Waziri Mkuu: Sukari haitakuwa tatizo Ramadhani

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300.

Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha Mipango mjini hapa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.

Pia alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000 zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.

Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.

“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema.

“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”

Alisema suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo.

Katika miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini, imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka nje ili kukabili upungufu uliopo.
 
Serikali ya Maigizo. Walisema sukari haitazidi Sh. 1,800 kwa kilo lakini sasa anasema tena isizidi 2,300. Kweli hii nchi imejaa maigizo ya Mzee Juha. Walisema hawataagiza sukari nchi za nje maana wamejipanga kumbe hata takwimu za mahitaji ya sukari katika nchi yetu kwa mwezi hawakuwa nazo. Hahaaaa kweli hii ni Bongo tambarare.
 
Tatizo s
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300.

Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha Mipango mjini hapa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.

Pia alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000 zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.

Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.

“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema.

“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”

Alisema suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo.

Katika miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini, imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka nje ili kukabili upungufu uliopo.
iyo Sukari..Tatizo bei ya Sukari......
 
Kwani ile bei ya 1,800/= nayo si lilikuwa Agizo
 
Hivi kuna haja gani ya kutoa bei elekezi wakati hiyo bei haielekezeki? leo asubuhi nimenunua sukari 3,500 kilo, wakati anasema sukari iuzwe 1800 alitumia data zipi na sa hivi hiyo 2300 anatumia data zipi?. Ila sio kesi ikifika 15,000 kwa kilo ndo taanza kulalamika rasmi sa hivi nimeamua nife kiume.
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu, suala si upatikanaji tu, bali hata bei.serikali ilipoweka bei elekezi ya sh.1800 tuliambiwa atakayeuza bei zaidi ya hiyo akamatwe,lakini sukari iliuzwa hadi sh 5000 tena bila kificho. sasa Mheshimiwa unasema "unawasihi" wafanyabiashara bei isizidi sh.2300. pale mlipotoa amri ya bei hawakutekeleza,sasa hili la kuwasihi linakuwaje?na hao wakuu wa wilaya na mikoa watasimamiaje hiyo bei wakati sio wataalamu wa biashara halafu ukizingatia sio amri ni ombi kwa wafanyabiashara? si wataishia tu kudanganywa kwa gharama wasizozijua?
 
Back
Top Bottom