Waziri Sitta achongewa kwa Lowassa

Waziri Sitta achongewa kwa Lowassa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya hiyo.

Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang'anyiro cha Urais 2015.

Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya wanasiasa hao wawili.

Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.

"Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,"alisema Shyrose Bhanji.

Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.

"Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo wake," aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao katika kujadili mambo ya jumuiya.

"Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao," alisema Mwinyi.


Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi; "Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia baadaye."

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba madai hayo si ya kweli.

"Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani? Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?

"Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki," alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki.

Imeandikwa na Beatrice Moses na Patricia Kimelemeta, Mwananchi, Dar
 
Mnafiki 6 anakwenda kuumbuka. Alisahau ule msemo kwamba maji hupigwa bara na hupiga Pwani pia.
 
Ni jambo la ajabu sana hakuna sera ya Afrika Mashariki.Sijui ni kwa nini hata kuwe na separate potfolio

Hata wizara ya Mambo ya nje tumeshasema sera inatakiwa iundwe upya.Ukitembelea balozi zetu nje utaona vituko tu

Hata Hivyo Lowassa sioni kama anaweza kuleta changes maana hata akiwa waziri mkuu aliyaona madudu haya.Busara za ghafla mda huu amezitoa wapi kama sio conflict of interest tu?
 
Mimi siamini kama hao wabunge wa EAC wanaenda huko Bungeni hawajui kitu gani wanachoenda kuongea na kama ni kweli basi kuna mamtaizo makubwa nchi hii siyo tu kujua sera gani za nchi za kuzitetea katika hilo bunge.
 
Mnafiki 6 anakwenda kuumbuka. Alisahau ule msemo kwamba maji hupigwa bara na hupiga Pwani pia.
Tatizo la unafiki , mnafiki hana haya.Sita anatapatapa tu.Anajivunjia heshima na utu wake.Wakati watu wameisha sahau yaliyotokea wakati wa harakati za uchaguzi yeye bado ana endekeza makundi na misemo ya kejeli.Mtu mzima OVYO.Inatakiwa ajitambue kuwa nafasi aliyonayo kitaifa hamruhusu kuwa na tabia ya vijiweni .Lakini naona Tabora kuna tatizo hata mbunge mwingine wa huko PROBLEM.Mwache atamjua Masai
 
tatizo la unafiki , mnafiki hana haya.sita anatapatapa tu.anajivunjia heshima na utu wake.wakati watu wameisha sahau yaliyotokea wakati wa harakati za uchaguzi yeye bado ana endekeza makundi na misemo ya kejeli.mtu mzima ovyo.inatakiwa ajitambue kuwa nafasi aliyonayo kitaifa hamruhusu kuwa na tabia ya vijiweni .lakini naona tabora kuna tatizo hata mbunge mwingine wa huko problem.mwache atamjua masai

unazungumza pumba tu atamjua masai ndo nani katika nchi hii? Wewe na huyo mwizi wako wa mali za umma. Hasara alizotutia hamzioni kila siku masai masai masai ondoeni upuuzi wenu mnawatia umasikini wa tanzania kila kukicha na masai wenu fisadi.
 
Lowasa ni nani???

Ni mwenyekiti wa kamati ya mbunge ya mambo ya nchi za nje, ni mbunge wa monduli, ni waziri mkuu mstaafu na ni mgombea urais ajae kupitiua tiketi ya CCM na mwisho ni mtanzania anayepakwa matope kutokana na ukwasi wake!
 
Ni jambo la ajabu sana hakuna sera ya Afrika Mashariki.Sijui ni kwa nini hata kuwe na separate potfolio

Hata wizara ya Mambo ya nje tumeshasema sera inatakiwa iundwe upya.Ukitembelea balozi zetu nje utaona vituko tu

Hata Hivyo Lowassa sioni kama anaweza kuleta changes maana hata akiwa waziri mkuu aliyaona madudu haya.Busara za ghafla mda huu amezitoa wapi kama sio conflict of interest tu?

Ni nani huyo sasa atakayeweza kuleta hayo mabadiliko kama wote hawawezi?
 
wote EL na 6 ni wanafiki.EL kalitumbukiza taifa kwenye ufisadi mkubwa wa richmond,6 naye akauzima mjadala wake usiindelee bungeni.alichotaka 6 ni kujiuzulu kwa EL tu,lakini hakuangalia maslahi ya taifa kwa kusimamia utekelezaji wa maazimio ya bunge.wa kulaumiwa hapa ni JK na CCM kwa kuendelea kuwapa madaraka.wote EL,6 PAMOJA NA CCM HAWATUFAI.
 
