Waziri Tizeba aamua kuondoka hotelini baada ya bili ya 100milioni

Mimi nafikiri mnamuonea bure Tizebwa, hajapewa nyumba, alikuwa hakai Dar. Sasa afanyeje? Tulalamikie Serkali ambayo iliuza nyumba kana kwamba Serkali nayo inastaafu lakini si kwa mtu anayestahili kupewa nyumba na hajapewa.

sasa baada ya kuondoka amenda kuishi wapi ambako kulishindikana mwanzo
 
Yani ilishindikana kupata hata ka apartment pale Makumbusho? Hawa watu hawana uzalendo
 
Hakuna utetezi wa kuwabeba wauaji hawa!... Hii fedha ingesaidia watanzania wengi wanaokosa huduma za afya na elimu!... Nyumba zenye hadhi klwa bei nzuri zipo DAR!... laki 3 mpaka 4 mikocheni, masaki, makongo juu, upanga mpaka changanyikeni!!!

Tenende

Niaelewa frustration yako. Lakini kumbuka bado ni mfumo wa Serkali na siyo mtu binafsi kupangishiwa nyumba. Yeye Kama mteule walipaswa kumpa nyumba whether ni ya Serkali au ya kupangisha kwa watu binafsi. Kama angeikataa (kama tulivyoambiwa kwa waziri wa mambo ya ndani wakati ule)hapo kingekuwa suala lingine.
 
Waziri Dr. Charles Tizeba makamu wa Mwakyembe ambaye amekuwa akiishi katika hoteli ya nyota 4 ya New Africa aondoka baada ya bili kufikia milioni 100.

Hiyo ni bili ya malazi na mlo wa asubuhi tuu achana na buffet na vinywaji!

Jamani huyu waziri ni mzalendo kweli wa kuishi hotelini hadi kufikia kiasi hicho cha pesa? Sina hamu jamani sijui wadau mnalipi la kusema.

Source ni The Guardian on Sunday habari na Floriani Kaijage!

Wewe ulitaka akae wapi! fanya mabadiliko sasa
 
It's great! A minister staying in a hotel for 247 days charging $250 per night. The bill for just bed and breakfast tallied to be Sh98.8 million, all this squared from public funds. Hatuna viongozi Tanzania!
 
Mie nahisi hii ni style mpya ya ufisadi ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya chukua chako mapema. Kuna sababu gani ya msingi ya Dr.Tizeba kuisusia nyumba yake na kuishi hotelini? Je ameamua kubadilisha hotel au la !?
Ikumbukwe tulidokezwa na mdau mmoja kuhusu hili sakata la Dr. Tizeba kuishi new Africa Hotel ya jijini Dar es Salaam hapa hapa JF siku chache zilizopita, naweza nika - link hili sakata la yeye kuondoka hotelini na hiyo post kwani ni matukio yanafuatana kwa ukaribu sana.

Lakini ni vyema mwenye taarifa za kuaminika atujuze, ni kweli Dr. Tizeba alikuwa anaishi hapo hotelini kwa kipindi chote tangu ateuliwe kuwa naibu waziri, usije kuta jamaa alikuwa anaishi kwake na kila siku anariport hotelini kusaign tu na mwisho wa siku wanagawana mapato ya wavuja jasho.
 
Hoja nzuri sn... lakini ushahidi sio dhaifu tu bali haupo kabisa. Lete vitu vikiwa vimekamilika ndugu.
 
kama ameondoka mwenyewe bila kufukuzwa basi ni mzalendo!serikali ndio walimuweka akae hapo because nyumba za viongozi wa serikali waliuziana!!waziri mzima hawezi kwenda kulala sinza!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

We ni mpumbavu! wewe ndo mmiliki wa kampuni. umemwajiri tizeba awe managing director wa kampuni yako. unatembelea kanda mbili zilizochoka mpaka zimetoboka kisiginoni, wakati yeye anatumia rasilimali yako kwa vitu vya gharama sana vya anasa alafu unaona ni stahili yake. kama siyo upumbavu ni nini?
 
kwa wenyeji wa dar mtusaidie kujua nyumba ya 4m per month ina ubora kiasi gani?



mkuu acha tu. hii nchi ni tabara. hata akili ya kawaida haielekezi hivyo. mbona nyumba ziko nyingi nzuri tu, lakini who cares about our money. ipo siku watu watajifunga mabomu. too much tired.
 
