Waziri Mpango 'ameteleza', asamehewe

Waziri Mpango 'ameteleza', asamehewe

Waziri Wa Fedha na Mipango., Dr. Phillip Mpango amelivuruga Bunge. Ni kama amesababisha vurugu zisizo na tija Bungeni. Ni baada ya 'kulitumia' Bunge kupiga kampeni kwa chama chake cha CCM kuelekea Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa, Oktoba mwaka huu.

Kiukweli, Waziri Mpango amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali iliyosheheni matumaini makubwa kwa weledi na umakini mkubwa. Ameiwasilisha kwa kuelewekavyema na kwa umahiri mkubwa. Lakini, alipoingiza 'kampeni kwa CCM' aliteleza.

Alianza vyema kutaja sifa zinazofaa kuwepo kwa viongozi wetu na wanaotaka kuwa viongozi wetu. Sifa ya kwanza hadi ya tisa zilikuwa ni sifa za jumla na njema Sana. Ya kumi iliyoleta mtafaruku ilianza vyema kuwa atokane na chama chenye kupigania maslahi ya taifa. Kuitaja CCM ndiyo kuteleza kwenyewe.

Kimsingi, Waziri Mpango hakupaswa kulifanya Bunge kuwa jukwaa LA kampeni kwa CCM. Alisababisha kelele na vurugu zisizo na maana Bungeni. Bunge Si uwanja Wa kampeni Wa chama chochote! Aliteleza na asamehewe.
they will never listen!!!!
 
CCM kila walipo wao ni kampeni tu kama CCM inapendwa kwanini mpige kampeni kila penye mkusanyiko?
 
Kama kulia lia tu.. wakili leo hukutaka kukosa kupata la kulaumu kama kawaida yako na wenzako humu.

Hasingeyatamka hayo mngesema hata shukurani hawana.

Bajeti tamuuuuuu eeeeh
Tunazidi kupaaaaa

Magufuli oyeee
 
Ulitegemea asemeje wakati yeye ni mwana CCM? Ikumbukwe kwamba kila mbunge yupo bungeni kwa tiketi ya chama chake cha Siasa.

Isitoshe, katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli, imedhihirika wazi kwamba chama chenye kupigania maslahi ya taifa ni CCM, vingine ni SACCOS, vyama vya mifukoni au vina sura ya udini, ukabila na ukanda.
Umeinamishwa? kwani bungeni wote waliopo ni kutokana na vyama? au wewe ni miongoni.mwa.wapumbavu wanaosemwa na Magu?
 
Hoja na jibu lako yanadhihirisha kiwango chako cha ustaarabu. Asante
 
Ulitegemea asemeje wakati yeye ni mwana CCM? Ikumbukwe kwamba kila mbunge yupo bungeni kwa tiketi ya chama chake cha Siasa.

Isitoshe, katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli, imedhihirika wazi kwamba chama chenye kupigania maslahi ya taifa ni CCM, vingine ni SACCOS, vyama vya mifukoni au vina sura ya udini, ukabila na ukanda.
Hayo maneno yataendelea kusemwa kama yalivyo mpaka kihama labda matumbo yenu yewe yamechanika.
 
Ukikosea umma unapeta ukiikosea serikali ndio unatumbuliwa; JE serikali iko juu ya UMMA wa WATANZANIA?
 
Back
Top Bottom