mkwere hakuwa mjinga kumtimua pale Necta, Huyu Ndalichako ni Pandikizi tu mwenye nia ya kutaka kuua Elimu yetu. Sijui inakuwaje mpaka anafika Rank ya juu sana, We should wake up now

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wizara ingekuwa sensitive isingezalauliwa Kias hichi! Waziri Hana msaada kwa walimu waliochin yake! Walimu wanamiaka mnne SASA hawapandishwi madaraja,hakuna nyongeza ya mishahara mpaka nashangaaa kwa NN hii idara(walimu)wanafundisha kwa bidii ili Hali maisha Yao kwa kipnd hichi ni mabaya Sana hata haielezeki wkt waliojuuya hii idara wote n walimu ukianza na jiwe mwwnyewe lkn kaamua kuwaonesha kuwa yeye n jiwe
Ndugu,

Wizara yake haihusiki ni walimu! Wizara yake kwa sasa inahusika na SERA na MIPANGO

Mambo mengine kama hayo unayoyazungumzia ni ya

TAMISEMI na UTUMISHI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom