Waziri Sitta achongewa kwa Lowassa

Waziri Sitta achongewa kwa Lowassa

lol! acha kujibaraguza banaa!!! kwa kujifananisha na akina Socrates na Plato. Subiri watu wakupigie debe siyo kujipigia debe mwenyewe. Kwa taarifa yako ni ----- tu ambao ndio unashusha hapa kutokana na uwezo wako finyu wa kuchanganua mambo.

Madudu kama haya unayoyaandika ndiyo yanayoonyesha uwezo wako wa kutafakari kwa kina kabla ya kuandika pumba zako.

Uliandika:
Hivyo hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni "mshindi halali"

Ungekaa chini na kutafakari kwa akina athari za kuwa na Rais ambaye ameingia madarakani kwa njia za haramu basi kamwe usingeandika pumba zako hapo juu, lakini mimi nitakusaidia kwa kukupa mifano hai ya athari za Kiongozi kuingia madarakani kwa njia haramu.

Kikwete inajulikana jinsi alivyobebwa na kundi lake la mtandao katika kutafuta mgombea toka CCM katika uchaguzi Mkuu wa 2005. Kikwete na kundi lake la mtandao walijua fika kwamba kamwe kwenye utendaji asingeweza kusimama na SAS katika kinyang'anyiro kile na hivyo kuamua kukusanya mabilioni ya pesa toka kwa mafisadi mbali mbali nchini ili kutumia pesa zile chafu katika kumchafua SAS na pia katika kununua wajumbe wa CCM ambao katiba ya chama chao iliwapa nafasi ya kumteua mgombea toka CCM.

Kikwete alipoingia madaraka wengine walithubutu kumuita kwamba ni "chaguo la mungu" kutokana naahadi zake chungu nzima zikiwemo "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya", "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" "Nitaipitia tena mikataba ya uchimbaji wa madini yetu" na nyingine chungu nzima ambazo hadi hii leo hakuna hata moja aliyoitimiza.

Kama utakumbuka mwanzoni tu mwa awamu yake kukaibuka kashfa kubwa ya EPA ambayo mimi nilidhani Kikwete angeitumia kashfa ile kujijengea heshima kubwa sana kwa kuamua kuwashughulikia mafisadi wale wa EPA bila kuwaonea huruma ya aina yoyote ile, lakini hakufanya hivyo. Tukaanza kusikia kauli mbali mbali za kustaajabisha kama toka kwa Pinda, "Wahusika wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto", "Asilimia kubwa ya pesa za EPA zimerudishwa na wahusika na zimeshawekwa katika bank account" lakini Watanzania tulipoomba majina ya waliorudisha pesa na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja na pesa zile zimewekwa katika Bank ipi na bank account waiweke hadharani. Kikwete na Serikali yake wakashindwa kutimiza hata moja ya maombi ya Watanzania. Mpaka leo hakuna ushahidi wowote ule kama kweli pesa za EPA zilirudishwa kama inavyodaiwa.

Kukawepo na sakata la Richmond/Dowans ya swahiba wake Rostam Azizi, pamoja na kampuni ile kuidanganya Serikali kwamba ina HQ yake Houston, Texas na ina uzoefu wa muda mrefu katika ufuaji wa umeme na hivyo kujipatia mkataba mkubwa toka TANESCO wakati nchi ilipoingia gizani kampuni ile ikashindwa kuzalisha hata tone moja la umeme pamoja na kwamba ilikuwa ikiendelea kulipwa mabilioni ya pesa toka TANESCO. Kama utakumbuka Kikwete alikuwa kimya kwa muda mrefu wakati wa sakata la Richmond/Dowans kitu ambacho kiliwastaajabisha Watanzania wengi kuona Rais wao yuko kimya katika sakata lenye uzito mkubwa katika maslahi ya nchi.

Mwaka jana kukaibuka sakata lingine la "Mabilioni ya Uswissi" Kikwete na serikali yake hadi hii leo wanajizungusha zungusha katika kuwataja wahusika wa pesa hizo na pia kuhakikisha zinarudishwa nchini huku ukiwepo ushahidi wa kutosha kwamba kweli zimerudishwa nchini

CCM ikaendelea kuyumba yumba huku Watanzania wengi tukiita "Chama cha mafisadi" ndipo miaka michache iliyopita Kikwete na chama chake wakaibuka na kauli ya "Kulivua gamba". CCM walidai wanachama mbali mbali wakiwemo, Lowassa na Rostam, wa chama chao ambao wamekichafua chama kutokana na ufisadi watafukuzwa chamani katika jitihada za kukisafisha chama ili kiondokane na sifa mbaya miongoni mwa Watanzania walio wengi kwamba ni "Chama cha Mafisadi" lakini kama kawaida hakuna lolote lile lililofanyika.

Sababu kubwa ya kushindwa kuwashughulikia wahusika wa EPA, Richmond/Dowans, Rada ya akina Mzee wa Vijisenti, Wakwapuaji wa nyumba za Serikali, Wakwapuaji wa Kiwira Coal Mining, mabilioni ya Uswiss, Meremeta, Kagoda, wachafuzi wa CCM hadi kufikia kuitwa "Chama cha Mafisadi" ni kwamba uongozi wa nchi yote umeoza. Huwezi ukamnyooshea kidole mwenzio kuhusu uchafu wake wakati naye anajua uchafu wako ambao akiamua kuuanika hadharani basi nchi itawaka moto. Haya ndio matatizo ya kuwa na kiongozi aliyeingia madarakani kwa njia haramu kwa kutumia mabilioni ya pesa chafu ili kujisafishia njia kuelekea Ikulu. Siku zote atakuwa muoga kutimiza wajibu wake kama Rais pamoja na nguvu kubwa alizopewa na katiba ya nchi.

