Waziri Ummy, Taarifa yako kuhusu makusanyo haiendani na Kilichomo kwenye website ya TAMISEMI. Je, Watendaji wamekudanganya?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Salaamu kwa wote.

Hivi karibuni mh.Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu alitoa taarifa ya makusanyo kwa kila Halmashauri ikiwa ni utaratibu wao wa kufanya tathmini ya utendaji wa Halmashauri zetu.

Taarifa husika ilikuwa na uchambuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindanisha makundi ya Halmashauri zilizoko kwenye hadhi sawa kama Majiji, Manispaa, miji na Halmashauri za Wilaya.

Baada ya taarifa ya Waziri kuisoma kwa waandishi wa Habari,mh.alisema taarifa yake kwa undani inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Tamisemi.

Kwa bahati mbaya kulizuka malalamiko kutoka baadhi ya Halmashauri kama Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Madiwani wakilaumu kwamba taarifa iliyotolewa na Waziri sio sahihi.

Sasa kanakwamba haitoshi Viambatanisho vilivyowekwa ku support taarifa ya Waziri haviendani na Takwimu zilizoko kwa mfano anadema Jiji la Dar limeongoza kwa makusanyo ghafi sh.67 bln wakati kwenye kiambayinaonyesha sh.48 bln,hivyo hivyo kwa Dodoma nk .

Sasa Hali hii inazusha maswali Kuhusu usahihi wa taarifa husika.Nitoe wito kwa mheshimiwa Waziri kupitia taarifa yake na kilichowekwa website la sivyo utadanganywa sana na watu wa Tamisemi,huku kumejaa wababaishaji na wapigaji.

Attachment ziko hapo chini👇👇

Screenshot_20210804-064951.png


Screenshot_20210804-065008.png
 

Attachments

  • Waandishi - TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA MAPATO YA NDANI - WN-2.pdf
    160.8 KB · Views: 5
  • KIAMBATANISHO 1-3.pdf
    81.5 KB · Views: 4
  • KIAMBATAMISHO 4-5.pdf
    161 KB · Views: 3
Back
Top Bottom