Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live Tbc

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
1-18-768x514.jpg

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live na Television ya Taifa kama serikali ilivyosema na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

”Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku”Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.
globalpulishers
 
Tunaomba tuchangishwe kila mpenda Bunge shilingi za Kitanzania mia moja ili kuiwezesha TBC kurusha live kwani tunahitaji kujua tunatoka wapi na nchi yetu na wabunge wetu tutajuaje wanatuwakilishaje? Hapana Tunaomba utaratibu uandaliwe tuchangie mpaka pale Bunge litakapo isha Serikali ikishirikiana Na kampuni za Cm waweke namba maalumu tutachangia
 
Tunaomba tuchangishwe kila mpenda Bunge shilingi za Kitanzania mia moja ili kuiwezesha TBC kurusha live kwani tunahitaji kujua tunatoka wapi na nchi yetu na wabunge wetu tutajuaje wanatuwakilishaje? Hapana Tunaomba utaratibu uandaliwe tuchangie mpaka pale Bunge litakapo isha Serikali ikishirikiana Na kampuni za Cm waweke namba maalumu tutachangia

Khaaaa! mbona TBC tunaichangia kitambo tu kupitia kodi zetu?
 
Huu ni mwanzo mbaya kwa serikali hii ya awamu ya tano tulidhani tumepata kumbe tumepatwa
Tutazid kuisomba namba,sio tulomchagua lowassa tu haya nyie mlochagaua hawa wAnaounga mkono binge lisiteme jino mo ,Bado mengi yanakuja ikiwemo Sheria ya mtandao itawaumiza wengi.Hii ndio Tanzania according to roma
 
...hivi haya mamlaka ya serikali kuliamulia bunge yanatoka wapi?! hawa watu mbona madaraka yamewapofua sana!!
 
...hivi haya mamlaka ya serikali kuliamulia bunge yanatoka wapi?! hawa watu mbona madaraka yamewapofua sana!!
Hawajaliamulia bunge ila TBC imesema haina pesa za kuonyesha live kipindi cha bunge muda wote
 
Naomba niulize ,kwani vyombo binafsi kupewa kibali haiwezekani?au bado ni shughuli kama TBC hawana fedha ya kutosha!Mimi mwenzenu sijaelewa hata kidogo .Kwani naamini vituo vingi binafsi vinaweza kufanya hivyo kama issue ni serekali kubana matumizi.Magu umetisha sana,miaka mitano tutaona mengi walahi!!!!
 
ukawa waanzisshe radio kama uhuru na waonyeshe bunge. wapitishe harambee. ila wajjiepushe propaganda kali wasiije fungiwa
 
Kuna unafiki mkubwa umejificha nyuma ya uamuzi wa serikali kuruhusu TBC kutorusha LIVE mkutano wa 11 wa Bunge letu tukufu. Tusubiri!?
 
Back
Top Bottom