Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live Tbc

Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live Tbc

hapa kazi falsafa imeanza vibaya matangazo ya moja kwa moja kwa bunge si hiari na serikali ilitakiwa ihoji ukosefu wa pesa za kurusha matangazo ,ila kutokana na kuwa ni chombo cha umma ,ukosefu wa fedha umeonekana ni sahihi .ikiwezekana watangaze tenda kwa kufuata taratibu ili wananchi wenye nafasi wapewe kazi ya kurusha matangazo ,na sio serkali kubariki uamuzi huo.kinachoonekana kwa nje ni kuwa watawala wanaogopa vivuli vyao wenyewe ,na kunyima raia uhuru wa kupata habari kikatiba .
 
Hii inshu naona kama inakuzwa hivi.. Haya mahaba ya ghafla na TBC Sijui lengo lake..
 
Huko mbele ya safari asije akasema tena kwamba serikali haikukataa bunge lirushwe Live ,kama alivyokuja hapa na habari kwamba hakukataza maandamano ya kisiasa bali alikua anaongea kama mbunge ,hata kama ulikua unaongea kama mbunge kuna mbunge mwenye mamlaka ya kupiga marufuku maandamano ya kisiasa ????
 
Huu ni mwanzo mbaya kwa serikali hii ya awamu ya tano tulidhani tumepata kumbe tumepatwa
Wewe huna kazi ya kufanya na unataka muda wote uangalie bunge tuu? Mbona usiku kila siku wanaonyesha ndugu? Au ndiyo bendera kufuata upepo? Hapa kazi tuu na si lelemama. Mnataka kutoka kimaisha kazi hamtaki mnataka kuangalia binge live. Hahahahaaaa. Wabongo bana. I like you guys.
 
Na hotuba za rais tuwe tunaonyeshwa usiku.. Hata akizindua au akitumbua majipu waonyeshe saa nne usiku magazeti watu wasome usiku.. Habali zote zianze saa nne usiku.. Hii serekali inaweza kuwa mbovu kuliko zote.. Mmeshindwa hata kuwasilisha mpango wenu wa miaka mitano bungeni
 
Back
Top Bottom