Waziri Stergomena alivyozindua Kamati Tendaji ya JKT

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Waziri akizindua Kamati Tendaji.jpg


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Stergomena Lawrence Tax (Mb) amezindua Kikao cha Kwanza cha Kamati Tendaji ya Jeshi la Kujenga Taifa, baada ya kuiunda rasmi tarehe 12 Agosti, 2022.

Kikao hicho cha kwanza na cha aina yake, kilifunguliwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kililenga kuzindua rasmi Kamati hiyo na kupitia majukumu ya Kamati yake.

Kamati hiyo inaundwa na Waziri wa Ulinzi na JKT, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa JKT, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT pamoja na Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo JKT.

Waziri ameiunda Kamati hiyo Tendaji kwa mamlaka aliyopewa na Kanuni Na. 5 ya mwaka 1964. Majukumu yake ni kama yalivyoainishwa katika Kanuni rejewa.

Akifungua Kikao hicho, Mwenyekiti aliwapongeza wajumbe wa Kamati kwa kuteuliwa kwao na kuwasihi kutoa ushirikiano katika kutekeleza kwa ufanisi utendaji kazi wa JKT, ili malengo ya Kamati hiyo yaweze kufikiwa. Aidha, Mheshimiwa Waziri amewapongeza waandaji wa kikao kwa maandalizi mazuri yaliyofanikisha kufanyika kikao hicho cha kuhistoria.

Kamati Tendaji ya JKT.jpg


Jeshi la kujenga Taifa lilianzishwa mwaka 1963 kwa Sheria Na.16 ya Mwaka 1964. Likiwa na majukumu makuu matatu yakiwemo Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali pamoja na Ulinzi wa Taifa. Chini ya Sheria hii, kanuni mbalimbali zimetungwa kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya JKT.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom