beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amewataka wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu kuona umuhimu wa kulipa, na wenye fedha wasisubiri kukatwa 15% ili Wanafunzi wengine waweze kunufaika na kupata Ajira.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Esther Matiko aliyehoji ni lini Serikali italeta mabadiliko ya Sheria ili kupunguza makato kufikia angalau 8%, Waziri Ndalichako amesema Mnufaika anakatwa 15% na kubakia na 85%
Ameeleza, "Tukumbuke kwamba Mkopo wa Bodi ndio uliotangulia kabla ya Mikopo mingine, na kwa Kanuni Utumishi, Mtumishi anatakiwa abaki theluthi moja ya mshahara"
Aidha, ameeleza kuwa, lengo la kuanzisha mfuko wa Mikopo ilikuwa ni watu wafanye marejesho, Mikopo ijiendeshe yenyewe na kutosheleza kuwapatia Wanafunzi wengine.