KABILINDUNDU
New Member
- Dec 30, 2015
- 1
- 0
Katika muendelezo wako wa kupora maeneo yote ya ardhi ambayo yanamilikiwa na watu na hawayaendelezi, nakuomba sana Mheshimiwa Lukuvi usiliache pori ambalo lipo eneo la Mbagala Misheni nyuma ya MBAGALA SPIRITUAL CENTRE, pori linamolikiwa na Mtanzania mwenye asili ya Asia anayejulikana kwa jina la GOHA na pori hilo ni maarufu kama kwa GOHA.! Lipo kwa miaka mingi sana na wala halifanyiwi muendelezo wa aina yeyote ile, limekuwa maficho ya wezi na kuwapa adha kubwa sana wakazi wa eneo hilo. Mheshimiwa Lukuvi nakuomba ufike uliangalie na ligawiwe kwa wananchi waweze kuliendeleza.