Waziri Muhongo anasa bil. 400/-

Change hiyo heading kuwa watz watapata bil.400,hela za raslimali ni za kuboresha ustawi wa jamii na miundo mbinu(shule,afya,barabara,nishati,mawasiliano,chakula bora,etc.). Huu uwe mwanzo wa kuigeuza nchi yetu kuwa first world.
 
Mwanzo mzuri...tunahitaji more governance katika hii sector kama tunataka kutoka....

Tukichemsha kwenye gesi basi tutakuwa masikini daima....
 
Nchi yetu ina sifa zote muhimu za kuifanya iendelee...

Tuna strong state and stable democracy (si kama Nigeria, DRC, Msumbiji, Uganda na nchi nyingi za Sub Saharan Afrika) kwa maana kuwa nchi yote inatawaliwa na serikali....hii pekee ni nguzo kubwa sana kwa maendeleo kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama yetu kwa kuwa serikali ikiwa makini itatumia pato la rasilimali kuendeleza sector nyingine tofauti na hao wenzetu ambao kila mtu ana tax natural resources (DRC, Nigerian militants))


Ndio maana inabidi tuwe wakali sana kwenye gesi hakuna kuleta u namjua fulani, basi nipe tender...ni ushindani baaasi.

Nilikuwa nasoma kitabu fulani 'Why Nations Fail" kumbe Egypt walikuwa na mawaziri wafanya biashara...yani mfanya biashara mkubwa kwenye sector ya mawasiliano ndio kapewa wizara husika, utalii same, natural resources same.... Kilichofuata ni kuwa walitengeneza oligopoly ya nguvu ya economic and political elites. Ambao walihakikisha wanazuia makampuni ya kigeni kuwekeza Egypt ili kuondoa ushindani; lakini hao hao wazawa hawakuwasaidia chochote walala hoi wa Egypt bali walijenga matabaka ya wenye nacho (washikaji wa karibu wa Mubarak) na wasio nacho...kulikuwa na matajiri wakubwa 30 nchi nzima wote well connected na rais au watoto wa rais....kilichofuta ndio hiyo arab spring...

Hiki kitabu ni noma wametaja majina ya hao vigogo 30 mpaka bei walizokuwa wanauziana state owned corporations pale walipoamua ku liberalize economy (SAP). Hayo makampuni yote yalikuwa ya serikali before hayajauzwa kwa bei ya kugawa kwa washikaji wa rais wa Egypt
 
Waliouza viwanja kariakoo kwa bei waliyodhani wameula,leo hii wakiangalia bei za viwanja kariakoo wanaishia kupata maumivu ya vichwa,
Ningefurahi kusikia serikali ndo imeuza hisa au vitalu hivyo kwa fedha hizo badala ya kuwagawia wajanja wakauza afu
serikali ikapewa kodi tukashangilia kama mazuzu.
 
Soma vizuri,Mhe. Zitto Zuberi Kabwe ndie aliyeanzisha hii kitu ikawa sheria,sio waziri. All kudos to Mr ZZK
Hizi siasa za kugombea fito Watanzania sijui sitatufikisha wapi! Hapo kila mmoja ame-play role yake vizuri! Zitto, kama mbunge ametekeleza wajibu wake na ameleta mswada wenye maslahi kwa taifa! Lakini Muhongo na wenzake nao wame-play part yao vizuri...kusimamia uuzaji na kuhakikisha taifa linapata stahiki yake. Hao wengine wasiolipa kodi si kwamba hakuna sheria; zipo na hawalipi. KImsingi hapa hoja sio hiyo mnayoshindana nayo nyie; hoja ni kwamba je, hizo 20% ambazo Ophir wameuza kwa USD 1.3 Billion, kweli hiyo ndiyo thamani waliyouza? Let me keep it this way ili mpate kunielewa. Assume unanunua gari Japan kwa USD 250 million. Lakini unafahamu wazi kwamba, hiyo gari ya USD 250 million, TRA watachukua nyingi sana za kwao. Ili kukwepa panga zito la TRA, unaamua ku-collude na Seller na kisha anaandika Stakabadhi mbili; moja anaandika USD 250 million(hii unabaki nayo) na nyingine anaandika USD 100million (ndiyo unayoenda kuonesha TRA). Hii ilikuwa inafanyika sana; tena sana hadi TRA walipoamua kuanza kufanya evaluation wenyewe! Sasa basi, kodi ambayo ilibidi itokane na USD 250million, will eventually come from USD 100 million! Meaning that, at the end of story, TRA watachukua chini ya 50% ya kodi halisi!!

