NGOSWE.120
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 219
- 233
Naibu waziri wa Elimu bwana Mulugo amewadanganya wakufunzi wa chuo cha Ualimu Songea kuwa madai yao yote yanayohusu upandishwaji wa madaraja/vyeo, malipo ya malimbikizo ya mshahara, likizo, na mengineyo yatalipwa ndani ya quarter ya kwanza ya mwaka wa fedha yaani btb July and September.
Hata hivyo kuanzia jana wakufunzi wote wa vyuo vya Ualimu Tanzania ambavyo vipo chini ya Idara ya Ualimu wameanza mgomo wa kutoingia madarasani kufundisha hadi pale madai yao yatakapolipwa hata ikiwa ni mwakani lakini darasani haingii mtu hata kwa mtutu wa bunduki.
Aidha wameishinikiza serikali kuanza kulipa mishahara kwa scale mpya stahiki za wakufunzi kutokana na waraka mpya uliosainiwa na katibu mkuu utumishi bwana yambesi lakini hadi leo hawajaanza kulipwa mishahara hiyo .
NB: Wanachuo wa chuo cha Ualimu Songea nao leo hii wameanza mgomo kwa kutoingia darasani kuishikiza serikali wawalipe wakufunzi ili wao wapate elimu walio ifuata hapo chuoni.