Huyu fisadi wako naye Lowassa hana uwezo wowote kama kiongozi. Ukimuuliza katika miaka yote aliyokuwa ndani ya Serikali ni lipi ambalo amelifanya linalostahili Watanzania kujivunia nina hakika hana hata moja ambalo Watanzania tunaweza kusema hili lilifanywa na Lowassa Watanzania tunaweza kujivunia kwa miaka mingi ijayo. Hivyo naye atatumia mabilioni ya pesa chafu zitakazokusanywa na mtandao wake kama ilivyokuwa 2005 ili kujisafishia njia ya kuingia Ikulu 2015. Atatumia ubavu wa vyombo vya dola kuwatisha Viongozi wa CDM, kuvuruga kampeni zao, kuhonga pilau, kanga, kofia, fulana na pombe. Na akiingia kule haya tuliyaona katika hizi awamu mbili yataendelea kama kawa bila kuwepo tofauti yoyote ile, kwa maneno mengine nchi kuendelea kuangamia pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao.

Tukitathimi hii awamu ya Kikwete hakuna hata moja la ahueni. Usafiri wetu wa ndege, reli, barabara na majini bado ni wa kukatisha tamaa kupita kiasi, Kiwango cha elimu nchi mwetu kinazidi kushuka katika kiwango cha kutisha mwaka hadi mwaka, Hospitali zetu mambo ni hovyo hovyo yaani zinatisha kusema kweli, upatikaji wa huduma muhimu kama maji na umeme hauna ahueni yoyote. Kwa kifupi grade anayostahili Kikwete katika hizi awamu mbili ni F au kama ni marks ni SIFURI.

Wewe muandika pumba hapa jamvini Hivyo hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni "mshindi halali" huoni athari zote zinazosababishwa na kuwa ni kiongozi aliyepatikana kwa njia za haramu. Kwako wewe hata akikiuka vipi taratibu za uchaguzi zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ambayo si huru ali mradi tu Tume hiyi ambayo si huru ikimtangaza kwamba ndiye mshindi halali basi kwako wewe muandika pumba mchezo ndio umekwisha!!!! Jitahidi kutafakari mambo kwa kina si kwa kuyaangalia juu juu tu ili ujue athari zake.

Nadhani kuna haja katika katiba mpya kuwepo na kipengele kitakachosema kwamba Mtanzania yeyote yule ambaye aliwahi kushika nafasi ya juu Serikalini, Taasisi yoyote ile ya umma, private company ambaye alijiuzulu au kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ambayo iliingizia Serikali/taasisi ya umma/private hasara kubwa basi Mtanzania huyo kamwe hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ile kuanzia Ubunge hadi Urais. Hii itatusaidia kupunguza mafisadi wanaounyemelea Urais ili wakaendeleze ufisadi wao.
Mkuu BAK, kama kipimo cha GT ingekuwa ni kwa kuandika tuu au kufanya uchambuzi makini, kwa uchambuzi huu, hakika na wewe ni Great Thinker pia! kwa sababu uchambuzi wako huu, umeweza kuoanisha madhara ya uchaguzi wa kiongozi asiefaa na matokeo yake, asante kwa hili!.

Now bach to basics, "uhalali" wa urais is a legal process, kuna uongozi wa aina mbili, "de jure" na "de facto", de facto ni uongozi wa unaopatikana kwa mapinduzi na mara nyingi ni wa kiimla!, hata uongozi huu ukiapisha ni "halali!". De jure ni uongozi unaopatikana kwa uchaguzi, hata kura zikiibiwa vipi, anayetangazwa mshindi akishaapishwa ni kiongozi "halali!", hivyo maneno haya "hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni 'mshindi halali'", niliyasema, ninayasema na nitaendelea kuyasema bila kubadili chochote!.

Kitu ambacho nakukubalia, ni neno "pumba" kwa sababu ni relative na uelewa wako!, Hata Galileo Galilei, alipogundua telescope ya kusema dunia ni duara sio tuu alichekwa na kudhihakiwa, bali alinyogwa kwa kuukashifu uumbaji wa Mungu wa dunia bapa!, hivyo kuniita "pumba" its ok with me, hainisumbui na naahidi kuendelea kumwaga pumba za aina hii as long as hizo pumba ni hard facts!.

Mkuu BAK, naomba tusiendelee kuurefusha huu mjadala, tufike mahali, tukubaliane kutokukubalia, naomba nimalizie kwa kukuuliza swali moja tuu, please be honest from your heart (dhamira),
Jee Rais Jakaya Kikwete ni rais Halali wa Tanzania?.
NB. Siulizii kama amepatikana kihalali, no, naulizia kwa hali ilivyo sasa, kuna nchi inaitwa Tanzania, na rais wake ni Jakaya Mrisho Kikwete, jee ni rais halali?, jibu YES or No. Swali hili lina maksi 100 na halihitaji maelezo yoyote!.

"Jee Rais Jakaya Kikwete ni rais Halali wa Tanzania?".

Thanks.

Pasco.
 
Back
Top Bottom