Hivyo basi, kama hakuna ushenzi wowote(Watanzania kutokana na kutopea uhalifu, mnaita "ujanja") na kwamba ni kweli kabisa Ophir wameuza hisa husika kwa USD 1.3 billion; then congrats to all waliohakikisha national interest zinazingatia hata kama ni wajibu wao kufanya hivyo...coz' they're being paid to do so.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hujafahamu vizuri jinsi haya mambo yanavyoenda. Tanzania haijapoteza chochote hapo, sana sana ime-gain.
 

hivi wewe Tanzania tunakimbia au tunatambaaa?tunatambaa chini ya swaga na ulaghai wa ccm,ufisadi na ubinafsi wa mawaziri wa chama chakavu ndo wanasainishana mikataba mibovu huku wakiramba ten /cnt zao nyie mnasema mnakimbia,kama sisi tunakimbia tueleze tunakimbiaje? Labda tunakimbia kwa riverse!
 
sisi vitalu tuliwapa kwa how much?
Ipo hivi. Assume mimi nina kiwanja 100mx100m=10,000 square meters City Centre. Unfortunately, sina uwezo wa kuendeleza au kuweka investment ya maana kutokana na eneo husika. Kisha, wewe unakuja na mwenzako (BG+Ophir) na kusema mna uwezo wa kuendeleza kiwanja husika kwa kujenga hiki na kile. Hapo nawaambia kwamba, mkitaka kiwanja changu, basi mradi ukikamilika mimi inabidi nipate 65% na nyinyi mchukue 35% ya mapato lakini. Lakini pamoja na hayo, nawaambia kwamba hicho kiwanja unachokiona leo; nimefanya hiki na kile; nimelipa watu kung'oa visiki; kulikuwa na dampo kubwa sana; nikalipa watu kulifukia kwahiyo ni lazima mnilipe kwanza hizo gharama! Hii maana yake ni nini? Kiwanja sitawauzia lakini gharama zilizofanikisha kiwanja kuwa hapo kilipo ni lazima mlipie.

Kumbuka kwamba, wewe umekuja na mwenzako ambao kwa ujumla wenu mtakuwa mnamiliki 35%...sasa assume katika hiyo 35%, wewe yako hapo ni only 25% ya hiyo 35%! Lakini ili muanze ujenzi, ni kwamba wewe na mwenzako mnabidi mchangie gharama za huo mradi. Sasa, inawezekana ukaona mfuko wako umepwaya kwahiyo wewe kama wewe unaamua kuuza sehemu ya umiliki wako wa ile 25% ya 35%(kuu ya wawili). Mzee mzima nakuibukia tena; nasema kwavile umeuza portion ya umiliki wako, nataka kodi yangu hapo hapo! Kwahiyo unanipa changu kwa roho safi, kisha mnaendelea na mambo yenu huku mkikumbuka kwamba 65% yangu ipo pale pale! Kwahiyo ikiwa mkataba ni kugawana vyumba kisha mkajenga jengo la vyumba 100, nabeba vyumba vyangu 65, nawaachia 35 vyenu.

Trust me, kama isingekuwa donda ndugu la ufisadi na wizi, deal la gesi lingeifikisha TZ level ya juu sana...wadau hawataki kabisa kuniunga mkono katika Approved Dictatorship Governance! Hii ndiyo njia pekee itakayopunguza ufisadi kwa kiasi kikubwa!
 
Ulifuatilia ITV jana kuhusu tathmini ya kisiasa na kiuchumi ya mwaka 2013. Hizo ni pea nut ulilinganisha na deposit za gas. Ni sawa na mikataba ya ma-chief wetu wa zamani waliodanganywa na wakoloni. Professor Mhongo hana tofauti na hao ma-chief ambao hawakujua kusoma na kuandika
 
Watu wenye uwezo finyu wa kuelewa wanaruka huku na kule kushangilia eti tumepata sh bilioni 400 out of $1.3 billion * 1,600= Shilingi 2,080,000,000,000 kwa maana nyingine rasilimali yetu imeifaidisha kampuni ya nje na kuweza kujizolea shilingi 1,680,000,000,000 (Trillioni 1.68) kweli wajinga ndio waliwao. Ushauri wangu capital gains iongezwe na kufikia 50% ili tufaidike zaidi badala 20%, ingekuwa capital gains ni 50% badala ya 20% basi nchi ingepata Shilingi Trilioni 1.04, shilingi bilioni 600 zaidi na ushee.

 
BAK usiangalie muuzaji kauza kiasi gani kwa kuwa ni wazi kuwa hatukumpa bure hivyo vitalu....

Unless unambie faida alopata baada ya kutoa ela ya ununuzi na any additional investments ndio u conclude kuwa tumepata kidogo...still there is nothing we can do kwani ndio haki yetu kisheria

Hata wewe hapo ukiuza gari si unatakiwa ulipe kodi...unataka kunambia serikali itakuwa imekutendea haki ikichukua zaidi ya say 50% ya ela ulopata?


Mimi naona hiki kipato ni cha kujisifia kwa kuwa ndio haki yetu kisheria...sasa ukitaka kulalamika muuzaji kapata ngapi; basi tururdi bungeni kurekebisha sheria less than that tutakuwa wanyang'anyi...



