Waziri wa Elimu okoa wanafunzi wa Algeria

Waziri wa Elimu okoa wanafunzi wa Algeria

Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?

Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.

Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .

Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.

Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .

Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.

N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu
Poleni sana wandugu...Mngekuwa huku mngegoma kuingia darasani.
 
yaani umeniwahi; huyo dogo ni shida kweli ushuja wao nini? yeye aombe fedha apige kitabu fulstop; anataka kusema yeye ni matawi ya juu zaidi ya wenzie wa UDSM au SUA?

~~>>>>>Huyu dogo ni limbukeni........ Hakuna Ushujaa kwa kusoma nje nchi......
 
Na sisi tulioko marekani jamani watuangalie hali mbaya.
 
Nilipata admission na Ufadhili Russia nikagoma kwenda....
Good call! Ungeenda huko ungebaguliwa ungekuwa huna hela na ungeowa (kama wewe ni dume) kikongwe cha kirusi ambaye hakuachii hata chooni mnaingia pamoja. Hongera!!!!
 
Ndalichako hana uwezo huo!
Yeye ni matamko tu ndio uwezo wake kikazi
 
Juzi juzi kwenye auditing inakutwa kuna wanafunzi walikuwa wanakopeshwa hadi 12mil kwa mwaka. Urusi ndo balaa. Mkuu wetu akataharuki kana kwamba alikuwa hajui. Halafu nchi zenyewe wanazosoma sasa,eti Mauritius, Msumbiji, Sudan, Botswana. Report iliyoandikwa nadhani na scholarships zenyewe zimefutwa na evaluation mpya ya gharama imefanywa. Hivyo kama hawajapewa basi ni dhahiri kuwa timu ya evaluation imejiridhisha kuwa huko wanahudumiwa kama wanafunzi wa ndani wa nchi hiyo na serikali husika. Ila poleni sana wadogo zetu, kila jambo na wakati wake. Mkazane mmalize mjekutumikia taifa maana lime invest jasho la walipa kodi kuwasomesheni.
 
Sasa kwani waliopanga hivyo viwango c walikuwa hao hao viongoz wa bodi ya mikopo??,, au tatizo ni nin??,,
 
yaani umeniwahi; huyo dogo ni shida kweli ushuja wao nini? yeye aombe fedha apige kitabu fulstop; anataka kusema yeye ni matawi ya juu zaidi ya wenzie wa UDSM au SUA?
Ajabu sana.Kusoma nje ya nchi eti ni ushujaa!
Nilihitimu na rafiki yangu mmoja pale old moshi alipata ufaulu wa kawaida mno na alipata ufadhili wa serikali kwenda kusoma huko Algeria!
Wakati huo kuna vijana kadhaa kutokea hapo hapo old moshi na mwaka huohuo walifanya vizuri kitaifa na wakaishia UDSM na UDOM na vyuo vingine kama hivyo.
Haya mambo ni bahati bwana mdogo!
Hongera kwa kuipata hiyo bahati.
 
Poleni sana i can imagine km ukiwa nyumbani tu ukikosa hela shida seuze nje ya nchi poleni sana sana watz wenzanguu
 
Back
Top Bottom