Waziri wa CUF Zanzibar abariki upigwaji mwandishi wa Channel ten | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa CUF Zanzibar abariki upigwaji mwandishi wa Channel ten

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhogomchungu, Jan 28, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi apigwa kikatili Zanzibar


  na Mohamed Said Abdullah, Zanzibar


  [​IMG]
  Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Munir Zakaria, juzi, alikamatwa na kupigwa na askari wa Baraza la Manispaa ya Zanzibar katika eneo la Darajani na baadaye kutakiwa kusalimisha kamera na mkanda wa video.
  Tukio hilo limetokea wakati mwandishi huyo akifuatilia zoezi la kuwaondoa wafanyabishara katika maduka ya makontena yaliyo eneo la Darajani na wale wanaopanga biashara katika eneo la wazi la shule ya msingi na sekondari ya Darajani.
  Wakati mwandishi huyo akimulika sehemu ya mgogoro huo, askari hao wa manispaa walimvamia na kumweka chini ya ulinzi kabla ya kumpakia katika gari la manispaa huku wakitumia nguvu na kumtaka kusalimisha vitendea kazi vyake kwa sharti la kuwekwa rumande endapo atapinga kutekeleza amri hiyo.
  Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema askari hao walimkamata Munir na kumueleza kuwa ni mchochezi na mhamasishaji wa vurugu zinazofanywa na wafanyabiashara wanaopinga maduka yao kufungwa kwa siku ya nne mfululizo na wengine wakilalamika maduka yao kuvunjwa usiku na kuchukuliwa bidhaa bila ya wenyewe kuwepo.
  Mashuhuda hao walisema, askari hao walimdhalilisha Munir kwa kumbeba kwa staili ya ‘Tanganyika Jeki’, kumpiga kiunoni, begani na chini ya taya, kabla ya kumrusha kama gunia la mchele katika karandinga la manispaa lenye namba za usajili SMZ 4740 na kumfikisha makao makuu ya manispaa hiyo.
  Baada ya kufikishwa katika ofisi za manispaa, Munir alifuatwa na askari kadhaa wa manispaa hadi ofisi ya mkurugenzi Rashid Ali Juma ambaye alikuwa akimfokea mwandishi huyo wa habari na kumshutumu kuwa ni mchochezi na mhamasishaji wa vurugu hizo za Darajani.
  Mkurugenzi huyo, alimpatia Munir masharti matatu, kusalimisha vitendea kazi ikiwemo kamera na mkanda wa video au kuswekwa kizuizini kwa makosa ya kushupalia habari za mgogoro huo wa Darajani.
  “Munir taarifa zetu, zinaonyesha kuwa kila unapokwenda Darajani na kuwahoji wafanyabishara, hamasa zinapanda. Wafanyabiashara wanaanza kuwashambulia askari wetu, hatutaki mpige picha eneo la Darajani, katafuteni habari maeneo mengine, kwani lazima Darajani?!” alisema Rashid Ali Juma.
  Baada ya majadiliano yaliyochukua zaidi ya saa mbili, hatimaye Munir Zakaria aliachiwa huru baada ya kusalimisha mkanda wa video ambao alikabidhiwa jana saa 12.40 mchana kwa masharti ya kufuta picha zote alizopiga Darajani zilizokuwa zikiwaonyesha askari wa manispaa waliokuwa kwenye lindo la eneo la Darajani.
  Naye Munir Zakaria alithibitisha kukamatwa na kupigwa na askari hao wa manispaa, na tayari amesharipoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Malindi na kupatiwa RB namba MAL/R/B358/2011 na kudai kuwa tukio hilo limeingilia uhuru wa vyombo vya habari katika kutekeleza wajibu wao.
  “Wamenikamata. Wamenipiga, wamenidhalilisha mbele ya jamii, sifahamu kitu gani kinachofichwa wakati yanayofanyika yako mbele ya macho ya watu, haiwezekani watu wazima wanapigwa magongo bila ya kuwa na hatia yoyote,” alisema Munir.
  Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui, amelaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kujitokeza katika eneo hilo la Darajani, hasa baada ya maduka kuvunjwa na mengine kufungwa kwa siku ya nne mfululizo.
  Waziri Mazrui alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakidhalilishwa na baraza hilo kwa muda mrefu, jambo ambalo alisema si la kiungwana na liko nje ya misingi ya taratibu za utawala bora.
  Alisema kabla ya operesheni hiyo kufanyika vyombo vyote vinavyohusika vilistahili kuhusishwa ikiwemo uongozi wa wafanyabishara, hasa kwa kuzingatia wafanyabishara hao ni raia na wana haki ya kutafuta riziki ndani ya nchi yao.
  Alisema kama waziri mwenye dhamana na masuala ya biashara atafuatilia mgogoro huo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa kukutana na pande zote zinazohusika ili tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi wa kudumu. Tangu kuibuka kwa mgogoro huo watu wanne wamejeruhiwa katika operesheni ya kwanza ya kuwahamisha wafanyabiashara hao, tangu Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilipoanza kutekeleza majukumu yake.


  WAZIRI WA WIZARA YA HABARI WA SEREKALI YA KITAIFA NI JADI KUTOKA JIMBO LA MAGOGONI CUF. JEE CUF NDIO WALIOKUWA HAYA WAKIAYATAKA?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nini? Mara hii CUF madaraka imeshawapandeni kichwani kama hawa CCM???
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  "WAZIRI WA WIZARA YA HABARI WA SEREKALI YA KITAIFA NI JADI KUTOKA JIMBO LA MAGOGONI CUF. JEE CUF NDIO WALIOKUWA HAYA WAKIAYATAKA?"

  kwenye hii habari uliyoleta amenukuliwa waziri mmoja tu sasa huyo wa waziri wa habari amebariki vipi? au una bifu binafsi na CUF?

