Waziri Mkuu wa DRC ajiuzulu

Waziri Mkuu wa DRC ajiuzulu

Jean Pierre Bemba Gombo anajiandaa kuchukua wadhifa huo,

kwasasa ni waziri wa ulinzi,
baada ya kusota jela kwa zaidi ya miaka 10 katika sero za ICC huko Hague, akikabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita, madhila yaliotoke kabla ya 2008 akiwa miongoni mwa Makamu wa Rais wa wakati huo DRC 🐒
Yes Bemba anafaa kuwa PM wa DRC
 
angeachwa nje ya serikali angesumbua sana, halafu ni wale watu wenye nyota ya kupendwa na watu bila sababu 🐒

Alipotoka Hague alipata mapokezi ya nguvu sana DRC, kumbuka alikamatwa 2008 akiwa madarakani kama makamu wa Rais, tena alikamatwa akiwa njiani nje ya nchi safari ya kikazi 🐒

Ni kiongozi wa upinzani lakini pia alikua kiongozi wa waasi ambae alihusika uhalifu wa kivita DRC na Central Africa. Rais Felix Tshekedi anaamin huyu ndie mtu sahihi kudeal na hayo makundi ya waasi kwasabb anaweza kua anayafahamu vizuri ndio maana akapewa dhama ya ulinzi 🐒

Hata hivyo,
kwa hali ya kisiasa ilivyo DRC, Rais Felix Tshekedi anaamin huyu ndugu Jean Pierre Bemba ndie mtu sahihi wa kurithi mikoba yake atakapo maliza ngwe za uongozi wake miaka kadhaa ijayo, ili aishi kwa amani akiwa amestaafu 🐒
umeandika nilichotaka kuandika kuhusu warlord Jean Pierre Bemba
 
Mimi nadhani baada ya uchaguzi na yeye kushindaa,kuunda serikali mpya ni kawaida...na waziri mkuu kuwakilisha barua cuz ni utaratibu baada ya kuambiwa inaundwa serikali mpya.

Nimefikiria tu hivyo,nipo tayari kwa masahihisho.
 
Back
Top Bottom