Waziri Ndalichako akijibu kuhusu mgawanyo wa mikopo TBC

Unapoona profesa anakwepa kujibu swali hapo ujue MAJI yamezidi unga! aliulizwa kuwa hiyo idadi ya wanafunzi ambao mtawapa mkopo maana yake ni uwezo wa serikali umeishia hapo au ni kwamba waliobaki hawana vigezo? Hilo swali kalisepa!
Unapoona profesa anaongea with zero confidence hapo maji yamezidi unga! Wote tunaijua confidence ya profesa, lakini kwa suala hili amekuwa mdogo kuliko piliton! Hakuthubutu kuitazama camera ili awatazame watazamaji watarajiwa machoni!
Suala hili linahitaji utashi toka mamlaka za juu! Huyu mama tumsamehe bure!
Serikali iwe wazi! kama kwenye gudulia hamna kitu semeni! Japo watanzania watajiuliza kulikoni bomberdier zilipewa kipaumbele kuliko elimu?
Bomberdier Nazitaka sana ila elimu naitaka zaidi!
 
silijui vizuri hili sakata na naogopa kulisogelea kwa karibu kwakuwa linaweza kuniumiza sana na wiki yangu ikawa vibaya.
serikali irudi na kuwasaidia watu hawa sio wengi mimi nauhakika wakiwapa wote mikopo itawezekana kujenga ushawishi na sisi tunaodaiwa tulipe haraka.
sio siri kuna vifo vinatokea katika taasisi za elimu kutokana na njaa achilia mbali umalaya usiotegemewa na hili linatokana na jinsi tulivyowalea watoto wetu.
hivyo serikali iangalie tusije kuangamiza kizazi hiki kwa ubahili usio kuwa na maana hizi si hela nyingi kwa serikali inayowapenda wananchi wake.
kama tumekosea tusione aibu kurudi nyuma na kufanya marekebisho hali ni mbaya sana kwa wadau hawa.
please jitahidini tafadhali
Ni kweli mkuu tunasema elimu inazalishwa vyuoni ila kwa kadri siku zinavyosogea na hali ilivyo sasa vyuo vinaweza vikazalisha watu wa ajabu ajabu kama. ........ kunahitajika umakini mkubwa sana kulishulikia hili la vijana wetu
 
Back
Top Bottom