Waziri wa Elimu okoa wanafunzi wa Algeria

Malcom the X

New Member
Joined
Nov 11, 2016
Posts
3
Reaction score
8
Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?

Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.

Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .

Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.

Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .

Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.

N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu
 
Wekeni majina yenu hapa labda itasaidia.
 
Si mrudi mje mkae na familia zenu ajira zenyee hazipo bora mje mlime malimao tu
 
Enzi zile za kwenda chuo Algeria kupitia Dubai kupiga selfie zimeisha madogo, kwanza tunahakiki kama mlikuwa na vigezo au mlienda kupitia vimemo, pili tunahakiki kama mlistahili kupata mkopo maana wengi wenu ni wa Feza, hahahaha.....!
 
Hii ndiyo Tanzania ya Magufuli. Jaribuni kuwasiliana na taasisi husika otherwise fikeni ubalozini. labda itasaidia kutatua tatizo.
 
Shida mna matumizi mabaya ya pesa.Wanafunzi wa Algeria mnapewa hela nyingi sana.Next time mjifunze kusave itawasaidia mkicheleweshewa mikopo.
 
Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?

Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.

Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .

Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.

Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .

Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.

N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu
Maendeleo gani ? Umeenda kusoma kwa faida yako binafsi,Wangapi walisoma huko kwa scholarship hawajarudi
 
Kupelekwa nje ya nchi na serikali umekuwa shujaa..
 
~~~>>>>Kwahiyo kusoma nje ya Nchi ndio Ushujaa???...... Huu ni uwendawazimu.....
Anaonekana ni libukeni wa kutembea nchi za nje...eti shujaa na analia Hall ni mbaya..au ni shujaa njaa...
 
Wanafunzi wa Algeria mlikuwa mnapewa hela ndefu saaaaan enzi za serikali ya Vasco da gama.. Kuna jamaa namjua alikuwa anazitumnua sana mpaka akaowea mke mwaka Jana... Nawasihi ndugu zangu ishini kwa kusoma alama za nyakati enzi hizi sio za mkwele....

Mkipewa hela jitahidini mzisave ili ziwasaidie kipindi kama hiki hali sio nzuri kama mwanafunzi wa nyumbani hapa hajapewa mkopo itakuwa nyie mlio ng'ambo hata vilio vyenu havionekani...

All in all kama imeshindikana rudini nyumbani mbona wanafunzi waliokuwa wanasoma Ukraine walirudi baada ya mgogoro wa Crimea....
 
Nilipata admission na Ufadhili Russia nikagoma kwenda....
 
Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?

Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.

Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .

Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.

Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .

Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.

N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu
Nimependa unavyojiamni bwana "shujaa" wa mkopo . .....
Desturi za kitanzania ukiwa unaomba jifunze lugha ya unyenyekevu .
Poleni sana,serikal ifanyie kazi maombi yao j amani.
Ni aibu kwa wananchi wa "donor country"kuteseka na njaa wakiwa masomoni .
 
Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?

Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.

Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .

Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.

Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .

Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.

N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu
poleni sana tatizo ni serikali imefilisika,tatizo jingine bajeti ya serikali haiheshimiwi kabisa mfano mapanga shaa hayakuwa kwenye bajeti lakini yamenunuliwa kwa cash.
 
Poleni sana,Mwenyezi Mungu atawafanyia wepesi katika mazito hayo ya kukosa mkopo
 
Back
Top Bottom