Mimi nafikiri mnamuonea bure Tizebwa, hajapewa nyumba, alikuwa hakai Dar. Sasa afanyeje? Tulalamikie Serkali ambayo iliuza nyumba kana kwamba Serkali nayo inastaafu lakini si kwa mtu anayestahili kupewa nyumba na hajapewa.
Hakuna utetezi wa kuwabeba wauaji hawa!... Hii fedha ingesaidia watanzania wengi wanaokosa huduma za afya na elimu!... Nyumba zenye hadhi klwa bei nzuri zipo DAR!... laki 3 mpaka 4 mikocheni, masaki, makongo juu, upanga mpaka changanyikeni!!!
sasa baada ya kuondoka amenda kuishi wapi ambako kulishindikana mwanzo
Waziri Dr. Charles Tizeba makamu wa Mwakyembe ambaye amekuwa akiishi katika hoteli ya nyota 4 ya New Africa aondoka baada ya bili kufikia milioni 100.
Hiyo ni bili ya malazi na mlo wa asubuhi tuu achana na buffet na vinywaji!
Jamani huyu waziri ni mzalendo kweli wa kuishi hotelini hadi kufikia kiasi hicho cha pesa? Sina hamu jamani sijui wadau mnalipi la kusema.
Source ni The Guardian on Sunday habari na Floriani Kaijage!
Hoja nzuri sn... lakini ushahidi sio dhaifu tu bali haupo kabisa. Lete vitu vikiwa vimekamilika ndugu.
kama ameondoka mwenyewe bila kufukuzwa basi ni mzalendo!serikali ndio walimuweka akae hapo because nyumba za viongozi wa serikali waliuziana!!waziri mzima hawezi kwenda kulala sinza!
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
kwa wenyeji wa dar mtusaidie kujua nyumba ya 4m per month ina ubora kiasi gani?
Kabla ya kuteuliwa alikuwa anakaa wapi? Kwani JK ana wake wangapi kujaza magogoni yote? Kwani hiyo kazi hakuna mtu mwingine mwenye nyumba Dar anaweza kuifanya?Aulizwe Mkapa na Magufuli.. Sasa Tizeba na wadhifa wake angekaa wapi..
Naamini wengine wana bills kubwa zaidi. Nenda hata Courtyard hotel..
Ndugu watu hapa wanahoji uzalendo wake uko wapi. Alikuwa na uwezo wa kutambua hilo sio jambo jema kwa nchi na wizara anayoiongoza.. Nashindwa hata kuelewa unachokitetea hapo ni nini... Mwezi mmoja au hata wiki mbili zikipita tangu aanze kuishi hotelini alipaswa kuhoji tena kwa nguvu zaidi mahala pa kuishi tofauti na hotel. Tunaona baadhi ya viongozi wakitoa mifano ya kukataa mambo yanayoiongezea nchi gharama zisizo za ulazima kama vile Pinda alivyokataa V8,huo ni utambuzi wa lililo jema kwa nchi yakoTenende Niaelewa frustration yako. Lakini kumbuka bado ni mfumo wa Serkali na siyo mtu binafsi kupangishiwa nyumba. Yeye Kama mteule walipaswa kumpa nyumba whether ni ya Serkali au ya kupangisha kwa watu binafsi. Kama angeikataa (kama tulivyoambiwa kwa waziri wa mambo ya ndani wakati ule)hapo kingekuwa suala lingine.
Nafikiri kuna mambo mengi tusiyoyaelewa. Unajuaje kuwa Mh. Alikuwa ahoji. Sidhani Kama mtu mwenye familia anafurahia kukaa hotelini kwa kipindi chote hicho. Je unafikiri kurudisha V8 kulisaidia?. Si bado ana V8 ingine na aliyorudisha bado iko serkalini ikiingiza hasara ileile kwa walipakodi. Ningeona sahihi Kama angebadilisha mfumo kuhakikisha Serkali haitumii haya maV8 yanayowagharimu walipakodi.Ndugu watu hapa wanahoji uzalendo wake uko wapi. Alikuwa na uwezo wa kutambua hilo sio jambo jema kwa nchi na wizara anayoiongoza.. Nashindwa hata kuelewa unachokitetea hapo ni nini... Mwezi mmoja au hata wiki mbili zikipita tangu aanze kuishi hotelini alipaswa kuhoji tena kwa nguvu zaidi mahala pa kuishi tofauti na hotel. Tunaona baadhi ya viongozi wakitoa mifano ya kukataa mambo yanayoiongezea nchi gharama zisizo za ulazima kama vile Pinda alivyokataa V8,huo ni utambuzi wa lililo jema kwa nchi yako