Aulizwe Mkapa na Magufuli.. Sasa Tizeba na wadhifa wake angekaa wapi..
Naamini wengine wana bills kubwa zaidi. Nenda hata Courtyard hotel..
Kabla ya kuteuliwa alikuwa anakaa wapi? Kwani JK ana wake wangapi kujaza magogoni yote? Kwani hiyo kazi hakuna mtu mwingine mwenye nyumba Dar anaweza kuifanya?
 
hii laana ya kuuza nyumba za serikali,,haitamwacha mkapa na magufuli..siku ya ukombozi ikifika,hata kama wamekufa watafufuliwa na kushtakiwa!
 
Tenende Niaelewa frustration yako. Lakini kumbuka bado ni mfumo wa Serkali na siyo mtu binafsi kupangishiwa nyumba. Yeye Kama mteule walipaswa kumpa nyumba whether ni ya Serkali au ya kupangisha kwa watu binafsi. Kama angeikataa (kama tulivyoambiwa kwa waziri wa mambo ya ndani wakati ule)hapo kingekuwa suala lingine.
Ndugu watu hapa wanahoji uzalendo wake uko wapi. Alikuwa na uwezo wa kutambua hilo sio jambo jema kwa nchi na wizara anayoiongoza.. Nashindwa hata kuelewa unachokitetea hapo ni nini... Mwezi mmoja au hata wiki mbili zikipita tangu aanze kuishi hotelini alipaswa kuhoji tena kwa nguvu zaidi mahala pa kuishi tofauti na hotel. Tunaona baadhi ya viongozi wakitoa mifano ya kukataa mambo yanayoiongezea nchi gharama zisizo za ulazima kama vile Pinda alivyokataa V8,huo ni utambuzi wa lililo jema kwa nchi yako
 
Tutakula wapi? Mlituchagua wenyewe sasa mnashangaa nini?Mbona mpaka tuifilisis hii Tanzania ndio tutaanza kuota kuondoka!
 
Hapo kwa Unafki tunaongoza bila shaka la kupanda train ni unafki uliopitiliza. Nashangaa wanafunika tusione wakati tunajua sasa sijui wanafanya nini, Wanadhani wafanyayo ni kizani hautoni wala kujua na wanakuja na kutudanganya kuwa Wanatumia usafiri wetu sisi makabwela. Hii ndo Tz bwana kuna walalahoi na walalahai kam wao waliopewa dhamani ya kusimamia na kuitekeleza ilani za chaguzi zao. Sasa hiyo Milioni 100 ipo katika bajeti gani hasa toka zile walizojadiuli Bungeni???
 
Ndugu watu hapa wanahoji uzalendo wake uko wapi. Alikuwa na uwezo wa kutambua hilo sio jambo jema kwa nchi na wizara anayoiongoza.. Nashindwa hata kuelewa unachokitetea hapo ni nini... Mwezi mmoja au hata wiki mbili zikipita tangu aanze kuishi hotelini alipaswa kuhoji tena kwa nguvu zaidi mahala pa kuishi tofauti na hotel. Tunaona baadhi ya viongozi wakitoa mifano ya kukataa mambo yanayoiongezea nchi gharama zisizo za ulazima kama vile Pinda alivyokataa V8,huo ni utambuzi wa lililo jema kwa nchi yako
Nafikiri kuna mambo mengi tusiyoyaelewa. Unajuaje kuwa Mh. Alikuwa ahoji. Sidhani Kama mtu mwenye familia anafurahia kukaa hotelini kwa kipindi chote hicho. Je unafikiri kurudisha V8 kulisaidia?. Si bado ana V8 ingine na aliyorudisha bado iko serkalini ikiingiza hasara ileile kwa walipakodi. Ningeona sahihi Kama angebadilisha mfumo kuhakikisha Serkali haitumii haya maV8 yanayowagharimu walipakodi.
 
Back
Top Bottom