Waziri Nchimbi alaaniwa na Wazanzibari! Maalim Seif amjia juu...

Ugaidi maana yake ni nini? Inaonekana mleta mada na watu wengi ni mbumbumbu kabisa. Ugaidi ambao kwa kiingereza unaitwa terrorism, neno hilo linatokana na neno terror. Ni vitendo vinavyofanywa, mara nyingi vya mauaji, vinavyofanywa ili kujenga hofu kwa jamii fulani au jamii yote ya mahali hapo kwa nia ya kulazimisha jambo fulani.


Je mauaji na uchomaji makanisa Zanzibar, unafanywa kwa lengo gani kama siyo kuwatisha wakristo, waone kuwepo kwao Zanzibar ni hatari, na dhamira ni kuwafanya waogope? Huyu aliyeandika waraka huu kama si hayawani basi lazima ni punguwani wa kiwango cha hali ya juu kabisa. Hana akili, hana elimu, hana ufahamu, hana hekima wala hana utu, na hana uzalendo na upendo kwa jamii ya Wazanzibari na Watanzania wote.

Nchimbi hakumaanisha dini yeyote kwa neno ugaidi, halikadhalika mleta mada !
Ila unapolihukumu hilo jambo ni ugaidi wakati hujaanza hata hatua za upelelezi unakuwa na maana gani ?
Kwa mfano angesema nitukio la kijambazi ungeelewaje ?
 
Mi nina wasi wasi huyu maalim ni mfadhili kama yule marehemu mwenye madevu.
 
KAULI yake ndIo ya kitaalam sababu tukio limetokea kutokana na matishio ya vipeperushi vyao, kusema UGAIDI ni kuwaweka waislam on safe side kuwa sio wote but few(magaidi). usiwe UNAPINGA kila kitu, YOU BETTER CHANGE...
 
MHALIFU anaweza kuitwa majina mengi tu ili kutoa picha kuwa amekosa ubinadamu. Tukianza kubishana kuhusu tafsiri na namna ya kuwapa jina zuri zaidi wahalifu ni dalili kwamba hata kwenye uchunguzi wa jambo hilo hatutakuwa wamoja.

I salute you mama Porojo, sijui nini kimekutokea but recently umekuwa ukiandika thread zilizojaa hekima na busara tupu bila kuegemea upande wowote.
 
Hiyo ni kauli yako na porojo za kigalatia tu ! Paulo pia alikuwa akiwauwa wafuasi wa Yesu !
Yani hata Waislamu mkae wenyewe lazima tu muanze kuchinjana.Hata Zbar mkimaliza Wakristo mtaanza kubaguana huyu Msunni na huyu Mshia na kuanza kuchinjana kama wenzenu wa uko Pakistani na Iraq.
 
NAPITA TU ila tatizo la Nchimbi anapenda sifa mno Waziri ambae tutajuta na kumlilia endapo tukimkosa tehe tehe tehe tehe.
 
Wewe si uliletwa kipindi kile 1995 kuja kupiga kura kusaidia CCM ishinde. Ndio umehamia moja kwa moja? Kama ZNZ ingekuwa iko hivyo unavofikiri si ingekuwa umeshahama au una jamaa wa Kizungu kule Kiwengwa?

Vyovyote iwavyo, mada ni zanzibar naijua na labda zaidi yako wewe na nimeishi uswahilini sana magogoni kidatu wapemba wanahamia nipo, na kila kitu na mawazo ya wengi nayajua...
 
Yule aliyekoswa na risasi naye alikuwa na matatizo gani. Huko Zanzibar huwa munalipiza kisasi kwa bunduki kwa watu wangapi mpaka sasa?? Wasilete kupotosha na kinachotakiwa ni uchunguzi huru na makini. Hawa wameshajua kuna kujulikana ndo maana wanakuja na matusi ya kijinga jinga. Taasisi huru za uchunguzi acheni zifanye uchunguzi na mwisho wa yote itajulikana tu..
 
DR.NCHIMBI USIPALILIE FITNA ZA KIDINI ZANZIBAR
images

Juu: Dr Nchimbi akilaaniwa na Wazanzibari kwa kutoa hukumu
kabla hata uchunguzi wa mauwaji hayajaanza!


Tumesikia na kupokea kwa masikitiko makubwa kuuwawa kwa kupigwa risasi Padri wa Kanisa la Katoliki ka Beit-El- Ras, Fr.Evarist Mushi.

Hakuna anayependa kuona kifo cha namna hii, au kufurahia. Pia hakuna dini inayoruhusu hayo kufanyika.

