Waziri Mulamula: Watanzania walioko Ukraine wajitahidi waingie Poland. Wananchi msiwe na wasiwasi Serikali inafuatilia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,532
141,335
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Et wana nchi wasiwe na wasiwasi.

CCM huwa hamjiongezi , Watu wameanza kuwatoa RAIA wao wiki kadhaa kabla ya Vita hiyo.

Nyie mnastuka saizi tena baada ya Raia kuhoji .

Sasa mipakani tu huko Ukraine, Waafrika wanabaguliwa ,hamna kuondoka , sisi wazungu kwanza ndo tunasepa .
Ndio wapambane sasa waingie Poland.

Wataikuta ATCL inawasubiri!
 
Mh.Mulamula yuko sahihi....

Imeshakuwa vita sasa serikali ya JMT ilaumiwe nini ?!!!

Je Kuna nchi ya Afrika ya Mashariki iliyotoa ndege kuwaamisha raia wake?!!!

Zosin na Ustyluh ni miongoni mwa mpaka baina ya Ukraine na Poland....kwa kuingia Poland njia hii ni bora zaidi....waondoke Ukraine!!!

Kwanza Urusi imeshawaambia wakazi wa Kyiv kuondoka...tena wamewaonyesha njia ya SALAMA NA AMANI.....

VITA HAINA MACHO

#Siempre JMT🙏
 
Kwan kuna shida gan kuchukua mwewe mmoja chap hapo bandan hasa yule drimu laina! Maana napata shida kidogo na hlo zoez la uratibu!

Wanaccm mnaweza kulifanya mradi wa kukusanya hela za uchaguzi
 
Mh.Mulamula yuko sahihi....

Imeshakuwa vita sasa serikali ya JMT ilaumiwe nini...🙏
Kwanini ilishindwa kuwatoa hali ilipoanza kuwa tete wakati wengine walipoanza kuondoka!

Tukumbuke vita haikuanza ghafla kwani maandalizi yalichukua zaidi ya wiki.
 
Kwanini ilishindwa kuwatoa hali ilipoanza kuwa tete wakati wengine walipoanza kuondoka! Tukumbuke vita haikuanza ghafla kwani maandalizi yalichukua zaidi ya wiki.
Hivi Putin alipopeleka wanajeshi wake 150,000 mipakani na kabla ya kuviondoa na kurudi kivita je kuna nchi gani ya Afrika iliondoa raia wake?
 
I mean wameshindwa kurudi kwao maaana ndege haziendi Ukraine,vibali vya kukaa Zenj vimepitwa na muda na baadhi wameishiwa salio.
Ipo ndege ya moja kwa moja Zanzibar to Poland.

Balozi wao aliyeko Kenya ndiye anaratibu safari yao!
 
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika...
Waingie Poland kwa usafiri gani.

Hivi ukimwambia mtu aliyeko mtwara aingie Kenya bila msaada wa kumuwezesha kufika Namanga again ataingia kweli Kenya?

Watawezaje kufika huko na watakuwa wanakula nini?
 
Back
Top Bottom