Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,471
- 12,373
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesitisha zoezi la utoaji chakula kwa wagonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo serikali itakapojiridhisha faida na hasara ya zoezi hilo.
Hii ndio Tanzania.
------------------------------
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema,
- Hata hivyo nimepokea maoni mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo itaanzisha utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa’
- Kufuatia hali hii kuleta wasiwasi kwa wananchi na wagonjwa, nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpak hapo tutakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya unaopendekezwa’