Kumfukuza waziri haitasaidia chochote, turudi nyuma na kuangalia mfumo mzima wa AFYA na ELIMU nchini. Mtasema weee mkiukwepa ukweli lakini swala litabakia pale pale. Uongozi wa JK umeshindwa ktk ngazi zote za uongozi kwa sababu mfumo mzima wa kiutawala unakumbatia UFISADI na yeyote utakayemweka ktk nafasi hizo atajua hawajibiki.. Tukubali sote tumeshindwa na tunataka mwanzo mpya. tunataka mabadiliko - CHANGE, na hakuna atakayeweza kuyaleta mabadiliko haya isipokuwa wewe, mimi na Watanzania wengine wote ambao wanaipenda nchi yao kwanza.
Najua sana kwamba mara nyingi hutofautiana na watu wengi na wengine huniona mpuuzi lakini ukweli umesimama kwamba tatizo ni sisi wananchi na suluhu ni sisi wananchi kuweka Uzalendo mbele ya kila kitu..Na bahati mbaya natambua taratibu kwamba hata wasomi wetu wamesoma sana lakini hawaelewi maana zaidi ya Unafiki mbele. Sidhani kama kuna mtu hapa anaweza kunambia kwa nini mwaka 1992 ktk kura za maoni wananchi wengi walipinga mfumo wa vyama vingi wakati rohoni mwao walitaka kuwepo kwa vyama vingi?..
Jamani tuache unafiki tuippende nchi yetu na tuwe tayari kujitoa mhanga ktk kutetea maslahi ya Taifa na sii kutazama rangi zetu...