Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Mar 30, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu


  na David Frank, Loliondo


  WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Watoto Sophia Simba, ameonja joto ya jiwe baada ya kuzuiwa na wananchi kumfikia Mchungaji Ambilikile Maisapila, kwa madai kuwa ‘alichakachua’ foleni kumfikia.

  Waziri Simba alifika katika kijiji cha Samunge majira ya alasiri (Alhamisi iliyopita), akiwa katika msafara wa magari manne na kutaka kwenda moja kwa moja kumwona Babu eneo alilokuwa akitolea tiba hiyo.

  Ghafla waziri huyo alivamiwa na kundi la watu wenye hasira ambao wengi wao walikuwa wamekaa kijijini hapo kwa zaidi ya siku saba, wakisota kumwona Babu.

  Mashuhuda wa tukio hilo la aina yake, waliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa Waziri Simba alizuiliwa kwani alitaka kumwona Babu muda mfupi tu baada ya kuwasili kijijini hapo bila kufuata foleni.

  “Watu hawakujali uwaziri wake, walimzonga na kumhoji imekuwaje amefika na kukimbilia kikombe bila kupanga foleni kama wanavyofanya wao. Uliibuka mzozo mkubwa kati yake na wananchi hao ambao baadhi walikuwa wakisema hovyo kwa hasira,” alisema shuhuda wetu.

  Wakati tafrani hiyo ikitokea, wasaidizi wa Babu pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji cha Samunge, walikimbia kwa hofu ya kupewa maneno makali na wananchi, hali iliyomlazimu Babu kusitisha tiba yake kwa muda kutuliza hali hiyo.

  Wakati akituliza hali hiyo, Babu akiwatahadharisha wananchi waliofurika kijijini kwake kwamba wanapaswa kuwaheshimu viongozi wanaofika hapo kwani mbali ya kupata kikombe, pia wanaratibu shughuli zinazohusiana na tiba hiyo ya ajabu.

  “Nawaomba muwaheshimu viongozi wanaokuja hapa kwani mbali ya kuja kupata tiba wanafika kuona namna ya kuboresha hali ya mazingira ili tiba hii iweze kuwa endelevu,” alikaririwa Babu akisema.

  Babu alimwongoza Waziri Simba kwenda kumpa kikombe pamoja na ujumbe wake na baada ya kupata tiba hiyo, waliondoka kurudi Arusha.

  Katika hatua nyingine siku chache tu baada ya Babu kusitisha huduma kwa watu na wagonjwa wanaotoka ndani na nje ya nchi, kumeibuka staili mpya ya magari kusafiri na kupeleka watu kwenda kijijiini Samunge kupitia njia za panya.

  Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mbali na barabara zilizowekewa vizuzi, yapo magari yanayotumia barabara ya Longido kupitia Ziwa Natron na kuingia moja kwa moja kijijini Samunge.

  “Pamoja na kuwepo vizuizi maalumu kama vile vya Arusha, Mto wa Mbu, Babati mkoani Manyara, Mugumu na Musoma mjini mkoani Mara, bado madereva watukutu wanafanya hila na kusafirisha watu na wagonjwa hao kupitia Longido na kuchepukia Ziwa Natron na kuunganisha moja kwa moja kwa Babu,” alisema mmoja wa viongozi wa wilaya ya Ngorongoro.

  Wakati hayo yakiendelea, magari zaidi ya 300 yamezuiliwa katika kizuizi cha Mto wa Mbu, huku zaidi ya magari 100 yakiwa yamekwama eneo la Melerani wilayani Monduli, yakiwa njiani kwenda Loliondo.

  Kuzuiliwa kwa magari hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mchungaji huyo ambapo aliomba wagonjwa wapya kusitisha kuingia Loliondo katika kipindi cha wiki moja.

  [FONT=&quot]Chanzo: Tanzania Daima.


  My Take:

  Wadau -- hii anavyofanya Babu ni sahihi -- kuwatetemekea wakuu wa siasa na serikali kwa visingizio ya kuboresha mazingira? ya sehemu hiyo

  Sasa kila kiongozi wa serikali ataruka foleni kwa kisingizio hicho -- hiyo dawa itawaponyesha?

  [/FONT][FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Babu ameanza kuvunja masharti yake kuhusu kuruka foleni?
   
 3. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ha ha ha, babu naye ameanza kuchakachua.

