Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kimenajisi Tasnia ya Habari. Kamati yaundwa...

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819






Waziri Nape: Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Waziri Nape: Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi

Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya

Kusaga: Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!

Reginald Mengi: Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!

Nape Nnauye(Waziri wa Habari): Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

Nape: Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

Nape Nnauye: Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24

====

Habari zaidi....

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atajiuzulu nafasi yake kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru.
Nape%20%281%29.jpg

Waziri Nape Nnauye

Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clauds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.

Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.

"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo hili". Alisema Nape

Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.

Mengi.jpg

Dkt. Reginald Mengi

Pamoja na hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Dkt. Reginald Mengi amesema hawezi kutoa lawama kwa mtu yoyote mpaka pale ukweli utakapofahamika japokuwa ameonekana kukerekwa.

"Kwetu sisi hili ni jambo ni la hatari sana, linatuogopesha na linatishia maisha ya waandishi wa habari". Alisema Dkt. Mengi

Kwa upande mwingine Mengi amewasihi waandishi wa habari kutokuwa waoga kwa jambo lolote wanalopambana nalo ila wanachopaswa ni kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.

Hapa chini ni kamati iliyoundwa

81bec248-c091-4e4b-bb60-f258b0167d1a.jpg
 
Ha ha ha! Paka anaenda kukamata panya; akikuta panya kakumbatiwa na simba sijui atafanyaje; sana sana atabana mkia kwenye miguu na kutimua mbio kunusuru maisha yake. Hebu tusubiri kuona mwelekeo wa hii movie; sijui series ya ngapi hii.

======== UPDATES ========

Naam! Kumekucha! Simba ametoa msimamo rasmi tena msimamo wa hatari dhidi ya paka na hayawani wengine wanaojaribu kuchezea himaya yake; nywele zote mabegani zimemsimama "mfalme" simba; amenyayuka pale! Ngurumo zinasikika pori lote. Kwa hakika ni hali ya hatari; taharuki kila upande. Paka anazo options mbili tu kwa sasa; kuendelea kupambana araruliwe vibaya au kuufyata abaki salama. Sijui atachagua lipi; kazi kwake.

Paka mwenye manati mkononi kweli atapambana na simba mwenye nguvu, kila aina ya silaha na ngao akitanguliwa na majasiri waliombembea silaha na ngao kwenda kupiganisha vita? Kwa hakika mshindi yu dhahiri labda utokee muujiza.
 
Ha ha ha! Paka anaenda kukamata panya; akikuta panya kakumbatiwa na simba sijui atafanyaje; sana sana atabana mkia kwenye miguu na kutimua mbio kunusuru maisha yake. Hebu tusubiri kuona mwelekeo wa hii movie; sijui series ya ngapi hii.
Movie ipo mwisho mwisho lakini Wadhamini wa movie GSM ndiyo wanapanga njia zote za Uzinduzi hata Mlezi wao baba jesca kaamua kuuchuna kiimya hataki kusikia kitu.
 
Kufoji vyeti ni miaka 7 jela, trespassing, wizi(flash aliyosema Ruge),defamation (kwa Gwajima na huyo mama), child abuse (kwa yule mtoto kupigwa picha n. K), kutumia vyombo vya dola kwa ishu binafsi.. Hayo ni miaka mingapi jela?
 
Ha ha ha! Paka anaenda kukamata panya; akikuta panya kakumbatiwa na simba sijui atafanyaje; sana sana atabana mkia kwenye miguu na kutimua mbio kunusuru maisha yake. Hebu tusubiri kuona mwelekeo wa hii movie; sijui series ya ngapi hii.
Hahahaha harare
 
Back
Top Bottom