Waziri Mkuu Pinda kwanini hutaki demokrasia mtaani kwako?

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita umeonyesha rangi halisi ya CCM na viongozi wake.

Mtaa wa Kigogo Fresh B Pugu-Ukonga anaishi Waziri mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda.Siku ya uchaguzi tarehe 14 December uchaguzi ulivurugika haukufanyika na mkurugenzi akatangaza ungefanyika wiki moja baadaye.

Mgombea wa Chadema aliaminiwa na wananchi wa mtaa huu kwa sababu anayajua matatizo ya watu wa Pugu.Wananchi walitaka kumpa ushindi wa zaidi ya asilimia 90% uchaguzi ungefanyika.Mgombea wa CCM alishindwa hata kufanya mkutano wa wazi kwa sababu kila alikokuwa anapita anazomewa na hata watoto wadogo.

Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi wa Marudio mkurugenzi wa Ilala akiwa amejifungia ofisini alimtangaza mgombea wa CCM kwamba ndiye mwenyekiti mpya wa mtaa wa Kigogo Fresh B bila ya uchaguzi.

Tangazo hili lilileta hasira kubwa kwa wakazi wa mtaa huu na wakaamua siku ya kuwaapisha kutumia nguvu ya Umma kumzuia mkurugenzi kufanya uhuni huu.Na kweli mkurugenzi akashindwa na kuahirisha zoezi.

Sasa kuna taarifa kwamba wakubwa wameamua ni lazima wamuapishe mtu wao waliyemuweka madarakani kwa njia ya mapinduzi.Kwamba ataapishwa leo Alhamisi tarehe 22/1/2015 saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Anatougle kwa sababu Waziri mkuu kamwe hawezi kuongozwa na Chadema mtaani kwake.

Wananchi wa Kigogo Fresh B wamesema kamwe hawatakubali udikteta huu kwenye mtaa wao.

Tusubiri tuone.....

Updates....

Kutoka Anartouglou ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mgombea wa ccm mtaa wa Kigogo Fresh B aliyetaka kuapishwa kinyemela amezuiwa na nguvu ya UMMA kwa kupigwa vibaya na umati mkubwa wa watu uliotanda nje ya ukumbi huo.

Mgombea huyo wa CCM amepigwa mpaka alipookolewa na polisi waliofika eneo hilo kumuokoa.
 
Hata kama hataki kuogozwa na chadema ataoongozwa tu 2015 ataongozwa na ukawa na wakileta za kuleta tunafanya kama wananchi wa migombani dar tunaleta wakili nguvu ya uuma inachukua nafasi
 
Pinda mhuni tu akisimama bungeni analialia akijifanya mtakatifu kumbe panya tu.
 
Hata kama hataki kuogozwa na chadema ataoongozwa tu 2015 ataongozwa na ukawa na wakileta za kuleta tunafanya kama wananchi wa migombani dar tunaleta wakili nguvu ya uuma inachukua nafasi

huyu tujichukua nchi Kwa ujambazi anaofanya kwake Ni gereza LA segerea tu...
 
Halafu naye huyu asiyeamini ktk demokrasia anataka kuwa Rais wa Tanzania. Really? Yaani 'rais mtarajiwa' asiyeheshimu matakwa ya watu; asiye mwaminifu ktk yaliyo madogo huyo hakika hatufai

Watanzania wote kwa ujumla tuko pamoja na wananchi wa Kigogo Fresh B kwmba wana haki ya msingi ya kukataa dhuluma na unyanyasaji mkubwa namna hii

Hakika nguvu ya umma itashinda tu
 
huu urahisi huu mpaka wapumbavu wanautaka..
 
Hii ni aibu kubwa sana sana!!!! na ni picha tosha ya kuonyesha bado tanzania ni nchi maskini sana hasa "KIFIKRA"
 
Asante kwa taarifa mkuu. Naamini wananchi na wapenda amani wa MTAA WA KIGOGO FRESH "B", watachukua uamuzi sahihi kwa ajili ya haki kutendeka. CCM ni kama EBOLA
 
Hili ni anguko kubwa mno kwa Pinda kama Waziri mkuu na kiongozi wa chama chawala ni upepo mbaya mno kisiasa
 
.ccm ni kidole yenye kansa na lazima ikatwe tu.......wananchi wa Pugu hawa mafisadi siku zao zinahesabika.

Hawa ni wa kudelete tuuu!
 
CCM siku zote haitaki amani yetu iendelee kudumu. Wao wanaanzisha fujo halafu wanakuwa wa kwanza kulalamika. Itawezekana wapi watu wang'ang'anie madara kiasi hiki halafu waachwe tu !!? UKAWA jiandaeni hii ni sura mbaya kwa uchaguzi mkuu ujao, msipoziba ufa mtajenga ukuta.
 
Hili ni anguko kubwa mno kwa Pinda kama Waziri mkuu na kiongozi wa chama chawala ni upepo mbaya mno kisiasa

Hatuko tayari kutawaliwa na madikteta, hata kidogo. Tusimame pamoja tupinge dhuluma hii siku zote
 
Akiapishwa kwa ridhaa ya Pinda huyo atakuwa ni Mwenyekiti wa CCM,wananchi nao watafute njia mbadala ya kumuapisha Mwenyekiti Wao wanaoamini kuwa ndiyo chaguo Lao.
 
Hivi kweli waziri mkuu ambae badala ya kuwa custodian mzuri wa kusimamia haki na sheria za nchi yeye ndie anavunja mhhhhh

Tumesikia ametangaza kugombea urais kimya kimya! shame on him, mpuuzi kabisa huyu.
 
.ccm ni kidole yenye kansa na lazima ikatwe tu.......wananchi wa Pugu hawa mafisadi siku zao zinahesabika.

Hawa ni wa kudelete tuuu!

Dah ni kweli mkuu LiverpoolFC CCM ni kansa sugu, imeshasambaa mwilini kote, yafaa kuukata mwili wote hawafai hawa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom