Waziri Mulamula: Watanzania walioko Ukraine wajitahidi waingie Poland. Wananchi msiwe na wasiwasi Serikali inafuatilia!

Hii ndiyo sababu kubwa ya serikali kukataa kutoa pasipoti kwa kila mwananchi. Serikali inajua raia wake wakipata matatizo kwenye nchi za watu, haina uwezo wa kuwasaidia.
Wajibu wa Serikali na hizo balozi huko nje ni wa nini hasa kama wanashindwa kusaidia raia wakati wa shida.
 
Tusiwe na wasiwasi wakati tunaona mbwa anapakiwa kwenye treni kupelekwa Poland mswahili anashushwa.
Sisi tuandae ubwabwa na maturubai tu
 
Poland kwa sasa haiwezekani.wameondoka kuelekea Romania na Hungary.Tuwaombee ALLAH awafanyie wepesi na tutoe sadaka kwa nia ya vijana wetu wasidhurike.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Na hao wa ukraine hapo zenji mkawabwage kwa balozi wao (kama wanao) maana si watu wale
 
Wana uswahiba gani na nyinyi, mkishaona tu nchi yenye nguvu isiyohoji wizi wenu wa kura mnajifanya rafiki zenu.
Uswahiba huu....
IDU_David_McAllister-600x600(0).jpg
 
Waziri anasema tusiwe na wasiwasi. Waziri hazifahamu fat bombs za Warusi walizozitumia Syria.
 
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
nilifikiri angetuelezea hatua zilizo chukuliwa. aelezee wamefanya nn kuhakksha wanapita mipakani salama, mabalozi wetu wanasaidia vp ...nk. kufatilia anakozngmzia maana yake nn? tumeona wenzetu Ghana wakikumbatiana na watoto wao baada ya kuwasili makwao, au mambo yataji solve yenyewe!?
 
Kama mnasoma huu uzi na mpo Ukraine ,nawataka sana sana mbanane huko huko ,msije mkaingia mkenge na kutaka kurudi huku,maana hali ya maisha ni tete joto ,kama mtanisikiliza bananeni huko chini ya reli. Majuto ni mjukuu kama zako zipo hutakufa kwa kupigwa misaili maana hata huku mnakoambiwa mrudi ni kama kumepigwa nyuklia .
 
Unapotosha uma.Ulichoandika sicho alichosema waziri🐒🐒🐒

Mods please pigeni huyu mpotoshaji ban kwa manufaa mapana ya JF na kwa manufaa mapana ya uma kwa ujumla.
 
Waingie Poland kwa usafiri gani.

Hivi ukimwambia mtu aliyeko mtwara aingie Kenya bila msaada wa kumuwezesha kufika Namanga again ataingia kweli Kenya?

Watawezaje kufika huko na watakuwa wanakula nini?
Ongezea na baridi lililopo huko !!
 
Back
Top Bottom