Waziri Mkuu ndio mwenye jukumu la kubeba mchanga wa dhahabu huko Buzwagi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,914
Hivi Waziri Mkuu alikwenda Buzwagi kwa lengo la kufanya ziara au lengo hasa lilikuwa kuchukua mchango?

Kama ni kuchukua mchanga,hilo kweli ni jukumu la Waziri Mkuu?

Au ndio tutaambiwa swala la kuchukua mchanga limeibuka tu wakati wa ziara hiyo na halikuwa kwenye agenda?

Mimi mbona hapa sielewielewi!!
 
Nafikiri ndio alichopangiwa na Mkulu juzi mara baada ya kupokea report ya CAG..
Mpaka PM ndio akabebe sample..??
Mambo mengine bwana.
 
Jamani, msishangae tatizo ni kuwa wapigaji ni wengi sana kila kona.

Wewe angalia watu wanasema mtambo wa kuchenjua ni lazima uwe 150,000 tones wakati wao wanaweza kutoa 60,000 tones.

Hivyo, hawataki kutafuta mitambo midogo, kana kwamba mitambo iliyopo duniani kote ni mikubwa pekee.

Sasa, hapo kumbuka kuwa ni wataalamu wetu waliofanya huo utafiti uchwara kuwa ni mitambo mikubwa tu iliyopo wakati ukweli ni kuwa kuna mitambo midogo pia ya hadi wa kuchambua 10tones.

Kwa hiyo. Tatizo ni watu wetu kuwa matapeli na kukosa. Mfano, yule katibu mkuu wa wizara. Le professier aliyetumbuliwa alikuwa anafanya uchakachuzi wa documents zinazoletwa wizarani pale.

Kwa hiyo, PM anahusika sana katika mazingira kama hayo.

Pia, nina wasiwasi sana na mleta mada unaweza ukawa mpiga deal au mfanyabiashara wa mchanga kwenda nje ya nchi.
 
kikubwa wanatakiwa kufanya chochote wanachodhani ni sahihi kwa faida ya wengi.
Kama hizo sample zimekuwa zikichukuliwa na government officials na maelezo yao hayaaminiki ni afadhali wachukue na wakuu ili majibu yakipatakina utata uishe...
Una uhakika?
 
Una uhakika?
hakika ya nini mkuu. iko wazi hairuhusiwi huo mchanga kutoka bila uwepo wa mwakilishi wa wizara MEM, TMAA na TRA ili wakokotoe na Royality yetu baada ya kujua ni kiasi gani kimo.

Sample nne huchukuliwa. Moja ya serikali/TMAA, Nyingine inabaki kwa Mwekezaji,Nyingine inasafirishwa na mzigo kwa mchenjuaji/smelter na Moja inabaki incase wakitofautiana popote itumike kama reference. Yote yanafanyika kwa transparency hayo ni maelezo kutoka kwa wahusika na hayajapingwa popote, na sio siri ni procedure. Ndio maana ni vzuri na PM ajiridhishe kwa upande wake ili kuondoa utata @@Salary Slip
 
Midimu, onywanoko! CAG kasema hajaona pato lolote la madini, kesho yake katibu mkuu MEM akatengeneza zengwe la kumpeleka ndugai bandarini na siku hiyohiyo akafutwa kazi. Hujiulizi? Hujiulizi Muhongo anavyopenda camera za waandishi hajaonekana kabisa kwenye gogoro la mchanga utadhani katumwa kutibiwa India.

Kwa taarifa yako marahaba yote hailipwi TRA, inaliwa pale MEM. Ndio maana hakuna hata mmoja anayethubutu kusema hiyo marahaba tumeshavuta ngapi, pamoja na makontena kuwa na seal za TRA.
 
Mwekezaji kasema hayo majitu yalikuwa yanamwingizia bilioni arobaini kwa wiki, tra tuambieni mnalipwa ngapo kama marahaba? Naimani JPM nae kauliza swali kama mimi na ndio maana ndani ya wiki moja boss wa TRA na MEM wote wametimuliwa na Muhongo kajificha ukara anafunga umeme wa sola.
 
Hivi Waziri Mkuu alikwenda Buzwagi kwa lengo la kufanya ziara au lengo hasa lilikuwa kuchukua mchango?

Kama ni kuchukua mchanga,hilo kweli ni jukumu la Waziri Mkuu?

Au ndio tutaambiwa swala la kuchukua mchanga limeibuka tu wakati wa ziara hiyo na halikuwa kwenye agenda?

Mimi mbona hapa sielewielewi!!
Sasa atafanya kazi wakti kazi hamna,ndio mana unamuona buzwagi kutuandalia sinema mpya kma kawaida yao.si unajua wote na pogba wazee wa comedy
 
JPM Komaaa Babaaa .
Jamaa wametokeza kwenye TV eti makontena ni yao. Wamechakaa wala hawafanani kabisaa.
Dawa ni kutoza kodi kisawasawa ili hiyo biashara isilipe.
Ianzishwe kodi mpya ya mchanga. Toza kwelikweli. Ebo !!
 
Back
Top Bottom