Waziri wa Afya, mheshimiwa Ummy naomba ulishughulikie hili

Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
665
902
Habari za wakati wanajamvi wenzangu, eee bhana nimetoka kuchukua form ya Kumfanyia maombi mdogo wangu aliyemaliza Form six juzi kati. Matokeo yake hayakuwa mazuri sana hivyo nikaona nimpeleke akasome diploma ya Utabibu.

Sasa nimepitia hii form ya hiki Chuo, Bima ya Afya kwa Mwanafunzi hapa wanatoza 60,000/- tofauti na bei iliyoelekezwa na Wizara ambayo ni 50,400/-.

Sasa mheshimiwa ummy kama kuna ufafanuzi basi ningependa kupatiwa ufafanuzi au Kwa yeyote hapa jamvini Jeifu anaweza kunipatia ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom