Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyau adai Gaza hakuna njaa, wamekuwa wakiruhusu misaada kipindi chote cha vita

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyau adai Gaza hakuna njaa, wamekuwa wakiruhusu misaada kipindi chote cha vita

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
6,929
Reaction score
6,030
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema hakuna mtu anayekufa kwa njaa Gaza na kwamba Israel haijawahi kuwa na sera ya kuwanyima Wapalestina chakula

“Tunaruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza wakati wote wa vita la sivyo, kusingekuwepo na Wapalestina Gaza,” alisema Netanyau

Lakini Rais wa Marekani, Donald Trump, hakubaliani naye. Akizungumzia picha zinazoonyesha watoto waliokonda sana, Trump alisema: “Watoto wale wanaonekana wana njaa sana.” Kauli hiyo imekuja wakati ambapo mashinikizo ya kimataifa yamelazimisha Israel kutangaza kusitisha mapigano kwa muda mfupi na kuruhusu misaada zaidi kuingia Gaza. Hata hivyo, wakaazi wa Gaza wanasema hali haijabadilika; bado misaada haitoshi au haifiki kabisa. Umoja wa Mataifa umeeleza hatua hizi kama ongezeko la wiki moja la msaada, lakini Israel haijaweka wazi ni kwa muda gani utaratibu huo utaendelea

Israel inaishutumu Hamas kwa kuzuiwa kwa misaada hiyo, ikidai kuwa wapiganaji wake wanaiba misaada kwa ajili ya kuendesha utawala wao

Umoja wa Mataifa unakanusha madai hayo, ukisema wizi wa misaada si wa kawaida na huwa unadhibitiwa pale misaada ya kutosha inapopelekwa. Changamoto nyingine ni kuwa misaada inapowasili kwenye mpaka wa Gaza, U.N. inahitaji ruhusa ya kijeshi ya Israel kuichukua – lakini zaidi ya nusu ya maombi ya ruhusa hizo yamekataliwa katika miezi mitatu iliyopita. Iwapo magari ya U.N. yakifanikiwa kuichukua, mara nyingi hukumbana na misururu ya watu wenye njaa na makundi yenye silaha yanayoiteka na kuchukua chakula. Polisi wa kiraia waliokuwa wakiwapa ulinzi, walioko chini ya Hamas, wamesitisha kazi hiyo baada ya kushambuliwa kwa mabomu na Israel

=====


Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu says no one in Gaza is starving: “There is no policy of starvation in Gaza, and there is no starvation in Gaza. We enable humanitarian aid throughout the duration of the war to enter Gaza – otherwise, there would be no Gazans.”

President Donald Trump on Monday said he disagrees with Netanyahu’s claim of no starvation in Gaza, noting the images emerging of emaciated people: “Those children look very hungry.”

After international pressure, Israel over the weekend announced humanitarian pauses, airdrops and other measures meant to allow more aid to Palestinians in Gaza. But people there say little or nothing has changed on the ground. The U.N. has described it as a one-week scale-up of aid, and Israel has not said how long these latest measures would last





Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu speaks to the audience at a conference in Jerusalem, Sunday, July 27, 2025. (AP Photo/Ohad Zwigenberg)





Source: AP News, DW & CNN
 
Wavaa Makobazi kama wanahuruma sana,kwanini wasiondoke kwenda kuwasaidia gaza?

Yaani unamuonea huruma gaidi wakati huo wewe umejikunyata kwenye shuka !

Hiyo Gaza inapaswa ifutwe kwenye uso wa Dunia!
Sikiliza Binti,hao wayahudi waliomsulubu Mungu wako,huu ni mwaka wa 2 wanahangaika na kaeneo kadogo tu kama Gaza,uwezo wao ni kupiga wanawake na watoto tu,Hamas inawapelekea moto,kila siku wanarudishwa ndani ya masanduku,Pamoja na kupewa silana na kusaidiwa kila kitu na Westerners ila ngoma imewashinda,

Wewe nenda kawasaidie kuwaokoa mateka wao waliotekwa kwa zaidi ya miaka 2 sasa.
 
Hata Hitler hakuwa KATILI KIHIVI!
🥺☹️😭
Hitler hakuwa katili bali alikua anapambana na hawa makatili waliojipenyeza ujerumani wakaanza kuungana na maadui wa ujerumani.
Ni vile tu tecnolojia imekua maana bila hivo wangebadilisha hata historia ya hiki wanachotenda pale Gaza na kujifanya wao ndio wanatendewa
 
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu:

Hakuna njaa huko Gaza, hakuna sera ya njaa huko Gaza, na ninawahakikishia kwamba tuna dhamira ya kufikia malengo yetu ya vita.

Tutaendelea kupigana hadi tufanikiwe kuachiliwa kwa mateka wetu na kuuangamiza uwezo wa kijeshi wa Hamas na utawala wao na hawatakuwepo Gaza tena.
Hamas sio wanamgambo tena,sasa ni wanajeshi(wana ewezo wa kijeshi)
 
Marabbi zaidi ya 100 wamesaini barua kuitaka serikali ya Israel iache kutumia njaa kama silaha ya vita.

Taasisi ya haki za binadamu ya B'Tselem ya Israel kwa mara ya kwanza imesema serikali yao ya Israel inafanya Genocide huko Gaza.

Meanwhile kuna mtu mmoja hapa JF anaamini akimbariki Netanyahu na kushangilia mauaji ya wanawake na watoto basi huo ndo Ukiristo wenyewe na atalakiwa na bwana Yesu mawinguni.

Wewe mleta mada hebu soma hii article kutoka katika gazeti linaloheshimika la Times of Israel

 
Back
Top Bottom