Waziri Ndugulile, afungua kikao maalum cha viongozi wa Shirika la Posta Tanzania

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
UFUNGUZI WA KIKAO MAALUM CHA VIONGOZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KWA AJILI YA KUTATHIMINI UTENDAJI KAZI WA SHIRIKA KWA MWAKA ULIOPITA 2020/2021 NA KUKUBALIANA MALENGO YA MWAKA HUU 2021/2022

Shirika la Posta linaendelea na kikao maalum cha tathimini ya utendaji Kazi kwa Shirika la Posta Tanzania kwa mwaka 2020/2021 na kukubaliana malengo ya Mwaka 2021/2022.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe Dkt. Faustine Ndugulile. Waziri amewapokenza shirika la Posta kwa kuandaa Mkutano huo wa tathimini kwa watendaji wakuu wa Shirika la Posta ili wote kwa pamoja waweze kujitathimini na kupanga pamoja muelekeo wa Shirika bila kuachwa nyuma katika kutafsiri kwa vitendo uendeshaji wa Shirika.

"Tunahisi kuwa tunaowapa majukumu wanaelewa majukumu yao ila kwa haya mafunzo yatakuwa chachu kubwa katika kuongeza ufanisi na utendaji wa Shirika la Posta Tanzania" alisema Mhe. Dkt Faustine Ndugulile.

Pia Kaimu PostaMasta Mkuu ndg Macrice Daniel amesema lengo la kuu Mkutano huu wa siku tano kwa watendaji wakuu pamoja na mameneja wa mikoa wa Shirika la Posta Tanzania ni kujitathimini na kupanga pamoja namna bora ya kuendesha shirika la Posta Tanzania katika misingi yenye weledi na ushindani katika kuwahudumia Wananchi ndani na nje ya Nchi.

Malengo mengine ya mkutano huo alisema Kaimu PostaMasta Mkuu ndg Macrice Daniel ni kama vile:-

1.Kuwapatia mafunzo ya uelewa wa kiungozi na kusimamia rasilmali zetu zilizopo katika mikoa yao Tanzania nzima.

2.Kubadirisha uzoefu kutoka katika taasisi iliyofanikiwa kwa vitendo na taasisi hiyo ni Benki ya Posta. Mkurugenzi wa Benki ya Posta atatupitish katika siri ya mafanikio kwa vitendo waliyoipata Benki hiyo.

3.Kupata mafunzo ya vitendo kutoka katika mfumo wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ili na sisi tupate uelewa wa kutumia mfumo huo wa Serikali katika kutoa huduma zetu kwa wananchi.

4.Kujifunza Itifaki na tabia za kistaarabu katika kutoa huduma kwa Wananchi kutoka chuo cha diplomasia.

5.Kupata mafunzo ya maswala ya utunzaji wa siri za serikali na kula kiapo cha uadilifu.

6.Kupata uelewa wa pamoja katika mifumo ya TEHAMA ya Shirika la Posta Tanzania wenye lengo la kutoa huduma zetu Kidijitali zaidi na kurahisisha ufanyaji Kazi kwa watendaji wakuu wa Shirika pamoja na mameneja wa Shirika la Posta Tanzania mikoani.

7.Kujadiliana na kufanya tathimini ya Shirika kwa Mwaka 2020/2021 pamoja na kutambua mchango wa wafanyakazi hodari na kuwapatia zawadi wakati wa sikukuu ya Mei mosi mwakani.

8.Pia katika kikao Kazi hichi cha mafunzo tumepanga kupata nasaa za wazee waliokuwa wafanyakazi wa Posta wakati huo ili kubata uzoefu kutoka kwao namna walivyoweza kuliendesha shirika la Posta Tanzania na namna walivyokabiliana na changamoto wakati wa utendaji wao.

#MkutanoWaTathiminiNaKupangaMwelekeoWaShirikaLaPostaKwaMwaka2021/2022.

IMG-20210805-WA0243.jpg
 
Shirika limejaa mijitu MICHAWI kweri kweri yalimroga na kumuua dada mmoja anaitwa Mage Mabula mchana kweupe hapo Mbeya.
 
Back
Top Bottom