FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,192
Kuna vitu viwili kwenye hoja yako, ambapo kimoja ni sahihi na kingine si sahihi. Mosi kama tukichukuwa kuwa hoja ya Serikali uchumi unakuwa kwa zaidi ya 6% basi hoja ya IMF ya 4% inatkuwa si ya kweli. Na kama ukichukulia hoja ya IMF ni sahihi basi kwa upande wa pili basi takwimu za Serikali si sahihi na hivyo basi kuna kupikwa kwa data ili kuonyesha wananchi tupo na muelekeo mzuri.
Ila kwa maoni yangu, IMF huwa hawadangani tuliona ya Zimbabwe na kwa mataifa mengine mengi tu
Takwi za kukua kwa uchumi zinategemea "research data" imetokea wapi na imefanyika na nani.
Tanzania ilipitishwa sheria ya takwimu zote zitokee na zitolewe na sehemu maalum iliyoruhusiwa. Naamini maalum bank baina ya serikali na IMF ni takwimu za IMF wamezipata wapi na zimeruhusiwa na nani?
Ukuwaji wa uchumi kwa asilimia yoyote ile hauashirii uwezo au ubora wa maisha kwa raia. Hiyo simply ni report inayosaidia kukopesheka na uwekezaji.
Sifahamu mnachobishana nini kuhusu hiyo report kwani unaweza kuwa na uchumi a unaokua kwa asilimia 10 lakini na wewe umeongeza raia kwa asilimia 11. Ukuwaji wako umekusaidia nini?
Au unaweza kukua kwa asilimia 10 ya billion moja na mwengine akajuwa kwa asilimia Tatu ya trillion moja. Nani zaidi hapo?
Kumbuka kuwa reports za IMF na world bank zinalenga au kujenga uankubomoa kutokana na hali ya faida kwa nchi zenye kufaidika kuwakopesha mikopo ya masharti maalum, si vinginevyo.
Mnachobiashania humu ni nini haswa? Sijaona mantiki.