Waziri Mwigulu: Tanzania inakopa kwa Sababu ina Uwezo wa kulipa

Kweli kabisa, na kudaiwa sio issue, mbona mtoto wa Mbowe juzi kidogo nyumba yake iuzwe kwa kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wa gazeti la Tanzania Daima, halafu na yeye huwa anaandamana akitaka serikali ipandishe mishahara, wakati yeye na baba yake hata kulipa hawawezi
 
Huyu si alisema madeni hayatuhusu watz na akaongeza hakuna mtz hata mmoja atakayegongewa mlangoni mwake kulipa hilo deni.
 
Duuh.

Kwahiyo ni lazima tukope hata kama hatuhitaji kukopa??

Kwa maelezo haya nahitimisha kwamba mabeberu huwa wanawalazimisha viongozi wetu kukopa.
Siku zote nakumbuka zile stages of development s,kwamba ukiwa na maendeleo makubwa kuliko uwezo wako wa kumenage/kusimamia ni KAZI bure.chukua mfano mdogo makampuni ya mabus ,Makampuni mengi tuliokuwa tunayafahamu yalifilisika baada ya kukopa kupitiliza na hatimaye yakashindwa kusimamia Makampuni hayo kutokana na ukubwa wa Kampuni,nani asiyekumbuka"Scandaviani buses,Fresh ya Shamba ,Sleeping coach na mengineyo mengi,Ogopa sana "over development"tutake note,wale wanaotukopesha wanafanya biashara ,wanapenda biashara zao na sio kwamba wanapenda maendeleo yetu.wao Wana uhakika wa kuvuna faida zao asilimia mia moja.na hatta tukishindwa kulipa watakamata Mali za Wajukuu wetu .Nasisitiza tukope kwa kiasi na tuwekeze kwenye miradi tunayoimudu."quick win'..
 
Waziri wa fedha Mwigullu Nchemba amesema Watanzania wasiogope Nchi inakopa kwa Sababu ina Uwezo wa kulipa

Source: Mwananchi

Sabato njema
Tangu tupate uhuru, hatuja wahi kuwa na Waziri wa fedha kiazi kama huyu.
Marais walio pita walikuwa wana angalia mtu ambae ana toka kwenye watu walio zowea pesa.
Sasa Mama sijuibkatoka wapi na huyu omba omba.
 
Back
Top Bottom