Mpasuko mkubwa wa Ardhi watokea Mbagala Saku. Baadhi ya nyumba za watu zaripotiwa kubomoka

itakiamo

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
752
1,226
Hii sijui ni tetemeko au ni kitu gani, wataalamu tunaomba mfuatilie na mtupatie majibu, Ardhi inapasuka na nyumba zinabomoka, eneo ni Saku Mwisho DSM
---


Taharuki imeibuka kwa wakazi wa Mbagala Saku baada ya kutokea kwa mpasuko mkubwa wa ardhi na kusababisha kubomoka kwa nyumba nyingi za wakazi wa eneo hilo na kuacha nyingine zikiwa zimeathirika kwa kiasi kikubwa

Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kwenda kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha tatizo hilo na kugundua endapo ni salama kwa wao kuendelea kuishi katika eneo hilo pamoja na kuwapatia msaada kwa wale walio athiriwa zaidi na tatizo hilo
 
Hakuna tetemeko huko, kuna kutitia kwa ardhi kwa sababu ya watu kujenga juu ya udongo ulio dhaifu...

Tanzania watu huwa wanajenga kiholela tu, serikali hai-control watu wajenge maeneo yapi, wajenge aina gani ya majengo n.k

Unaweza ukakuta watu wamejenga juu ya mkondo wa maji wa chini na sasa uzito umekuwa mkubwa, ardhi inatitia...
 
Back
Top Bottom