Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui apinga chanjo ya Covid 19 hadi pale wataalamu ndani ya nchi watakapoitafiti kama inafaa

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Akizungumza katika makao makuu ya Wizara ya afya huko Mnazi Mmoja Zanzibar, Waziri Mazrui amesema Zanzibar haipo tayari kutumia chanjo yoyote ya Covid hadi pale wataalamu wa afya watakapoitafiti na endapo inafaa.

Mheshimiwa Mazrui pia amesema si kila mgonjwa anayesumbuliwa na matatizo ya upumuaji ana Corona bali magonjwa ya mifumo ya upumuaji yapo ya aina nyingi.

Waziri Mazrui amewaasa wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya ili kuepuka magonjwa hasa ya mlipuko.

Pia, Waziri Mazrui amepokea mpango mkakati wa Shirika la Afya Duniani wa kupambana na ugonjwa wa corela.
 
Mnatafiti chanjo ya mabeberu huo tunaita ni copy and paste kama vile wanavyo kariri madesa vyuoni.
 
Waambie upuuzi huo watu wanaotaka kwenda kuhiji Makka mwaka huu

Watu wamedunduliza fedha muda mrefu ili watimize nguzo muhimu ya dini yao, wengine ni wazee au wagonjwa wakiwa hawana uhakika wa kusubiri mpaka "uchunguzi" wenu uishe halafu una wapigia soga la Dr Gwajima.
 
Tunahitaji muda wa kuangalia na kutafakari kama kweli tunahitaji chanjo ya covid! Chanjo ambayo ina sintofahamu za kutosha! Kweli tuendelee kusubiri kidogo tukifanya uchunguzi wa kina na huku tukitafuta njia mbalimbali ya kujilinda na kupambana na gonjwa hili!
 
Chanjo zina sintofahamu gani ? Labda utujuze na wengine tupate kujua.
 
Hao wataalam wetu wamewahi kugundua chanjo ipi kiasi cha kuwa na uwezo wa kutafiti ubora wa chanjo zilizotengenezwa kwenye taasisi za utafiti zenye ubora wa kidunia?

Swali la msingi sana umeuliza!! Kama ufahamu tu walionao sasa kuhusu corona wanajifunza kutoka kwa watafiti wengine - huo utafiti wa chanjo watauweza vipi??

Wakati mwingine ingefaa wakakaa kimya na kusubiri!!
 
Waambie upuuzi huo watu wanaotaka kwenda kuhiji Makka mwaka huu
Watu wamedunduliza fedha muda mrefu ili watimize nguzo muhimu ya dini yao, wengine ni wazee au wagonjwa wakiwa hawana uhakika wa kusubiri mpaka "uchunguzi" wenu uishe halafu una wapigia soga la Dr Gwajima
Kwani hijja imekuwa kama ibada ya sala tano ambayo unalazimika kuswali hata ukiumwa? lishatokea janga sasa huo ulazima kwamba lazima mwaka huu uende hata iweje unatoka wapi?
 
Swali la msingi sana umeuliza!! Kama ufahamu tu walionao sasa kuhusu corona wanajifunza kutoka kwa watafiti wengine - huo utafiti wa chanjo watauweza vipi?

Wakati mwingine ingefaa wakakaa kimya na kusubiri!
Kwahiyo ulitaka kila nchi ifanye utafiti wake kivyake na itengeneze chanjo zake?
 
Tunahitaji muda wa kuangalia na kutafakari kama kweli tunahitaji chanjo ya covid! Chanjo ambayo ina sintofahamu za kutosha! Kweli tuendelee kusubiri kidogo tukifanya uchunguzi wa kina na huku tukitafuta njia mbalimbali ya kujilinda na kupambana na gonjwa hili!
Kaka namna gani sintofahamu za kutosha?
Chanjo za Covid zimetumiwa hadi sasa kwa watu mamilioni (mamia ya mililioni), idadi inaelekea bilioni tayari.
Kote zinapotumiwa idadi ya mifano mikali ya Covid inapungua, idadi ya maambukizi inapungua.
Unataka nini tena?
Halafu: vipi chanjo hizi zote zinazotumiwa nchini? Je kuna sababu gani kuangalia chanjo cha Covid tofauti na chanjo nyingine kama vile rubela (surura) au ukambi? Hadi sasa chanjo zote zinazotumiwa kila siku nchini zimebuniwa Ulaya, Marekani , Uhindi.
Kwa ni ni wanasiasa hawakuzizuia hadi wataalamu wa ndani walizichunguza (sidhani kwamba yoyote imefanyiwa utafiti nchini hapa lakini zinatumiwa kila siku)
 
Hata ningekuwa Mimi ningesema hivyohivyo,

Chanjo zoote zilizowahi kugunduliwa, kabla ya Matumizi Kwa binadamu zilifanyiwa majaribio Kwa sokwe,nyani na wanyama wengine ndipo zinakuwa tayari Kwa Matumizi ya binadamu

Ni hii tu chanjo Kwa mara ya Kwanza inatumika kama majaribio na huku kama chanjo

Ukisikia maajabu ya walimwengu ndio hayo sasa
 
Hao watafiti..., wanatafiti tu kama zinafaa au wanatafita kutafuta chanjo pia ?

Tusidanganyane hapa the only true utafiti mwisho wa siku ni kupata data za waliochanjwa wangapi wana-positive results na kupata sample kubwa, nzuri na ya uhakika ni kwa kushirikiana na dunia nzima
 
Hata ningekuwa Mimi ningesema hivyohivyo,

Chanjo zoote zilizowahi kugunduliwa, kabla ya Matumizi Kwa binadamu zilifanyiwa majaribio Kwa sokwe,nyani na wanyama wengine ndipo zinakuwa tayari Kwa Matumizi ya binadamu

Ni hii tu chanjo Kwa mara ya Kwanza inatumika kama majaribio na huku kama chanjo

Ukisikia maajabu ya walimwengu ndio hayo sasa
Mkuu clinical trials zilifanyika kitambo tu sasa hizi propaganda mnatoaga wapi?
 
Back
Top Bottom