  "Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui, amelaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kujitokeza katika eneo hilo la Darajani, hasa baada ya maduka kuvunjwa na mengine kufungwa kwa siku ya nne mfululizo.
  Waziri Mazrui alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakidhalilishwa na baraza hilo kwa muda mrefu, jambo ambalo alisema si la kiungwana na liko nje ya misingi ya taratibu za utawala bora.
  Alisema kabla ya operesheni hiyo kufanyika vyombo vyote vinavyohusika vilistahili kuhusishwa ikiwemo uongozi wa wafanyabishara, hasa kwa kuzingatia wafanyabishara hao ni raia na wana haki ya kutafuta riziki ndani ya nchi yao.
  Alisema kama waziri mwenye dhamana na masuala ya biashara atafuatilia mgogoro huo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa kukutana na pande zote zinazohusika ili tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi wa kudumu."


  Au huyo waziri wa habari ametoa kauli ya kubariki kupitia redioni au gazeti lipi? Tusaidie kufahamu hilo.
  Kama hajatoa kauli yoyote kuhusu tukio hilo, kuna haja ya waandishi wa habari kumhoji kutokana na tukio hilo.
   
 4. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwni mpaka ahojiwe? Kama hajahojiwa ndio anyamaze kimya?
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  saidi mwema na askari wenzake waliahidi kua police hawatotumia tena nguvu dhidi ya raia,haya mkwere na dr shen wanalipi la kutuambia??
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mahala pake!!!!!!!
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  kama hajapata taarifa ya tukio hilo jee?
  ndio maana nimetoa rai ya waandishi wa habari au tv wamhoji kuhusiana na tukio hili, ili tusikie msimamo wake...sio kama namtetea hapa. kama hawajibiki basi awajibishwe...wewe umeleta habari kama vile ametoa tamko kuunga mkono udhalilishaji aliofanyiwa huyo mwandishi wa chl ten.
  bado huoni ni jambo zuri kuhojiwa ili tujue anasimama wapi?
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Siamini kama Dk Slaa angevumilia mambo haya
   
 9. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni mahali gani palipo andikwa yakuwa waziri amebariki kupigwa mwandishi ?nakumbuka wazee wetu walikuwa hutupa wasia tunapowaona watu kama hawa wenye kusema yasiokuwa ya ukweli mara nyingi mtu kama huyu Huwa ni DUYUUS aliyekubuhu
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huu uongo wa wazi kabisa!!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,668
  Trophy Points: 280
  CUF ni kitengo cha CCM kama ilivyo UWT au UVCCM ndiyo sababu wanaunga mkono kwa mwandishi kupewa mkong'oto. Ile CUF ya miaka ilee hili la kupigwa mwandishi kamwe wasingelikubali.

   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wala sishangai kwanza watu wenyewe wanajiita ngunguri, na wamezoea kupigana tu!
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jitahidini kusoma habari msivamie na kukurupuka ,yaani baada ya kuwa great thinkers mnakuwa great loosers ,nimesoma mara tatu kuona wapi waziri alibariki ,hamna ,nyie vipiiii?

  Haya kama si umbumbu tuiteje ,mtu unakurupuka nakusema kama angekuwa Slaa pasingekalika ? Jamani taratibuni msimtafutie mzee wa watu tabu maana mnaweza kumzidishia kasi ya kuota mvi maladufu.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Bro haki huletewi katika sahani ni lazima upapambane ,ungunguri wa CUF ndio leo umewafikisha WaTz walio wengi kuweza kustanda kwenye majukwaa na kutoa mistali. ,Kama mtakurupushwa na kuingia mitini basi mjue CCM itaitawala Tanganyika milele na milele.
   
 15. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 80
  Kusema kweli kitendo ambacho wanakifanya manispaa cha kuwaondoa wafanyabiashara (makontena na mchinaga) ni kizuri hilo la kupiga watu siko pamoja nao.Na huo uamuzi wa kuwaondoa ulikuwa ufanyike zamani sana tangu kwa yale makontena yanachafua mazingira ya ile sehemu na ni aibu kubwa sana kuwepo makontena sehemu kama ile. na kuhusu wamachinga ni jambo la kusikitisha ya kuwa serikali iliwaachilia mpaka wanablock na wanaleta usumbufu kwa wanafunzi wanaosoma shule ya darajani. na siyo kama eneo hawajatengewa bali wameshapewa eneo lakini bado wanalazimisha kubakia pale.Obi langu kwa serikali ni kuondoa uchafu wote wa makontena uliozagaa pale darajani na kama ikiwezekana na michenzani pia
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bw.Muhogomchungu naona rangi ya kijani na njano au sijuwi uchadema umekukaa na roho, huyo uliyemnukuu hapo ni waziri wa biashara na sijaona wapi Mh. Jihad amebariki upuuuzi huo.
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwa ninavyokuheshimu naogopa kukwita muongo mkubwa!
   
 18. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mwandishi anapigwa huku MH JADI AKIWA KIMYA. UNAMAANISHA HAKUBARIKI?
   
 19. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sijaona alipopotoa huyu anayedaiwa waziri wa CUF katika taarifa ya mtoa mada hii.
   
 20. C

  Calipso JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lol! hiyo heading na habari yenyewe ni tofauti kabisa,nilichoona mimi ni kuwa unaifagilia cuf badala ya kuiponda,kwani waziri hapo ametoa tamko zuri..

  DARASA NI MUHINU MWANANDUGU... INAONEKANA HUJUI UNACHOKIANDIKA
   
Loading...