Mhe Ummy Mwalimu naomba utueleze ukweli kuhusu hali halisi na huu ugonjwa wa corona hapa Tanzania ili tujihami kuliko kuficha ficha, ijapokuwa kila jambo lina athari zake!
Kama mtu wa kawaida sana nikiunganisha ninayoyaona na kuyasikia katika mazingira yangu naona tisho ni kubwa la ugonjwa huu katika nchi yetu, nitoe mfano kidogo;-
1. Wenzetu tunaoishi nao wanaotoka huko ugonjwa huu ulikoanzia asilimia kubwa yao ninaokutana nao naona wamevaa vile vya kuzuia pua na mdomo, hii kweli linaniongezea hofu kubwa sana ya uwezekano mkubwa wa ugonjwa huu kuwepo au kuingia dakika yoyote!
2. Tukio nililolisikia hapo daraja jipya la salenda kambi namba 2 ya upande wa ostabey juu mchina aliyekuwa akishukiwa na Corona katika kambi hiyo, ijapokuwa mlijitahidi kufanya kilichofanyika na kuwa ilivyosasa!.
Hayo machache na mengine ninayo yaona na kuyasikia yananiongezea hofu kubwa juu ya hili jinamizi la Corona!
Najua athari za kusema waziwazi juu ya uwepo wa corona ndani ya nchi, lakini kuongeza elimu au uelewa kwa wananchi na kuwapa updates zote juu ya jinamizi hili ni muhimu sana kuliko kukaa kimya bila kuujulisha na kuutahadharisha umma!
Kwa uchumi wetu, elimu yetu, teknolojia yetu, n.k, tukiingiliwa tutaweza? Bado naona kinga ni bora kuliko tiba, maana naona na kusikia jinsi nchi kubwa zinavyohangaika na hili jinamizi la Corona.
Sent using Jamii Forums mobile app