Waziri Mpango: Serikali ipo katika majadiliano ya IMF kuhusu ripoti ya Tanzania

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Fedha, Dkt. Phillip Mpango amelieleza Bunge leo mjini Dodoma kuwa Serikali iko katika majadiliano na IMF kuhusu ripoti ya Tanzania na kuna siku 14 za kujadiliana kufuatia wataalamu waliotumwa awali kutozingatia hoja za upande wa Serikali kama ulivyo utaratibu.
 
Inawezekana nikawa sina uweledi wa juu ya uwasilishaji wa taarifa za nchi katika jumuiya yeyote ya kimataiafa, ila naamini taarifa itabakia kuwa taarifa pindi baada ya kutayarishwa na kukidhi vigezo vya kuwa taarifa na kukabishiwa kwa upande husika ambao ndio wataichapisha au kuisoma na kuifanyia kazi kimya kimya. Kinachonishangaza ni kuwa kuna wataalamu ambao walitumwa awali na hawakuzingatia hoja za serikali kama ulivyo utaratibu? hapa kidogo kina ukakasi

Taarifa lazima iwe na vyanzo vyake ambavyo vinaaminika, kisha zinakusanywa pamoja na taarifa nyengine na kutengenezwa taarifa mama, sasa unaposema kuna wataalamu hawakua upande wa serikali ni kwamba taarifa haikuwa sahihi, au kuna data ambazo zinakinzana na yanayozungumzwa kwenye vyombo vya habari, hansad za bunge, kwenye tovuti za serikali au vp?

Ifike mahali kama kuna weusi tukubali kwamba mambo ni meusi na sio kusema mambo meupe wakati kabisa unaona kuna mambo meusi nyomi yametamalaki ndani yake. Hakuna binaadamu aliye kamili chini ya jua, na kama ulikuwa na nia njema ila hujafanikiwa basi amini katika vitabu vitakatifu kwamba kila zama na kitabu chake na ukiona jambo halijatimia basi jua wakati wake bado.

Au taarifa hizi ziliandikwa kwa mother tongiyo sasa wanataka kuziandika kwa kiingereza ndo wanapaeleka wataalamu wa kuzitengeneza? Ashindwaye pia ni mume toa taarifa watu wazione au ndo kama za Alhaj Asad wakataka kuficha ukweli naye akarusha bomu la Hiroshima mjini Dodoma mambo yakatindinganya.
 
Bunge letu chini ya comrade Ayubu kutoka kongwa lipitishe azimio LA kutofanya Na IMF
Waziri wa Fedha, Dkt. Phillip Mpango amelieleza Bunge leo mjini Dodoma kuwa Serikali iko katika majadiliano na IMF kuhusu ripoti ya Tanzania na kuna siku 14 za kujadiliana kufuatia wataalamu waliotumwa awali kutozingatia hoja za upande wa Serikali kama ulivyo utaratibu.
 
Something must have gone wrong somewhere. Haiingii kichwani ndani ya miezi mitatu hesabu ziteremke kutoka wastani kwa mwaka wa 7% hadi 4% bila kuwa na tukio kubwa (janga) lililotokea, hususani vita au "a big natural disaster". Tetemeko la Kagera kamwe haliwezi kuwa sababu. So what had happened in that period to justify for that sharp decline of these statistics? Ndiyo maana wajumbe toka IMF wako hapa kwa majadiliano na maafisa wetu wa BoT.

Tukumbuke katika kipindi hiko kulitokea mabadiliko ya uongozi wa juu wa BoT baada ya Gavana wake, Prof Ndulu kustaafu kwa mjibu wa sheria. Inawezekana hand-over ilikuwa haijakamilika vizuri wakati maofisa wa IMF walipotutembelea. Tuwe na subira ukweli utajulikana baada ya tathmini mpya ndani ya siku 14 kama alivyoahidi Mh. Mpango.
 
Viongozi wachumia tumbo..mafisadi wanaogopa kuanikwa wazi,..kama mwajiamini kwanini muogope sasa..ndio mana Ripoti ya CAG mmetulia tuli kama hamuioni kumbe mjaa ufisadi..

Mwogopeni Mungu,Ogopeni kodi za wavuja jasho wa Tz.
Simamieni haki na kweli...mjisahihishe

Nchi yetu sote hii.
 
Back
Top Bottom