VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,870
Ingekuwa kwenye nchi ya kidemokrasia na inayoiishi demokrasia, Waziri Nape Nnauye angeshapoteza uwaziri na ubunge wake muda huu. Angepoteza kwa shinikizo la wananchi au kuondolewa na Rais aliyemteuwa. Lakini hapa kwetu, Nape bado anadunda na anakejeli kwa kusema eti amechakachuliwa video yake ya kule Bukoba.
Nape Nnauye amewahi kushika nafasi nyeti chamani-Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa. Anajua kila jambo analolisema. Viongozi wa CCM hufundwa na kupikwa juu ya nini cha kusema; wapi pa kusema; lini useme; kwa jinsi gani useme na kwanini useme. Nape amesema akijua fika kuwa huo ndiyo ukweli wenyewe.
Nape anajua kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu mwakani. Ameanza, kwa kulewa madaraka na kujisahau kulikopitiliza, kuahidi kumpa ubunge Byabato wa Bukoba Mjini. Anaamini kuwa yeye anaweza kusema na kutenda lolote popote. Madaraka ya kulevya!
Waziri wa mgombea mtarajiwa wa Urais wa CCM-Mama Samia kusema vile kuna maana kubwa. Waziri wa tasnia ya habari akiisambaza habari kama ile ni jambo kubwa na la kuogofya. Kwamba, CCM hushinda kwakuwa ndiyo wanaohesabu kura na kutangaza matokeo. Hawashindi kwa kukubalika kwao na sera zao. Mambo mazito!
Mama Samia anafanya juhudi kubwa za kujipambanua kiutendaji na kikauli ili achaguliwe mwaka 2025 kama Rais wa Tanzania kupitia CCM. Nape anataka watanzania waamini kuwa juhudi zote za Mama Samia ni maigizo kwakuwa ana uhakika wa kutangazwa mshindi? Huu si uchochezi utoao machozi?
Nape amedhihirisha kwa umma wa watanzania mbinu chafu zinazoanzia kwenye chumba cha kuhesabu kura na wakati wa kutangazwa kwa matokeo. Wakati yeye akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, mwaka 2012, mimi nilikuwa 'active' chamani na serikalini. Kwa uzalendo wangu, niliripoti jambo lifananalo na lake likitokea chamani mwaka huo: KIZOTA-Chumbani kuhesabu kura
Nape ameianika CCM yetu. Amekuwa mchochezi. Awajibishwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nyegezi, Mwanza)
Pia soma