Lakini tumeshangazwa sana kusikia kauli ya Waziri wa Mambo ya Nchi, Dr.Emmanuel Nchimbi kutoa hukumu kabla ya hata upelelezi. Nchimbi umesema kuwa tukio hili ni la kigaidi. Hapo tayari umeshaamua na kutoa fatwa. Sasa ina maana gani kusema kuwa upelelezi utaendelea au hadi kufikia kusema kuwa utaomba msaada w anje ya nchi ili kusaidia upelelezi?


Bwana Nchimbi, kisheria na taratibu za kazi hukutakiwa kusema hayo, na wallah ingalikuwa ni nchi inayofuata sheria — umma ungalikutaka ujiuzulu.

Bahati mbaya sana umekuta umma wa Wazanzinbari umejaa ujinga, umbeya, usaliti na ushoga, plus na ule wa Watanzania ndio huo uliojaa ujinga wa kupindukia na hatimaye umeletwa huku kwetu Zanzibar.


Kwa nini useme ni ‘ugaidi’. Kanisa linaamini kuwa waliofanya hayo ni UAMSHO (kwa sasa ndio chaka la kila mtu); lakini jiulize nini wasfu wa Kadinali huyu Evarist Mushi:

- Anza kutafuta background check yake — ukiachilia shughuli zake za ‘kidini’ na ‘ucha mungu, alikuwa anafanya nini kengine hapa Zanzibar. Huko alikotoka, Moshi/Arusha alikuwa nani, na alikuwa anaishi vipi.

Jiulize, juzi tu, Jumatano iliyopita alikuwa wapi, na kweli aliongoza misa pale Beit El Ras (Ash Wednesday); lakini hasa hasa alikuwa nani (who is Evarist Mushi): Hao intel wako, waanze kuchunguza lineS (leadS) hizi. Contacts zake za mwisho, kupitia simu za mkononi, mlahaka wake na watu n.k. Mimi sikufundishini kazi, lakini ukachero wenu naona una mushkeli, maana unalenga upande mmoja tu, kuwasaka masheikh, waislamu.


Je, haiwi kuwa ni hitilafu yake na waumini/wafuasi wenzake au jamaa zake.

- Wewe Nchimbi umeshaamua kuwa hilo ni tukio la ugaidi. Je, kama upelelezi utagundua, at last, kuwa ni ‘financial dealings’ au extra marital affairs kama ‘sheikh fulani’, utasemaje? Although report yenu haitosema hivyo. Inasema kama ulivyokwisha sema, maana you pre-emptied the investigation /outcome which is wrong. Basi nyote mmeilemea Zanzibar namna hiyo: Kikwete, said Mwema, wewe Nchimbi.


- Angalia Dr.Nchimbi — Anna Makinda, spika wa Bunge, tumesoma kupitia magazetini, kuwa ametumiwa SMS za simu 600, zote za vitisho, matusi, kashfa n.k — mpaka sasa hatujaona polisi wala wewe kusema hata neno, na hii ni hatari zaidi na upelelezi wake hautaki Phd kama uliyonayo wewe. Maana TCRA — mamlaka ya mawasiliano TZ inayo data base yote ya simu za watu wote TZ. Ndio tuseme hawajulikani au hamtaki tu. Jamani hii biasness yenu, kutokutenda haki, ndio imetufikisha hapa. Akiuliwa muislamu mnakaa kimyaaaa; akiparuzwa hata mfagiaji wa kanisa, serikali yote inapiga kelele na kutetea ‘haki itatendeka’.

- Tumeona mauwaji ya Geita ya waislamu – serikali yako Bwana Nchimbi imeruhusu wakiristo kuchinja wanyama (mbuzi, ngombe, kondoo, kuku n.k) kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na kuuzwa public, kitendo ambacho hakuna nchi hata moja iliyoruhusu hivyo. Kenya mpaka leo wanaochinja wanyama for general public ni Waislamu, Uganda kadhalika, Ethiopia kadhalika, n.k kwengineko.

- Wakati wa ukoloni, Mngereza, Ujerumani – Tanganyika, pia waliokuwa wanaruhusiwa kuchinja wanyama kwa ajili ya kula – ni Waislamu. Nyie jamaa zangu wakoloni weusi mnakataa ukweli huo, na mmesababisha mauwaji kwa waislmu bila sababu kwa kitu ovyo kabisa. Kikwete anacheka, Mwinyi anacheka, na Said Mwema anakenua — hamna uongozi, hamna maamuzi — its’ nonsense. Hebu mjiulize kama kweli mna akili — imeanza lini, imeanza vipi, nini motive?
Tatizo jengine kubwa ni kuwa wakiristo wahamiaji wanalazimisha mambo kwa nguvu hapa Zanzibar. Tujue kuwa kama ukiristo, umeanza hapa Zanzibar kwanza kabla ya Tanganyika.