Ni nani huyo sasa atakayeweza kuleta hayo mabadiliko kama wote hawawezi?

Ni chama mbadala cha maCCM, kitakapochukua dola, I meant Chadema 2015 itaweza, baadaa ya siku mia, sera zote zitaanza kupitiwa upya.

Only Chadema can do.
 
Ni jambo la ajabu sana hakuna sera ya Afrika Mashariki.Sijui ni kwa nini hata kuwe na separate potfolio

Hata wizara ya Mambo ya nje tumeshasema sera inatakiwa iundwe upya.Ukitembelea balozi zetu nje utaona vituko tu

Hata Hivyo Lowassa sioni kama anaweza kuleta changes maana hata akiwa waziri mkuu aliyaona madudu haya.Busara za ghafla mda huu amezitoa wapi kama sio conflict of interest tu?
Eti busara za ghafla zinatoka wapi? umesahau wewe ulikua kiongozi wa masalia ghafla ukawa mzalendo na mtiifu wa Dr.
Acha unafiki kijana kila siku nakwambia au ndo nyani haoni .........? wewe gafla umekua mzalendo kwa Dr iweje kwa EL asiweze kugeuka ghafla na kua na busara,au kisa wewe una masters ya INDIA?

EL amekua waziri mkuu kwa miaka isiyozidi 3 wewe ulitegemea kikubwa kipi kwa miaka miwili ya uwaziri mkuu wakati huo nchi ikiwa imetoka kwenye uchaguz mkuu.
Ni ushamba kubisha kila kitu,anyway labda ndio asili yako thats y unajikuta kila mara uko kwenye makund.
wanafiki kama wewe tumewaona wengi ila Mwisho wa ubaya ni aibu.
 
Ukishazoea kudesa wewe ni wa kudesa tuu ni sawa na mbunge wangu aseme kuwa simpi ushirikiano wa issue za kwenda present kwenye bunge.Yaani kwa statement kama iyo uyo mtu hafai kuwa muwakilishi.
Bse sio paper zile kusema unaenda kufeli kuna waziri naibu waziri katibu mkuu na takataka zingine pale wizarani mtu mzima na akili zako timamu wasema haupewi ushirikiano.Wakati issue zingine kwa lile bunge unatumia common sense tuu kuijibu ndo maana wakenya wanatuona vilaza ivi ivi haya mambo ya kupeleka watu vihiyo itatucost kila siku
 
Ni jambo la ajabu sana hakuna sera ya Afrika Mashariki.Sijui ni kwa nini hata kuwe na separate potfolio

Hata wizara ya Mambo ya nje tumeshasema sera inatakiwa iundwe upya.Ukitembelea balozi zetu nje utaona vituko tu

Hata Hivyo Lowassa sioni kama anaweza kuleta changes maana hata akiwa waziri mkuu aliyaona madudu haya.Busara za ghafla mda huu amezitoa wapi kama sio conflict of interest tu?

Separate portfolio/ Ministry umekuja kutokana na makubaliano ya mkataba wa EAC wa 1999 (EAC Treaty 1999, article 8(3)(a)) kwamba kila Nchi efungue Wizara itakayoshughulikia masuala ya EAC.nanukuu:
"3. Each Partner State shall -
(a) designate a Ministry with which the Secretary General may communicate in connection with any matter arising out of the implementation or the application of this Treaty, and shall notify the Secretary General of that designation".

Kuh. sera/mwongozo kwenye EAC na balozi zetu za nje ulitakiwa utokane kwenye sera mama ya TZ kuhusu mambo ya nje(TZ foreign policy). Ukipita kwenye website ya TZ ministry foreign affairs utakutana na outline ya "TZ foreign policy the case of economic diplomacy" Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation - Tanzania. Sasa sijui hii ndio comprehensive TZ foreign policy au la(wenye nayo watuwekee jf tuipitie). Cha msingi ni kwamba TZ inaitaji kuandika upya sera yake ya mambo ya nje.

Nakubaliana nawe Lowasa hawezi kulete changes zozote ni msanii tu, alikuwapo serikalini mda mrefu mpaka ngazi ya waziri mkuu je alifanya nini cha maana? zaidi ya kukwapua pesa za walipa kodi!. Ninamuonea huruma kutojitambua kwamba siku zake zilishapita.
 
Back
Top Bottom