Waziri mkuu Pinda , anakatisha tamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu Pinda , anakatisha tamaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkomatembo, Jan 27, 2012.

 1. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Nimesoma kwenye magazeti ya leo karibu mengi yanaongelea jinsi Waziri mkuu Pinda alivopinda (kukwepa) kuongea na Madaktari angalau asikilize kilio chao kama alivowasikiliza wabunge na hatimae jana au juzi akatoa tamka huku akiwatetea wabunge kuwa wana hali ngumu ya maisha na kuainisha mshahara wanaopata na madhila wanayopata majimboni mwao na hilo ndio limepelekea kuongezewa mshahara.

  Najiuliza , waziri mkuu huyu ni wa wabunge na kuoneza posho au ni wa waTanzania wote.

  Juzi juzi tumesikia jinsi wanaKigamboni walivopandishiwa nauli na jinsi mbunge alivojitutumua kupigania watu wake na kuahidi swala hilo lipo kwa Waziri mkuu lakini mpaka sasa KIMYA na watu wanaendelea kulipa pesa nyingi hasa wa magari na maguta na mizigo.

  Na mambo mengi ambayo yeye kama Waziri Mkuu anatakiwa ayatatue lakini sielewi yupo kimya!

  Kitu ambacho kimeniuma kupita kiasi ni hiki cha Madaktari, kweli Waziri mkuu ameshindwa kuwasikiliza hawa madaktari wakati jana tu tumesoma Waziri huyu huyu mkuu akiwatetea wabunge na posho yao ya Tsh 200,000 kwa siku huku akisisitiza kuwa ETI WANA HALI NGUMU! jamani tumuogope Mungu, hebu aende aone wagonjwa wanavokufa pale Muhimbili au kwa sababu wao wanatibiwa India ?

  Kweli Pinda bora alivosema hataki kugombea uRais maana sidhani kama angeweza japo ANATAMANI SANA !
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  i am sick and tired with this guy, muongo wa kupindukia
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu yuko sahihi kabisa, hana madaraka ya kuongea wala kupata solution ya madaktari, hili linamhusu Rais mwenyewe, kama Waziri mkuu angekuwa na madaraka nchi hii basi asingempikia simu Rais kumuomba mwongozo wa kuhusu Jairo angemfukuza kazi siku ile ile.

  Hili swala ni la JK msubilini akimaliza picnic huko majuu atalikuta na ataangalia kama lina umuhimu wa kuwasikiliza au ni kiherehe chao tu hao madaktari, kwanza JK haitaji tena kura za wafanyakazi yeye anaandaa miposho yake ili akistaafu awe anakula raha mustarehe.

  By the way kile kibabu cha Kizenji kinachoitwa makamu wa Rais hivi shughuli yake hasa ni nini kwenye nchi hii? kwani Rais akiwa hayupo nchini ni nani anakuwa mkuu wa nchi? Hiki cheo cha makamu wa Rais kinahitaji mjadala mpana sana, ni mzigo kwa Taifa letu, hakuna haja ya kuwatengea Wanzibar cheo hichi ili waje kutafuna tu kodi zetu bila ufanisi wowote.
   
Loading...