  Waziri Simba ni mama wa mikosi - hata kwa babu nako kaumbuliwa teh teh teh teh
   
 4. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa sharti la babu, Ukiruka foleni tu dawa haifanyi kazi, ni sawa na kunywa juice tu hivyo na wasi wasi viongozi wetu wengi haitawasaidia.

  wanapenda kutumia vyeo vyao kujinufaisha wao kwanza km ilivyo kwa mafisadi.

  Ufisadi hadi kwa babu hii imezidi.

  ingekuwa vyema wakapanga foleni na kuona adha na machungu wanyayopata wananchi wengine wangeshughulikia suala la miundombinu kwa haraka.

  Ila sasa kwa kuwa wanajipa kipaumbele wakibwia kikombe tu wanasahau wananchi wanyonge ambao wamekaa ktk foleni siku kibao.

  hawa ndio viongozi wetu, kila pahala utaona wao wanataka wawe mbele mbele.

  Nakumbuka Mwalimu Nyerere alikuwa akienda kupiga kura anapanga foleni na wananchi, lakini hawa wetu maphoto genic, waonekane ktk magazeti na vyombo vya habari.

  Kwa wale wanaochakachua foleni dawa haitawasaidia kamwe babu alishasema hilo.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kiutu uzima, babu anaona aibu pale wadau wa serikalini wanapozomewa!...nadhani akichekelea kitu kama hicho ataonekana chizi...Uso umeumbwa na haya jamani!!
  NDIYO MAANA ANAPOONA kiongozi amekiuka taratibu na anataka ahudumiwe mapema kuliko wengine, basi anaamua kumpa dawa ili aondoke na hali irudi kawaida!
  SASA suala la mtu huyo kupona au kutopaona hatuwezi kujua zaidi!
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Lakini alitamka hakuna kuruka foleni, ama sivyo dawa haitafanya kazi!
   
 7. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu binafsi mimi nilitamani sana kuona Babu anasimamia kauli zake hii ingemuongezea heshima na umakini wake.
  Hii yakubadilibadili kauli kama nikweli itazidi kumpunguzia imani kwa jamii husika (ikumbukwe kwa Mungu hakuna aliye zaidi ya mwingine).

  Na maswali kidogo bado najiuliza:_
  Alisema ukichakachua foleni dawa haitibu je ni kweli haitatibu?Kama haitawatibu heshima yake kwao iko wapi sasa?na kama itawatibu kwanini alisema uwongo?je anapanda nini vichwani mwetu?
  Vp na ile aliyosema kua haruhusiwi kuhama hapo alipo linaukweli ?
  Vp serikali ikimtingishia kiberiti kua kama hawezi kuhamia sehemu ambayo itafanya huduma yake iwe nyepesi kufikiwa na salama kijamii asitoe dawa kabisa ataweza kusimamia alichokisema awali?

  Maoni yangu ...Kama Babu anaouwezo wa kuvunja masharti aliyopewa na hakutakua na madhara kimatibabu basi asiwe na upendeleo au kama vp aongee na kina Mengi au Bakresa waijaze kwenye makopo ya maji ya ya Uhai, Dasani au Kilimanjaro yaingizwe kitaa!!
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wakati akituliza hali hiyo, Babu akiwatahadharisha wananchi waliofurika kijijini kwake kwamba wanapaswa kuwaheshimu viongozi wanaofika hapo kwani mbali ya kupata kikombe, pia wanaratibu shughuli zinazohusiana na tiba hiyo ya ajabu.

  "Nawaomba muwaheshimu viongozi wanaokuja hapa kwani mbali ya kuja kupata tiba wanafika kuona namna ya kuboresha hali ya mazingira ili tiba hii iweze kuwa endelevu," alikaririwa Babu akisema.


  Babu alimwongoza Waziri Simba kwenda kumpa kikombe pamoja na ujumbe wake na baada ya kupata tiba hiyo, waliondoka kurudi Arusha.

  Sasa mbona hakufanya hivyo babu?
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Babu alishajua kuwa Mama huyu hatopona kwa kuwa karuka foleni....akaamua kuokoa jahazi ili hali irudi katika ushwari wake
   
 10. g

  gwacha Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo ni swala la kiimani ndio maana ni vigum sana kwa walio wengi kuelewa,kwakua aliruhusiwa na babu mwenyewe hakuna tabu.maana yeye ndie aliyepewa mamlaka na MUNGU wake.
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Waziri huyo na msafara wake wamekunywa juice na si tiba kwa mjibu wa babu
   
Loading...