Waziri Nagu ashangazwa na umasikini wa Watanzania

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akihutubia mkutano wa Makatibu Muhtasi nchini (TAPSEA), leo jijini Mwanza.



Dk. Mary Nagu

Waziri Nagu akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist Welle Ndikilo (kulia), baada ya kufungua mkutano wa TAPSEA leo jijini Mwanza. (Picha zote na Sitta Tumma).

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu Ameeleza kushangazwa kwake na hali mbaya ya umasikini unaowakumba Watanzania, huku taifa lao likiwa imejaa rasilimali nyingi zisizo na kifani. Amesema, Tanzania ni nchi tajiri sana wa rasilimali, lakini wananchi wake bado wanakabiliwa na tatizo la umasikini, jambo ambalo alisema upo umuhimu zaidi wa uwezeshwaji wa wananchi, ili kuondoa tatizo hilo la umasikini katika ngazi ya kaya, mkoa hadi taifa.

Waziri Nagu ameyasema hayo leo Jijini Mwanza, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili la Chama cha Makatibu Muhtasi wa umma na sekta binafsi Tanzania (TAPSEA), uliofanyika Malaika Hoteli jijini hapa. "Nchi yetu hii imejawa na utajiri mkubwa sana, lakini bado umasikini nao umekithiri kwa Watanzania. Hivyo uwezeshwaji wa wananchi lazima uwepo", alisema Waziri Nagu. Hata hivyo, alikwenda mbali zaidi na kuwaonya Watanzania kwamba, wasibweteke na hali waliyo nayo sasa, bali wachangamkie fursa zilizopo nchini za uwekezaji, ili wasije wakabaki watazamaji tu katika sekta hiyo muhimu na mkombozi mkubwa wa umasikini.

Katika hatua nyingine, aliwataka Makatibu hao Muhtasi nchini kuhakikisha wanafanyakazi zao kwa ufanisi na umakini wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kujenga ushirikiano mzuri kati ya mwajiri, jamii na watumishi wengine. "Kumbukeni ya kwamba, ninyi makatibu muhtasi ni chombo muhimu sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo. Bila ninyi Waziri, Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine hawawezi kufanyakazi zao vizuri. Jengeeni ushirikiano thabiti na imara", alisema.

Hata hivyo, Waziri Nagu alijikuta akilazimika kuzungumzia vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa yanayolinyemelea taifa kwa sasa, ambapo alisema: "Kwa sasa vuguvugu la mabadiliko limezidi kukolea hapa nchini. Mabadiliko haya yasichochee vurugu bali yawe ya amani".
Aidha, Dk. Nagu alieleza kukerwa na namna makatibu muhtasi wanavyofanyishwa kazi kwa kufananishwa na jiko la kupikia jinsi lisivyothaminiwa, lakini kila mtu anahitaji ale na kushiba kupitia jiko hilo hilo.

Alisema, dunia ya leo bado inatawaliwa na mfumo dume unaokandamiza na kuminya haki za wanawake, hivyo kwa vile kazi ya ukatibu muhtasi hapa nchini inafanywa na wanawake wengi zaidi, wapambane na kutokomeza mfumo huo dume, na watetee haki zao za kujiendeleza kielimu zaidi ili siku moja wapate nafasi ya juu kama alivyo yeye (Waziri Nagu). "Msije mkadhani najigamba, majigambo siyo huruka yangu. Mimi nimewahi kufanyakazi nikiwa ofisa wa chini sana kiwandani, lakini baadaye nikawa General Manager (Meneja mkuu), wa kiwanda nikiwa mwanamke miaka ya 86.

"Kwa maana hiyo, nawaombeni sana mjiendeleze kielimu mpate hadi masters ya ukatibu muhtasi na baadaye mje muwe mabosi na mhudumiwe kama mnavyowahudumia mabosi wenu ofisini", alisema Waziri huyo wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji nchini.
 
Hao wote baba yao mmoja na JK. Hakuna kiongozi wa serikali ya ccm anayejua chanzo cha umasikini wa wananchi, maana wao matumbo yamejaza vya dhulmati.
 
chama kilekile watu walewale sera zilezile hakuna jipia hapo aache unafiki inamana hayo ndio ameyajua leo?hatuoni anatukebehi watanzania?ccm hawana msaada nasie hatakidogo
 
Amekulia kwenye mteremko anaishi kwenye mteremko,wanapewa ubunge wa bure then uwaziri wenyewe wanaita viti maalum, huo umaskini wataujuaje, vigezo vya kupata viti maalum havijulikani maana miaka nenda rudi ni walewale,sijui hua wanagawa kwanza k****a kwa wanaume wa kamati kuu au ni wap****zi wao? Inakera sana kusikia wanatoa kauli kama hizi shxxxxz.
 
Amekulia kwenye mteremko anaishi kwenye mteremko,wanapewa ubunge wa bure then uwaziri wenyewe wanaita viti maalum, huo umaskini wataujuaje, vigezo vya kupata viti maalum havijulikani maana miaka nenda rudi ni walewale,sijui hua wanagawa kwanza k****a kwa wanaume wa kamati kuu au ni wap****zi wao? Inakera sana kusikia wanatoa kauli kama hizi shxxxxz.

Amepata ubunge wake in the name of Kiravo baada ya kuchakachua matokeo yaliyompa ushindi wa Rose Kamili huko Hanang'
 
Hata yeye mwenyewe hajielewi na haelewi anachosema.
Kazi kubwa kabisa angetakiwa afanye huyu ni kufua nguo na kudeki tu pale nyumbani
 
Huyu mama alitakiwa awe wa mwisho kuushangaa umasikini wa Watanganyika...jimbo lake Hanang' wale wambulu wenzake ni masikini wa kutupa kwa nini hawashangai hao?
 
Back
Top Bottom