Waziri Ndalichako awataka watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais Magufuli

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Watanzania wametakiwa kushikamana kwa kufanya Kazi kwa bidii kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili Taifa liweze kutumiza malengo ya kufikia uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya 19 ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere linalofanyika katika chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Ndalichako amesema Wizara itaendelea kukienzi Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kiendelee kuwa Kitovu cha maadili katika kuwajenga Viongozi na vijana ikiwa ni pamoja na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila amewataka viongozi na wanafunzi kuhakikisha wanakitumia chuo hicho kwa ufanisi ili kupata mafunzo yanayohusu uzalendo, uadiifu na kuwa mafunzo yanayotolewa chuoni hapo ni yale ya muda mfupi na mrefu.
Prof. Mwakalila amesema kila mwaka chuo hicho huandaa maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati wa Baba wa Taifa kwa Lengo la kujitathmini kama Taifa, tumetoka wapi na tuko wapi.
Katika kumbukizi hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo ile inayohusu Uhuru na Maendeleo katika kuelekea uchumi wa Kati, umuhimu wa uzalendo na uadilifu, umuhimu wa misingi ya Azimio la Arusha katika kustawisha Viwanda vya ndani.
 
Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Juhudi zote za kuwalazimisha watu waunge mkono mnahofia nini? Kuna kitu hakikubaliki mnalazimisha! Why all that "unga juhudiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, why all that force?
 
Ataachaje kumpromote hata kama anafany upupu wakati ndo anamfanya aende toilet!
 
Kwa vile hajui huku chini tunasumbukaje kupata mkate wetu wa kila siku muache aendelee kutuhimiza kuunga juhudi
 
Mbona matangazo mengi sana ya "nimependeni"?

Mtu hua haombwi kupendwa....Upendo na respect inakuja tu naturally...

Ukiona mtu anaji-promoti sana kuna walakini mkubwa sana kuhusu yeye!
 
Ukiona baba nyumbani kanunua vikombe vya chai vya udongo halafu mama anasema watoto tumpongeze baba kwa kununua vikombe basi jua nyumba hiyo ina uhaba wa mafanikio, yaani jambo Dogo linageuzwa kuwa mafanikio.
 
Back
Top Bottom