Waziri Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangallah, hawajaitendea haki wizara ya Afya!! | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangallah, hawajaitendea haki wizara ya Afya!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meningitis, May 19, 2016.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2016
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mdau wa afya mkorofi!!

  Msema kweli ni mpenzi wa Mungu...!hata Mheshimiwa Rais anaupenda msemo huu.

  Mimi nilikuwa pro Chadema kabla hawajaniboa kwa kumpokea fisadi na kumfanya mgombea wao wa urais!!

  Linapokuja swala la Afya ninasimama kama mwanaafya ninayepigania kwa nguvu na dhati ili sekta hii ikae vizuri.

  My observation kwa kipindi hiki cha uongozi wa Magufuli ni kwamba mengi mazuri yamefanyika na pia kuna fursa ya kufanya mengi zaidi iwapo weledi utawekwa mbele.

  Nimeobserve kwa muda sasa kati ya mengi ya malalamiko ya wananchi Afya yaweza kuwa namba moja au namba mbili hivyo ni janga la kitaifa.

  Sekta hii imeongelewa sana na wanasiasa lakini hakuna mwanasiasa aliyeifanyia jambo muhimu kwa kiasi cha umuhimu wake.

  Nilitegemea mawaziri walioteuliwa kwa slogan ya hapakazitu waweze kusimama na kutenda kwa slogan hii.

  Nilimtegemea sana @Hkingangwalla kama daktari angeweza kupresent tatizo la msingi la sekta hii kwenye baraza la mawaziri (kwa kumpa nondo waziri) ili tatizo kuu katika sekta ya afya liweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

  Badala yake naibu waziri huyu pengine kwa kukosa uzoefu wa mfumo wa afya nchini amejikuta akipambana na kushughulikia dalili za Tatizo katika sekta hii.

  Bado najiuliza kwa nini bajeti ya afya imeendelea kuwa ndogo ukilinganisha na bajeti za sekta nyingine kwa miaka yote hii? Hata mwaka huu ambao tumepata Rais mpambanaji?

  Najiuliza ni kwa vipi bajeti ya afya iwe ndogo despite kelele nyingi zilizotokea kwenye sekta hii toka Rais Magufuli aingie na kuanza kutumbua majipu ambapo mengi ya majipu yaliyoripotiwa ni kutoka sekta ya afya?(hapa naongelea majipu yaliyotumbuliwa kwenye local goverments)

  Kwa maoni yangu napatahisia kuwa waziri wa afya na naibu wake hawajafanya effort yaushawishi katika baraza la mawaziri katika kudai mkate mnono unaoweza kukidhi njaa ya sekta muhimu ya afya.

  I wish Muhongo angekuwa waziri wa afya...kwani amepewa mahela mengi ya kufanyia utafiti wa nishati ...ina maana mahela haya yataenda kwa wataalamu wa nje ya nchi!

  TUNAKOSOA KITAALAMU NA KIZALENDO!
   
 2. T

  Tanzania Njema Yaja JF-Expert Member

  #21
  Oct 11, 2016
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 3,061
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  Narudi kwenye mada... kwanza suala la chanjo kuisha kwa kweli halikubaliki... chanjo kuanzia miaka 0 mpaka 5 hutolewa ndani ya muda ulio pangwa kitaalamu ....sasa chanjo zinapo isha mnawezaje kuwa na uhakika kwamba walio zikosa hawataathirika? Kwamba ni kweli tunashindwa ku replenish stock ya dawa muhim kama chanjo? Na je mmewachukulia hatua gani wafanyakazi walio sababisha ucheleweshwaji wa dawa hizi muhim unao weza suababisha magonjwa hatari kama polio kuwapata watoto wetu?
   
 3. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #22
  Oct 11, 2016
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,548
  Likes Received: 4,035
  Trophy Points: 280
  Waziri Mwaimu na Naibu wake Andrew Bagaile wameshindwa!Uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana!
  Wao ni matamko baada ya matamko!Wameshindwa kusimamia dhana nzima ya upatikanaji huduma nafuu kwa mtz
   
 4. 100bucks

  100bucks JF-Expert Member

  #23
  Oct 11, 2016
  Joined: Feb 26, 2014
  Messages: 439
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 80
  Toka mwezi wa tano huu Uzi hauna wachangiaji
   
 5. amina ngalo

  amina ngalo JF-Expert Member

  #24
  Oct 11, 2016
  Joined: Jun 13, 2013
  Messages: 312
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 60
  kiujumla wameshindwa kazi waliyopewa watolewe pale afya
   
 6. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #25
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Nashindwa kuelewa kuhusu ajira za madaktari kwa hisani ya Kenya...its either mheshimiwa waziri hakushauri vilivyo wakati wa mjadala huo pale Ikulu au kwa sasa aneamua tu kuanzisha kiburi dhidi ya kauli ya Rais.

  Kwanza alitakiwa apinge siku ileile ya majadiliano kwa hoja za msingi...mfano bado nchi yetu inahitaji madaktari na sio busara kuwapeleka Kenya wakati vituo vyetu havijajitosheleza au hatujatimiza ilani ya ccm inayotutaka tuajiri madaktari kutoka ndani na nje ya Tanzania...Na kama alitetea basi angetoka clean and clearly kwamba hajakubaliana na uamuzi instead yeye ndiye aliyekuja kutangaza kwa mbwembwr zote.

  Pili yeye kama waziri aliahidi utekelezaji wa sera ya bima ya afya kwa wote kufikia septemba 2016 lakini mpaka leo sioni wala kusikia dalili...by the way hii ni mojawapo ya ahadi na sera kwenye ilani ya ccm.
  Sisi ni wabaya sana kwenye kuhoji kistaarabu na kulingana na mlichotuahidi...!!

  Bado nasisitiza kuwa hawa mawaziri despite all the so called dufficulties in facing Magufuli hawajafanya yale yaliyotarajiwa.
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #26
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Ili uchangie ni vyema ukawa mfuatiliaji na mjuvi kwenye hoja zinazohusu thread husika.
   
 8. kimbendengu

  kimbendengu JF-Expert Member

  #27
  Apr 21, 2017
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 2,342
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 280
  pesa za chanjo bilioni 10 zimeliwa
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #28
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Hili haliwezi kuwa hukumu kwao...ni ripoti ya CAG na wahusika wengi wako level ya halmashauri...tuwatuhumu na kuwapinga kwa hoja za kweli tu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...