 
Yaliyofanyika hapa ni makosa makubwa sana ambayo yamelikosesha Taifa pesa nyingi sana. Tuambie Serikali imeuza kwa hivyo vitalu kwa bei gani? Mfano wa kuuza gari na kuuza rasilimali hauna mantiki hata kidogo. Kwanini capital gains iwe 20% badala ya 50%?

 

Biashara hii ni complicated kuliko unavyofikiria kwani mikataba hii ilisainiwa under kitu kinaitwa PSA.
Maelezo hayo hapo juu kama yangekuwa sahihi Tanzania ingepata pesa nyingi kuliko tulizoambiwa kwy article.
Tanzania itaendelea kuibiwa sana kama itaendelea kuwaficha wananchi(wenye mali) wake mikataba wanayosaini.

gas iliyouzwa kwa mujibu wa NYSE commodity market ina thamani ya $ 60 billions wao wameuza kwa dola bilioni 1.3 that is very questionable NASDAZ. Wameuza kwa almost 90% off ya thamani ya gas hiyo. Gas ni ya kwetu tunaambulia dola milioni 260 which is less than 1% ya thamani ya gas inayouzwa halafu unaita hii ni kufaidika come on ???

inabidi ufanye assumption nyingi sana ili kuamini kuwa nchi imepata faida lazima ukubali kuwa bei ya dola 1.3 bilioni ni sahihi na pili je serikali ilishirikishwa ktk mapatano ya bei hiyo?? ne je serikali haikuona haja ya wao wenyewe kutafuta mnunuzi mwingine atakayelipa pesa zaidi ya hizi hasa ukizingatia ndiye mwenye hisa kubwa?? je muhongo alishauri nini serikali ktk kukubali bei hii ?? je alifanya research kuakiki bei hii au alichukua 10% na hakuwa na haja ya kufanya uchunguzi wa bei wala nini kama wengine wanavyofanya?? cha msingi kama nilivyokuwambia thamani ya gas iliyouzwa ni dola bilioni 60 wewe unaambuliwa makusanyo ya capital gain tax ya dola milioni 260 . i am very skeptical na hili deal inawezekana muhongo amefaidika kuliko nchi yetu.
 
Inawezekana mimi sijui ila katika Trillion 2 ya mali yetu tunaambulia Bil 400?
Am I dumb or what? Nisaidieni kunielimisha hapa sijaelewa kabisa!

Hata hizo bill 400 zitayeyuka tu hii ni Tanzania bana.
 

kama naiona minjino ya watu inavochelekea. naomba tujue hizo hela zitawanufaisha vipi watanzania!
 
Si ndio nakuuliza waliuza kwa kiasi gani? Na kama kuna kosa basi twende kwenye kubadili sheria kwa kuwa Muhongo alichofanya ni kusimamia utekelezaji washeria...

Badala ya kulalamikia case moja moja tunatakiwa tuweke institutions za kuondoa hizi lawama...

Wewe una propose tuchaji kiasi gani na kwa reference ipi? Wengine wanachaji kiasi gani?


 
Unajua nimegundua kwamba watu wengi hawafahamu vizuri haya mambo jinsi yanavyoenda...kimsingi wala hakuna tulichopteza ingawaje watu wanadhani tumepoteza. Kwenye sharing Agreement, Tanzania inapata 65% ya mapato ya gesi....kwahiyo hata wauziane mmoja baada ya mwingine lakini sisi 65% yetu ipo pale pale; sana sana tutakuwa tunachukua kodi yetu kila wanapouziana.

Labda watu wanapojichanganya ni kwamba wanachukulia uuzaji huu unafanana kama ilivyopata kufanyika kwa Sheraton Hotel and the like ambao kimsingi investor anauza; kisha anasepa wakati uuzaji wa aina hii ya sasa ni wa investor kuuza kwa ajili ya ku-accumulate capital....ni kama walivyofanya Swala Energy ambao wame-opt kuuza hisa DSE, hawa Ophir wame-opt kuuza hisa kwa one big investor.
 

kwako NASDAZ,
Napenda sana unavyojaribu kuwaelimisha wabongo kuhusu hii biashara ya gas lakini nigependa kukufanulia yafuatayo katika mikataba ya PSA .
hiyo asilimia 65 au 75 mnayogawana ni ya profit na siyo mapato kwani ktk mapato inabidi utoe gharama za uzalishaji halafu kilichobakia ndiyo hilo panga la hizo asilimia linapigwa. utata namba wani unakuwa ktk hili lifuatalo hatujui serikali ilichosaini kwenye kitu kinaitwa kitaalamu AFE hapo ndipo mara nyingi huwa serikali na nchi nyingi husika zinapopigwa bao. forget about profit, forget about revenue, forget about anything the most important document is AFE full stop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…