Na hapa wapo wakiristo tena prominent — marehemu Daurado, Augistino Ramadhan, na wengine — na hawa mpaka sasa wanaishi na watu vizuri, hawabagui mtu, wala wao hawabaguliwi.

Ukimuona Augostino Ramadhan msikitini hadi hii leo huwezi kujua kama ni muislam au mkiristo; huvaa kanzu, kofia na koti na makbadhi — Adam Mwakanjuki kadhalika, iweje leo iwe hivi??

Mjue kuwa Zanzibar ina aina nyingi za dini na watu hawajawahi kugombana – kuna: Shia Ithnasheer, Hindu, Catholic, Anglican, Muslim Sunni, Ibadhi, zaroastrim (wale waliokuwa akiabudu moto, na mahekalu yao yapo pale Maisara, alipojenga Sh.Ali Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu), wapo pia siku hizi wana-itikad mambo ya wahabbi/wahabbism, wapo hawa ahli tariqa n.k.nk.nk.

- Nchimbi, pamoja na doctorate yako nina hakika haya huyajui na sasa ndio ujue kuwa Zanzibar inahitaji respect/mutual respect yake — sio uje utumavie tu na kututukana kama paka wa mwituni. Sisi tuna nchi yetu, heshima yetu, adabu zetu, mila na desturi, busara zetu. Hiyo nafasi uliyonayo — mambo ya ndani tokea imeundwa, waasisi wake ni Wazanzibari, angalia chart ya tokea 1964 ilipoundwa, wazanzibari wamekaa hapo, na watanganyika wangapi wamekaa hapo. Ni Juzi juzi tu imeanza kubadilishwa na Kikwete. Unajua kwa nini?

Hiyo ni wizara inayotakiwa kushughulikia mambo zaidi ya dini na uhusiano wa watu na imani zao na hasa islamic affairs. Kikwete ndiye aliyepangua formula hii na akamuweka yule hayawani mmoja anaitwa Shamsi Vuai Nahodha, another mess iliyofanyika hapo. Mpaka wakati wa Mkapa, alikuwa Ali Ameir Mohammed. JK ndiye aliyeanza na yule check bob mwenzake Lawrence Masha, then Shamsi na sasa Nchimbi.

Hii wizara ilikuwa haiongozwi na mkiristo labda kidogo wakati wa Oscar Kambona, tena briefly tu. Nyerere alikuwa amemuweka Natepe etc etc. Ali Hassan Mwinyi pia amewahi kuwa Waziri hapo; ilikuwa ni mawaziri waislamu.

Tukisema nchi haina uongozi wala viongozi tunakusudia kusema kama haya, zile national ethos zinapuuzwa, na mtu kama Kikwete na timu yake.

Sasa, Bwana Nchimbi tumekusikia na tumeona unavyotuchimba mpaka uing'oe mizizi ya Zanzibar yote, na kanisa lichukue nafasi yake.

- Turudi nyuma kidogo, again, alipomwagiwa acid Soraga, hakuna kachero wala team ya inteligensia iliyokuja Zanzibar mpaka alipopigwa risasi padri, Mpendae — kwa kujitoa kimaso maso, na baada ya wananchi kulilia haki, ndio mkajifanya eti pia mnapeleleza kesi ya Soraga, na mnajua nini na nani alifanya, na kwa nini alifanya: sasa, kwa nini hamtaki kueleza umma hizo findings zenu. Wekeni ukweli wazi, ili kuondoa shaka – kanisa limeficha mambo mengi machafu, hatujui motive hasa za visasi hivi vinavyoendelea. Nyie dhana yenu ni Uamsho, pengine ni kitu chengine.

Siku za nyuma kidogo, kuna kada mmoja wa CCM alimwagiwa acid 2004/5 — CCM walitoa kauli wakasema ni CUF; lakini ukwlei ulipofichuka kuwa yule kada alikuwa na affairs na mke wa mtu – hapo kila mmoja alikaa kimya? (???). Nchimbi kama huijui Zanzibar wapo makachero waliobobea sana – sitaki kuwataja, lakini hata nchi za magharibi wanawategemea, wameshastaafu. Mmoja alikuwa waziri…mtafute.


