Waziri Mkuu wa Pakistan ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Pakistan ajiuzulu

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif amejiuzulu wadhifa wake muda mfupi baada ya Mahakama ya Juu kumzuia kuendelea kushikilia ofisi hiyo kama kiongozi mkuu wa serikali.


Uamuzi huo umetolewa leo baada ya uchunguzi kuhusu utajiri wa familia yake na ufichuzi wa mwaka 2015 wa wanasheria walioupa jina la Panama Papers, uliohusisha watoto wake na akaunti za benki ugenini.


Jopo la majaji watano wa Mahakama ya Juu walitangaza hukumu mbele ya umati mkubwa wa watu waliofurika katika chumba cha mahakama.
"Ameondolewa kuwa mmoja wa wabunge na kwa hiyo anakoma kuanzia leo kuwa Waziri Mkuu,” alisema Jaji Ejaz Afzal Khan katika ukumbi uliokuwa umefurika watu jijini Islamabad.
WAZIRI.jpg

Kuondolewa kwa Sharif, kwa hoja kwamba alisema uongo kuhusu mali anazomiliki wakati alipochunguzwa kuhusu tuhuma za rushwa, ina maana sasa kwamba chama chake cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) ambacho kina wabunge wengi, kinalazimika kuteua kiongozi mwingine wa Serikali.
Serikali inaweza pia kuitisha uchaguzi wa mapema, ingawa uchaguzi mkuu utafanyika Agosti mwaka ujao
 
Safi Sna Wenzetu Wapo Active Na Vyombo Vyao,huku Kwetu Tunateua Kaimu Jaji Mkuu,haki Ipo Wapi?
 
Naona Jenerali Musharraf akifunguliwa na kurudi madarakani
 
Hawa jamaa unakuta anajiuzulu huku akiwa mwenye nguvu na akili timamu tofauti na kwingine!
 
Kwani Gen Pervez musharaf alifungiwa
alirudi kuja kugombea uchaguzi wa rais akafichwa sehemu salama kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Musharraf ndio alimngo'a huyo Shariff kwa kutishia kudungua ndege yake wakati anarudi kutoka hijja.miaka hiyo
 
... ina maana sasa kwamba chama chake cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) ambacho kina wabunge wengi, kinalazimika kuteua kiongozi mwingine wa Serikali.
Serikali inaweza pia kuitisha uchaguzi wa mapema, ingawa uchaguzi mkuu utafanyika Agosti mwaka ujao
Mbona jina lake ni sehemu ya jina la chama? Is it by coincidence?
 
Aliwahi kupinduliwa na Generali Perves Musharaf kabla ya kurejea Mamlakni, alimpindua Muda mfupi baada ya Nawaz kuwa angani kwa Safari Kwa hiyo kwa Muda huo hakuwa na Mawasiliano na Afisa wake yeyote

Perves wakati huo alikuwa ndie Mkuu wa Majeshi
 
Tutauweka sawa tu Tundu Lissu amesema hatuna nyamaza
lakini mkia huu unaweza kutufanya wafu kwa mamlaka ulionayo. sasa kelele hizi zinatosha kuukata mhimili huuuu?. kweri sky?. au unampimishia tu tundu lissu aingie kwenye tundu vizuri umfyatue?
 
Udikteta uchwara mbele kwa mbele eti ule mhimili mmoja umejikita zaidi chini kuliko mingine wakati katiba haisemi hivyo! Mh! Uongo mwingine!

mataifa yenye mihimili mikuu mitatu. serikali, mahakama na bunge. sisi tunaigiza tu
 
Mihimili mitatu inafanya kazi
Bahati mbaya sana wengi hawajui siasa za Pakistan na hoja si muhimili wa tatu kufanya kazi hoja hapa ni kuwa mahakama kuu ya pakstani ipo chini ya jeshi na jeshi la pakistan ndilo linanguvu kuliko serikali ni kama ilivyo kwa nchi ya Misri nguvu ya jeshi ni karibu 80% ya total power ktk nchi na jeshi la pakistan halipo tayali kuona raia anatawala au akipishana na jeshi akiendelea kuwa madarakani
Mpaka sasa hv pakistan kumeshapita mawaziri wakuu 18 na hakuna waziri mkuu hata mmoja aliyemaliza muda wake na huyu ndio angeweka record ya kumaliza muda wake madarakani lakini haikutokea hvyo kwani uchaguz ni mwaka kesho tu
 
Back
Top Bottom