Waziri Mpango: Serikali ipo katika majadiliano ya IMF kuhusu ripoti ya Tanzania

Kwa ile report serikali ina hoja. Ukubwa wa hii habari umetokana na dhana ya serikali kuificha lakini content zake ni za kawaida maana ndio mijadala yetu ya kila siku.
 
Wataalam wa imf wamewasikiliza kina zzk na lissu badala ya kusikiluza wataalam wa serikali ndio maana kina lissu na zzk wanafurahia.

Wataalamu wa serikali wameacha weledi wamegeuka wapika data kwa kigezo cha uzalendo uchwara.
 
Kama kuna kitu nimejifunza kutokana na hii mijadala kuhusu ripoti za IMF na hata ile ya CAG, sisi watanzania ni wazuri sana kwenye kushabikia lakini wavivu/wagumu sana kwenye kutafuta taarifa sahihi. Kwa mfano:

1. Kuna baadhi ya watu wanashupalia kuwa IMF wanaandaa taarifa kuhusu hali ya uchumi wa nchi ilhali tuna wataalamu wetu ndani ya nchi ambao wanaweza kufanya hivyo. Je tunajua hata hizi taarifa zinatayarishwa vipi? Mbona hili liko wazi kwenye tovuti yao? https://www.imf.org/external/about/econsurv.htm

Sehemu ya taarifa hiyo:
Country surveillance
Country surveillance is an ongoing process that culminates in regular (usually annual) comprehensive consultations with individual member countries, with discussions in between as needed. The consultations are known as "Article IV consultations" because they are required by Article IV of the IMF's Articles of Agreement. During an Article IV consultation, an IMF team of economists visits a country to assess economic and financial developments and discuss the country's economic and financial policies with government and central bank officials. IMF staff missions also often meet with parliamentarians and representatives of business, labor unions, and civil society.

The team reports its findings to IMF management and then presents them for discussion to the Executive Board, which represents all of the IMF's member countries. A summary of the Board's views is subsequently transmitted to the country's government. In this way, the views of the global community and the lessons of international experience are brought to bear on national policies. Summaries of most discussions are released in Press Releases and are posted on the IMF's web site, as are most of the country reports prepared by the staff."

Huu ni utaratibu kwa kila nchi mwanachama wa IMF.

2. "Hakuna nchi mwananchama wa IMF, amepata maendeleo kwa kufuata ushauri wa IMF". Kweli inamaanisha nchi zote 189 ambazo ni wanachama wa IMF hakuna hata moja iliyoendelea kiuchumi? Ujerumani, Marekani, Uchina,nk. ni wanachama wa IMF na wao hawajaendelea?! Unadhani hizo taarifa wanazotoa ndio zinadidimiza/kukuza uchumi au zinaakisi uchumi uliodidimizwa/kukua?

3. "Wasitupangie uchumi wetu"

Kazi ya IMF siyokukupangia uchumi wa nchi ila kutathmini hali yake uchumi na kushauri kiutaalamu. Nchi inamaamuzi ya kufuata huo ushauri au la. Ila IMF inawajibu na mamlaka (kupitia mikataba iliyotiwa sahihi na nchi mwanachama) kutathmini na kutoa ripoti yake kwa utaratibu uliokubaliwa. Ikiwa walitoa ushauri nchi ifanye ABC ila nchi ikafanya EFG na bado uchumi ukaonyesha matokeo chanya kutokana vigezo vya tathmini, basi IMF hawawezi kupinga matokeo hayo. Hata wanavyovitathimni viko wazi kabisa kwenye tovuti yao

What does the IMF look at?
  1. Exchange rate, monetary, and fiscal policies.
  2. Financial sector issues assessment..which enables the IMF and the World Bank to gauge the strengths and weaknesses of countries' financial sectors.
  3. Assessment of risks and vulnerabilities stemming from large and sometimes volatile capital flows
  4. Institutional and structural issues: developing, implementing, and assessing internationally recognized standards and codes in areas crucial to the efficient functioning of a modern economy such as central bank independence, financial sector regulation, and policy transparency and accountability.
Hayo ni kwa uchache tu.

"Je inawezekana IMF wamekosea/wanapotosha? Iweje mwaka jana projection ilikuwa juu na mwaka huu ripoti inaonyesha projection imeshuka sana?": Maswali yanayolenga kufahamu zaidi kuhusu taarifa au ripoti hizi ni muhimu kuliko vijembe tunayorushiana. Tathmini ya kitaalamu hupingwa kwa tathmini ya kitaalamu, tena kwa uwazi wa hali ya juu.

Ila jamani kama ligi za kimataifa tunazishindwa basi ni bora kujiengua kulikoni kulialia hovyo kuwa tunaonewa kwasababu ni "watoto wa kambo tusiotaka mpira wetu uchezewe"
 
Uzi huu sijawaona wale watu wa hovyohovyo kutoka Lumumba vipi kunani
Ripoti ya imf imeandikwa kwa lugha ya kiingereza. Ingekuwa ya kiswahili mbona wangeshakuwa wakati kama pilipili kichaa. Mimi namshukuru sana mwl nyerere kuruhusu English kuwa lugha mojawapo maofisini vinginevo wangetusumbua sana hawa lumumba.
 
Aisee tuta mengi
 
14 day's not far Mpango😎
 
Hii sitaki, nataka inayofanywa na serikali yetu itatufikisha pabaya, muda ni mwalimu mzuri sana !
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana.

Bado mu miongoni mwa nchi masikini duniani halafu mnabishania ripoti ya uwezo wa kukopesheka?!

Mnataka kukopa nini?
 

Uzi unaongelea IMF wewe unaongelea CAG!

Hivi huwa mnaelewa hata kinachojadiliwa ni nini? Au mradi muandike tu? Eti kwa kuwa tu sasa unamiliki kisimu kinachokuwezesha kuandika kwenye mtandao.
 

Unataka kukopa nini?
 
Comedy inaanzia hapa " kazi, maana IMF inaihitaji Tanzania zaidi ili kutukopesha"
Nacheka mpaka nasinzia walahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…