Chanzo: Mzalendo.net

Maelezo marefu ya kuhalalisha tatizo. Inasikitisha sanaa!!! Hata kama kuna motives hazihalalishi mauaji hayo after all they are only assumption. Mwenye kufikiria mbali zaidi anaweza kujiuliza hivi haiwezekani kuna waliokuwa wakijua mienendo ya huyu padre na kupanga maauaji ili yaonekane ni ulipizaji kisasi while lengo ni jingine kabisa. Unayotumia hapa ni criminal psychology, na ningekuwa mimi ningeanza na wewe kujua hizo theory ambazo unatoa za kumislead investigation una motives gani!?
Huonyeshi hata chembe ya kulaani lililotokea unajaribu kuhalaisha mauaji kwa kuunganisha na uhalifu mwingine. Hii sio upotoshaji wa makusudi kulifanya suala la kihalifu kuwa la kisiasa. A LOT OF CONSPIRACY THEORY.
HAPA PANA TATIZO LAZIMA TUKUBALI HILO NDIO TUENDELEE.
Kuna viongozi wa kidini wanaamini wanachokiamini na kukisimamia ndicho wengine wanachokitaka na kukisimamia. I beleive in natural justace na usawa, haki, uhuru,uhalali, kutenda yale nisiyopenda kutendewa na au mtu asiyopenda kutendewa. Mimi kwangu dini ni ya pili au hata ya tatu. Je hayo aliyoyafanya huyo unayemuhukumu huwa na wewe hujawahi kuyafanya!? Je na wewe walikuhukumu?! Au binti yako au mwanao akifanya hayo utampiga risasi?!

Kudai uhuru wa Zanzibar hakuhusiana kivyovyote na kanisa kama mnavyopenda kutuaminisha.
 
Hili lililotokea zanzibar ni doa kubwa sana kwa nchi yetu. Tunapaswakulijadili kwa uzito bila kejeri, jazba ba ushabiki. Ni suala linaloguza umoja, usalama na mshikamano wetu.

Tusilijadili moja kwa moja kama ni tatizo kati ya waislamu na wakristo bali watanzania wastaarabu wanaoitakia nchi yetu mema na wahalifu wasioitakia mema nchi yetu. Sote tuwe kitu kimoja kuwasaka wahusika na walio nyuma yao bila kujali itikadi yao, dini yao na kabila lao. Pia tusiruhusu mambo yoyote yatakayotupelekea tuonane maadui sisi kwa sisi.
 
Kuna watu humu janvini wanajinasibisha kuwa ni wasomi lakini hamna kitu kabisa.
Hivi,kuna watanzania wangapi wameuwawa kinyama zaidi ya huyo padre na matamko kama hayo ya ugaidi hatujayasikia?

Padre ana thamani sana kuliko watanzania wanaoripotiwa kuuwawa takribani mikowa mingi ya Tanzania? Yale mauwaji ya mkulima aliyeporwa pesa yake na askari ambao wapo chini ya wizara ya mchimbi kule Morogoro mbona hatukusikia kuwa ni ugaidi?

Ila tu ikitokea kuuwawa kwa padre ni ugaidi!! Kulikoni?
Acheni kutoa maamuzi ya kushinikizwa yenye msukumo wa kidini. Tendeni haki watanzania wote ni sawa. Hizi tofauti ya elimu na kipato isiwe sababu ya kuweka matabaka. Namna hii inaweza kuleta machafuko zaidi ya haya.
 
Kuna msemo usemao, 'ukirusha jiwe katikati ya mbwa wengi, atakayebweka ujue ndiye jiwe limempata'. Maalim Seif jiwe limemgonga ndiyo maana amekuwa wa kwanza kupiga kelele.

Seif Sharif Hamad mwenyewe ni gaidi na ndio maana limemuuma. Ni kijimakamu cha rais kwa sababu chama chake cha ugaidi kinakubalika na magaidi wengi sana so sishangai. Ila, hata Nchimbi naye ana elements za kigaidi.....ukiuliza ntakujuza zaidi
 
katika nchi dhaifu na yenye vyombo vya usalama dhaifu bila shaka hili litaendelea mpaka siku wakristo nao waamue kupambana maana hii inalizidi jeshi la polisi na wanausalama wote! Seif anajua si magaidi bali ni mpango wa kudai nchi iliyogeuzwa kuwa mikoa mitano ya Tanzania......Ukiwa Zanzibar hili lipo wazi hawa wanajuana lakini wanapata support kutoka kwa baadhi ya viongozi kama huyo Seif ambaye hakulaami mauaji ya Padri lakini yupo mbele kupinga kwamba huo si ugaidi!

Zanzibar sio shwari tena!
 
Back
Top Bottom